KikulachoChako
JF-Expert Member
- Jul 21, 2013
- 19,185
- 37,239
Kweli maisha ni safari ndefu sana......
Nimekumbuka kisa kimoja miongo kadhaa nyuma.....wakati najitafuta nilijikuta nimepata hifadhi kwa Kaka yangu( Mola amrehemu).........Shemeji ilionekana hakuridhia uwepo wangu pale ingawa nilikuwa muda mwingi sipo nyumbani.....
Niliyajua hayo kupitia matendo yake maovu dhidi yangu kama vile kuninyima chakula....na kunifungia mlango ili nilale nje kipindi ambacho kaka amesafiri kikazi.......
Nikavunja ukimya na kumwambia kaka baada ya kuona mambo yanazidi kuwa magumu.....hapo ndio nilijua nguvu ya Shem kwenye nyumba ile.......
Sikujua kaka alifikisha ujumbe wangu kwa njia ipi lakini asubuhi baada ya kaka kwenda kazini... Shem alinifata na kuniambia kuwa..."Wewe unaongea na kaka yako mkiwa mmevaa nguo....mimi naongea na kaka yako nikiwa UCHI...je atamsikiliza nani..."
Nashukuru Mungu baada ya siku kadha kaka alinipangishia chumba cha bei chee maeneo ya manzese na kunihudumia hela ya matumizi mpaka nilipoweza kusimama mwenyewe kimaisha......
NILICHOJIFUNZA......
KUISHI KWENYE FAMILIA ZA WATU UNATAKIWA UWE MPOLE HUKU UKIPAMBANA UONDOKE HAPO HARAKA IWEZEKANAYO ILI AMANI IWEPO KATI YAKO WEWE NA NDUGUYO.....