Elections 2010 Sherehe za kumuapisha Rais JK - Uhuru stadium DSM

Elections 2010 Sherehe za kumuapisha Rais JK - Uhuru stadium DSM

anawashukuru akina slaa na wenziwe kwa kuwachangamsha katika kipindi cha kampeni na kuwafanya wafanye kazi zaidi
 
wanashukuriwa wapnzani kwa kuwachangamsha ccm! hahaha yaani Slaa kamchangamsha tu Kikwete ......
 
anashukuru kuwa kutokana na mchangamsho huo kua kazi ya kukuza demokrasi

na kusisitiza kua yaliopita si ndwele tugange yajayo


kazi iliopo na kujitahidi kushirikiana kutibu majeraha tulioisababishia nchi
 
baadhi ya maeneo anasema kulipindikizwa chuki za kidini na anasema kazi ya ccm ni kurejesha taifa katika hali ilio mwanzo
 
nitabaki kuwa mwanaCHADEMA, naamini Dr Slaa kashinda uchaguzi huu. hata km watu wote watahongwa na CCM nitabaki CHADEMA peke yangu na 2015 nitaipigia kura tena CHADEMA. kama walivyo washabiki wa liverpool very royal to their club ingawa mie sio mshabiki wa liverpool ndivyo nilivyo kwa CHADEMA, I WILL NEVER WALK ALONE! hence CHADEMA WILL NEVER WALK ALONE!
Tupo pamoja. Kama mimi nimeendelea kuipenda liverpool pamoja na kuboronga kwake msimu huu basi nataendelea kuwa mwana Chadema mwaminifu daima. Mbele kwa mbele nyuma mwiko
 
Anaisifu Tume iliyo mbeba kuwa Rais. Sifa tupu
 
anawasisitiza viongozi wa vyama na wote wanaoitakia mema nchi yetu kuijenga nchi yetu na kutoendelea kuishi katika migawanyiko iliosababishwa na uchaguzi na anasema kua tanzania ilikua inasifia kua ni kisiwa cha amani ambao hali hio isiharibiwe


pia anaishukuru sana tume kwa kazi nzuri walioifanya kwa kusimamia vyema zoezi la uchaguzi tokea mwanzo hadi mwisho
 
Wana JF naomba mnijulishe kama kuna Ofisi za Chadema UK na ziko wapi nikachukue kadi kabisa. Jamaa zangu wengi hapa ni wale wa kujikomba CCM na sitaki kuwauliza.

Usifuate mkondo wa ccm huko ukerewe. chadema ni chama cha watanzania. Kwanza cameron amesema anafuatilia hao watu wanaopractice siasa za nchi nyingine hapo UK.
 
Tupo pamoja. Kama mimi nimeendelea kuipenda liverpool pamoja na kuboronga kwake msimu huu basi nataendelea kuwa mwana Chadema mwaminifu daima. Mbele kwa mbele nyuma mwiko


hizi ahadi za kuwa mwaminifu kwa chama daima ndio zinazotufikisha hapa tulipo.

chadema si mama yako..........
 
anaahidi kushughulikia kasoro ndogo ndogo zilizojitokeza kwenye uchaguzi

anawashukuru wana usalama na kuwataka kutomruhusu yeyote kuvuruga amani ya nchi


na anashukuru kwa gwaride zuri la JWTZ
 
Tupo pamoja. Kama mimi nimeendelea kuipenda liverpool pamoja na kuboronga kwake msimu huu basi nataendelea kuwa mwana Chadema mwaminifu daima. Mbele kwa mbele nyuma mwiko

Mkuu vipigo alivyopigwa liverpool havikuchakaliwa. Vilikuwa vipigo halali tofauti na chadema. Kulinganisha liverpool na chadema unalidhalilisha chama. teh teh teh
 
nina maana alipofika kwa Salma angemkumbatia na kumpa mabusu yenye bashasha, mbwembwe na madoido
Ya nini hayo mbele ya kadamnas.Si wana nyumba yao iliyozibwa kwa kuta na mapazia.
Halafu pale hata watoto wanaangalia!.
Utamaduni wa kizungu hautufai sie.
 
baadhi ya maeneo anasema kulipindikizwa chuki za kidini na anasema kazi ya ccm ni kurejesha taifa katika hali ilio mwanzo
CCM ndio ilipandikiza chuki kwa kutumia magazeti yake ya Uhuru, Mzalendo, Sauti Huru, Changamoto, Jambo Leo, Rai na Ntan
 
anamalizia kwa kuwashukueu kamati ya mapambo na sherehe


na anawashukuru masheikh na mapadri kwa dua zao


na anategemea dua zao mungu atazikubali ili maendeleo kwa kasi zaidi

pia anataka tujitahidi kufanya kazi kwa bidii ili tuweze kuifikisha Tanzania yenye neema tele


ana malizia kwa kusema asanteni kwa kunisikiliza
 
Jamaa kaapa kwa katiba,swala la huyu dogo ridh1 linasikitisha.Lakini lawama ni ya baba ndiye anayeruhusu hayo mambo,Nyerere alikuwa na watoto,Mwinyi pia Mkapa htujawahi ona.Kina Nyerere tunawasikia wanaibuka sasa hivi kwa juhudi zao.Je huyu jamaa naona anatupeleka kwenye utawala wa kifalme ndio maana ridh1 anapata treatment kama price.
 
FISADI Rostam Aziz yupo "row" ya pili nyuma ya JK hapo jukwaani - anachekelea tu - anaanza kuitafuna KEKI YETU rasmi!
 
JK atahudumia muda si mrefu kuna watumbuizaji kama Marlaw, Msondo Ngoma na wasanii wa THT no wonder Kusanga and the company wanajikomba kinoma kwa JK
Wee nawe leo!!
 
Back
Top Bottom