Shemeji; Mimi naongea na Kaka yako nikiwa sina nguo, tuone atamsikiliza nani

Rafiki yangu aliambiwa hivi;
Shemeji, tutakusaidia mpaka lini? Jiongeze basi utoke!
 
Nje ya mada kidogo:
Hivi huwa inakuwaje mwanaume timamu anatawaliwa na mke wake wandugu?.

Ila kaka yako alikuheshimisha sana Mkuu, hakutaka mambo yawe mengi.
Mara nyingi inakuwa sio mtu katawaliwa bali anaepuka matatizo ili kuinusuru familia maana anajua hawa wenzetu huwa wanafanya maamuzi kwa mihemko lakini baadae hujutia....maamuzi magumu hufanyika kama wakivuka mipaka......

Kaka alikuwa anamuelewa mkewe roho yake na hakutaka kuongeza mgogoro.....alifanya maamuzi ya kiume Sana.....
 
Kaka Yako licha ya kufikisha ujumbe,alifanya jambo la maana kukupangishia chumba kwani aliona mbele mambo yataharibika
Alifanya jambo la maana na nilikuja kumuelewa baadae sana.....

Kuna umri ukifikia automatically unahitaji amani na utulivu ili kuijenga kesho njema ya familia yako......

Ni wakati ambao mwanaume anaonekana kuyapuuzia mambo mengi sana na wakati mwingine kuonekana mjinga.....lakini akivuka hali hiyo ndio huwa yanapita maamuzi magumu ili kudumisha amani ya moyo wake...
 
Shemeji yako alikua ana tabia za kibinadamu za kawaida tu!

Bro wako alikua na akili kubwa sana, ila binafsi naona angekufanyia maarifa ya room kimya kimya bila kumdokeza chochote mke wake

Kuna mashemu ni mashetani
Suala la yeye kunitafutia chumba nadhani hakumuambia mkewe alifanya kimya kimya....hata mimi aliniambia baada ya kuwa ameshalipa Kodi na kuweka fenicha kadhaa za kuanzia maisha.....nadhani ulikuwa mpango wake tangu nafika pale
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…