Mkuu wanawake so wakudhaminika..
Mm bro alienda mkoa fulani kikazi yeye ni fundi furniture.
Alikaa kwa muda pasi na kumtumia Hela shemeji, hivyo nikapata taarifa Kwa shemeji kama mdogo mtu.
Bro alipokua anaondoka aliacha Kuna meza imeandaliwa Bado kuuzwa tu.
Mm nikamwambia shemeji unaonaje tuuze hii meza upate mahitaji hata kiasi, shemeji akalibariki wazo.
Siku nimepata mteja naenda nae Kwa bro nikakuta shemeji ameficha meza na kabadilika, nikauliza vipi?
Akanambia meza hamna nimeuza tayari nikasema poa nikapiga chini
Kumbe alikuwa amempigia bro kamwambia mdg wako anataka kuuza meza eti anakudai Hela.
Aisee Kwa ufupi bro si mzungumzaji sana na tuliongea kiume.
Ila shemeji nilimfuata nikawasha full na mpaka Leo Sina ukaribu nae mkubwa.