Shemeji yangu amekataa! Abadani, Mwanangu hapimwi DNA ikibidi ndoa ivunjike tu

Shemeji yangu amekataa! Abadani, Mwanangu hapimwi DNA ikibidi ndoa ivunjike tu

Wakuu tumefika mwisho. Tumekuwa watabe kushauri kwenye mahusiano ya wengine huku mtandaoni lakini huku field Mke wa Brother(rafiki yangu wa longtime) ametushinda.

Ni hivi Mwaka Jana Mke wa Huyu Best Yangu alijifungua mtoto wa kiume. Tulifurahi kupata mtoto wapili na sisi kama ndugu na jamaa wa karibu sana ukizingatia yeye jamaa alinisaidi sana kusoma enzi hizo kipesa na kimawazo basi tulimfanyia Tafrija ndogo ya kupata mtoto.

Siku chache baadae furaha ya jamaa iliingia shubiri kila alipokuwa akifatilia ukuaji wa mtoto.

Yaani mtoto amekuwa na sura na mwonekano tofauti na Baba na Mama yake.

Yaani Mshikaji ni Mweusi na Mke wake maji ya kunde lakini Mtoto ni Mweupe.

Kwa sayansi ndogo tuliyo nayo kama baba mweusi na Mama maji ya kunde sio rahisi kupata mtoto mweupe. Pengine angepata rangi ya kunde kama Mama yake au Mweusi kabisa kama Baba yake.

lakini Baba ni msomi hawezi kufanya maamuzu based on just feelings. Ameamua kushauriana na mkewe kuwa wakampime DNSA maana jamaa roho inakataa kumpenda mwanaye kati kati ya mashaka.

Mke amekataa kata kata kuwa Mwanaye hapimwi DNA ikibidi hata ndoa ivunjike.

Ana dai kama hamwamini mke wake basi bora waaachane.

Mimi na Braza tume baki mdomo wazi juu ya msimamo wa Mwanamama huyu.

Tulitegemea angekubali ili kumwondolea hofu mumewe na upendo uzidi kutamalaki. Hali imekuwa tofauti.
Anatafuta demokrasia ili iweje. Achukue kucha tu za mtoto, mkapime wenyewe. Akishapata majibu ndo maamuzi yafate. Now mwanamke ana kiburi coz anajua hamjapima bado.
 
Wakuu tumefika mwisho. Tumekuwa watabe kushauri kwenye mahusiano ya wengine huku mtandaoni lakini huku field Mke wa Brother(rafiki yangu wa longtime) ametushinda.

Ni hivi Mwaka Jana Mke wa Huyu Best Yangu alijifungua mtoto wa kiume. Tulifurahi kupata mtoto wapili na sisi kama ndugu na jamaa wa karibu sana ukizingatia yeye jamaa alinisaidi sana kusoma enzi hizo kipesa na kimawazo basi tulimfanyia Tafrija ndogo ya kupata mtoto.

Siku chache baadae furaha ya jamaa iliingia shubiri kila alipokuwa akifatilia ukuaji wa mtoto.

Yaani mtoto amekuwa na sura na mwonekano tofauti na Baba na Mama yake.

Yaani Mshikaji ni Mweusi na Mke wake maji ya kunde lakini Mtoto ni Mweupe.

Kwa sayansi ndogo tuliyo nayo kama baba mweusi na Mama maji ya kunde sio rahisi kupata mtoto mweupe. Pengine angepata rangi ya kunde kama Mama yake au Mweusi kabisa kama Baba yake.

lakini Baba ni msomi hawezi kufanya maamuzu based on just feelings. Ameamua kushauriana na mkewe kuwa wakampime DNSA maana jamaa roho inakataa kumpenda mwanaye kati kati ya mashaka.

Mke amekataa kata kata kuwa Mwanaye hapimwi DNA ikibidi hata ndoa ivunjike.

Ana dai kama hamwamini mke wake basi bora waaachane.

Mimi na Braza tume baki mdomo wazi juu ya msimamo wa Mwanamama huyu.

Tulitegemea angekubali ili kumwondolea hofu mumewe na upendo uzidi kutamalaki. Hali imekuwa tofauti.
Mwambie brother yako achukue nywele za mtoto na zake zinatosha kuwa sampuli
 
Bado hujawajua wanawake that's why unatoa comment based on feelings.

Sio kujua wanawake reference tunayo hapa na mfano halis upo [mention]DeepPond [/mention] yeye ana mtoto wa njee je vipi siku akisikia kwa ndugu kuwa mtot wa kwaza wa mkewe anae amini ndio mtoto wake wa kwaza siyo wake pamoja na wapili atafanyaje na yeye ilihali ana mtoto njee?

Kuna muda ukweli lazima usemwe ww kama mkeo angekuwa ashiki mimba si unge hamisha kambi kimya kimya?
 
Mbona rahis sana. Kulikuwa hakuna haja ya kutangaza, inafanywa kimya kimya yanaouja onyeshwa majibu
Kwa Tanzania hilo haliwezekani, lakini kwa nchi za Ulaya na Marekani inawezekana.

Hapa Tanzania ili upate vipimo vya DNA ni laziima uwe na vibali maalumu. Kiufupi, kuna mlolongo mrefu sana. Mashine zenyewe zinamilikiwa na Serikali, chini ya Mkemia mkuu.
 
Man kuna namna ya kufanya kimya kimya. Hizi mission nzito huwa zinafanyika bila hata mzazi kujua. Wahusika tu wasijue lolote, aje tu kupewa majibu.

Si rahis mtu kukwepa majibu yenye udhibitisho
Siyo rahisi kama unavyodhani mkuu. Mamlaka ya kupima DNA yamekasimishwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali. DNA haipimwi bila amri ya Mahakama au maombi ya Wakili.

Sasa umchukue mwenza wako hobelahobela umpeleka kwa Mkemia Mkuu halafu asihoji kuna nini kinaenda kutendeka huko? Labda awe layman/laywoman, otherwise haiwezekani!

Na ni kosa kisheria kwenda kupima DNA bila consent ya wazazi wote wawili isipokuwa kama amri imetolewa na Mahakama, labda kama maombi yatapelekwa na Wakili, na wote wawili mkawa mmekubaliana.
 
Mwambie jamaa aache kuvuruga familia yake. Mwambie Kitanda hakizai haramu. Ampende mtoto, ampende na mke wake.
 
Sijui sheria za hapa sinasemaje ila nchi nyingine kama ww ni baba uliopo kwneye cheti cha kuzaliwa cha mtoto huitaji ruhusu ya mama kufanya "partenity" dna test. Kwasabbu unachopima ni ili kujua ikiwa ww ni baba wa kibiolojia. Kwahivyo kisheria unaweza kuufanya mchakato kimya kimya ukapata majibu ili uamue cha kufanya.
 
Why yawe ya uongo?
Sheria inasema majibu yatolewe kwa kuzingatia ustawi wa ukuaji wa mtoto, kwa muktadha huo lazima uambiwe wewe ndio baba wa mtoto kwani tayari sheria imewaelekeza hivyo, labda kama mpo wawili mnaogombea mtoto na pia lazima waangalie anaejiweza ndio anapewa mtoto
 
Hiyo sasa ni maabara au utopolo?? Hakuna maabara za hivyo zinaweza kupindishe geneology ya mtu kwa maslahi ya kulea mtoto kisa una uwezo.
 
Back
Top Bottom