Shemeji yangu amekataa! Abadani, Mwanangu hapimwi DNA ikibidi ndoa ivunjike tu

Shemeji yangu amekataa! Abadani, Mwanangu hapimwi DNA ikibidi ndoa ivunjike tu

Nimesoma genetics, hakuna kitu kama hicho.
Genotype ndo inajenga phenotype, anaweza asifanane Kwa asilimia 90%, ila lazima kuwe na 10% la sivyo uwe hujachangia chromosomes.
Acha upotoshaji.

Wewe umesoma genetic, lkn wengine tumesoma na kujionea.
 
Hata wewe ukiwa na Familia jitahidi kuchukulia mambo poa, utawin!! Mkuu itakusaidia nini endapo utajua kuwa sio mtoto wako lakini amezaliwa nyumbani kwako?

Hii inashida gani? hata kama sio wa kwako na ukamlea tu
Mkuu uhangaike na mtoto si wako? Biblia inakataa kubebe geneology isiyoyako.

Ndio maana wazee wanajiua mwishoni baada ya kujua mtoto aliye mhangaikia hakuwa wake na Mama alificha.

Ukumbuke Kiroho iko hivi. Mtoto kama si wako ukamlea kwa kudanganywa ni wako. Hata kama unampenda kivipi siku atakayogundua Baba yake wa Damu sio wewe na ni mwingine atakushangaza na wala usilaum ni Nature.
 
Hahitaji hata kumwambia au ruhusa ya mwanamke kupima DNA, nywele au mate ya mtoto yanamaliza kila kitu 100%, akipata majibu yasiyofaa uamuzi wa kuvunja au kuendelea ni wa kwake
 
Asee mbna kaz ipo.
Aje huku ndungu Kuna Mtaalam wa DNA za kienyeji, hapo haihitajiki hata mtoto kuwepo.

Na usikute mtoto wa mtoa mada rafiki. Ko kaka yako ajiandae na Majibu yotee🤣😲
Na huku Kwa Fundi wetu utaambiwa Hadi baba halisi wa mtoto.
 
Nimesoma genetics, hakuna kitu kama hicho.
Genotype ndo inajenga phenotype, anaweza asifanane Kwa asilimia 90%, ila lazima kuwe na 10% la sivyo uwe hujachangia chromosomes.
Acha upotoshaji.
Umesoma lin mkuu, ktabu gan?
 
Wakuu tumefika mwisho. Tumekuwa watabe kushauri kwenye mahusiano ya wengine huku mtandaoni lakini huku field Mke wa Brother(rafiki yangu wa longtime) ametushinda.

Ni hivi Mwaka Jana Mke wa Huyu Best Yangu alijifungua mtoto wa kiume. Tulifurahi kupata mtoto wapili na sisi kama ndugu na jamaa wa karibu sana ukizingatia yeye jamaa alinisaidi sana kusoma enzi hizo kipesa na kimawazo basi tulimfanyia Tafrija ndogo ya kupata mtoto.

Siku chache baadae furaha ya jamaa iliingia shubiri kila alipokuwa akifatilia ukuaji wa mtoto.

Yaani mtoto amekuwa na sura na mwonekano tofauti na Baba na Mama yake.

Yaani Mshikaji ni Mweusi na Mke wake maji ya kunde lakini Mtoto ni Mweupe.

Kwa sayansi ndogo tuliyo nayo kama baba mweusi na Mama maji ya kunde sio rahisi kupata mtoto mweupe. Pengine angepata rangi ya kunde kama Mama yake au Mweusi kabisa kama Baba yake.

lakini Baba ni msomi hawezi kufanya maamuzu based on just feelings. Ameamua kushauriana na mkewe kuwa wakampime DNSA maana jamaa roho inakataa kumpenda mwanaye kati kati ya mashaka.

Mke amekataa kata kata kuwa Mwanaye hapimwi DNA ikibidi hata ndoa ivunjike.

Ana dai kama hamwamini mke wake basi bora waaachane.

Mimi na Braza tume baki mdomo wazi juu ya msimamo wa Mwanamama huyu.

Tulitegemea angekubali ili kumwondolea hofu mumewe na upendo uzidi kutamalaki. Hali imekuwa tofauti.
Uyo mtoto ana umri gan mpk sas?
 
Back
Top Bottom