Sherehe ya Mwaka Mpya ni ya Kikristo, Waislamu tumeivamia tu bila kujua

Sherehe ya Mwaka Mpya ni ya Kikristo, Waislamu tumeivamia tu bila kujua

Hii kalenda tunayotumia,Gregorian Calendar ilikuja baada ya Julian Calendar, zote zina uhusiano na Issa ndio maana utakuta maneno kama AD au BC yote yanamrefer Nabii Issa.

Sasa sisi Waislam imekuwaje hatulijui hili au kufuata mkumbo? au ndio dunia inaongozwa na mfumo Kristo?

Hili jukwaa libadilishwe jina liitwe jukwaa la la kuusema ukristo. Yani, asilimia kubwa za mada ni kuusema Ukristo.
 
Watu ambao wamefilisika akili za maisha ndio huja na hizi hoja ili wapate uhalali katika jamii wanayoishi waonekane nao wana malengo au shughuli fulani.

Sasa nikikuuliza hapo unachokitafuta ni nini unaweza kunambia?!

So hiyo kalenda inakuzuia nini kufanya maisha yako au inakubugudhi nini hadi ushindwe kuishi kama wanadamu wengine?!

Ni dhahiri kichwa chako kimejazwa na hofu ya maisha na pengine kuna mambo hayakuendei sawa sasa unajaribu kutafuta sehemu ya kutolea hasira zako za maisha.

Sikiliza Dogo (nakuita dogo kwa makusudi iwe una umri mdogo au upo na miaka 50 wewe bado unaonekana haujakua kiakili kuongea vitu kama hivi), kwenye haya maisha usipokuwa na mfumo na mipangilio mizuri ya kuishi utabakia kuwa kama mwendawazimu.

Tuliza kichwa chako, tafakari njia zako, elewa vema mafunzo ya imani yako, tafuta pesa kwa uhalali, heshimu watu wengine ikiwamo imani kama vile wao ambavyo wanakuheshimu kisha uishi kwa utulivu sio ukorofi.

Achana na huo ujinga ujinga wa kalenda. Ingekuwa ni tatizo basi maisha yasingeenda kama vile unavyoyaona leo hii.
 
Badala ya kuhuzunika umesogea siku kadhaa kaburini unafikiria party [emoji3060]

Kusherehekea siku kama hizi na nyingine ni biashara kubwa sana na watu wwnatengeneza hela haswa

Majuzi kabla ya Xmas aliulizwa jamaa mmoja mwenye shamba la miti akasema ameuza miti ya Xmas 24,000 na bei zake kuanzia £60 (170,000) mpaka £120 (340,000 ya madafu kila mti
Sasa hiyo ndio biashara na bado card na booze
Leo unafurahia siku mpya kwani jua limetokea kwingine zaidi ya maumivu ya dhiki na Ada zikiwasubiri na hela zimeisha kwa kuwanufaisha wengine

New year ni kama siku nyingine tu ila ni bank holiday kwa baadhi ya nchi
 
Hii kalenda tunayotumia,Gregorian Calendar ilikuja baada ya Julian Calendar, zote zina uhusiano na Issa ndio maana utakuta maneno kama AD au BC yote yanamrefer Nabii Issa.

Sasa sisi Waislam imekuwaje hatulijui hili au kufuata mkumbo? au ndio dunia inaongozwa na mfumo Kristo?
Pengine wewe ndiye ulikuwa hujui au huelewi.
 
Back
Top Bottom