Watu ambao wamefilisika akili za maisha ndio huja na hizi hoja ili wapate uhalali katika jamii wanayoishi waonekane nao wana malengo au shughuli fulani.
Sasa nikikuuliza hapo unachokitafuta ni nini unaweza kunambia?!
So hiyo kalenda inakuzuia nini kufanya maisha yako au inakubugudhi nini hadi ushindwe kuishi kama wanadamu wengine?!
Ni dhahiri kichwa chako kimejazwa na hofu ya maisha na pengine kuna mambo hayakuendei sawa sasa unajaribu kutafuta sehemu ya kutolea hasira zako za maisha.
Sikiliza Dogo (nakuita dogo kwa makusudi iwe una umri mdogo au upo na miaka 50 wewe bado unaonekana haujakua kiakili kuongea vitu kama hivi), kwenye haya maisha usipokuwa na mfumo na mipangilio mizuri ya kuishi utabakia kuwa kama mwendawazimu.
Tuliza kichwa chako, tafakari njia zako, elewa vema mafunzo ya imani yako, tafuta pesa kwa uhalali, heshimu watu wengine ikiwamo imani kama vile wao ambavyo wanakuheshimu kisha uishi kwa utulivu sio ukorofi.
Achana na huo ujinga ujinga wa kalenda. Ingekuwa ni tatizo basi maisha yasingeenda kama vile unavyoyaona leo hii.