Sijui kuhusu sheria inasemaje kwa hapa kwetu ila inawezekana kutengeneza pombe nyumbani ila kwa kigezo hichi.. pombe aina ya wine na beer hutengenezwa kupitia process ya fermentation ambayo hii ni rahisi tu mtu anaweza jufanya hata nyumbani kwake fresh tu ikiiva unakuwa unajimwaya mwaya mwenyewe!.
Ila kwa pombe aina ya spirits ukishafanya process ya fermentation utahitaji kuifanyia Distillation process ili iwe spirit na hii process inahitaji mtambo na utaalum kwaajili yakufanya hivyo, sasa kwa hili hapa ndio serikali huingia sasa maana huu mchakato bila utaalum unaweza kutengeneza sumu badala ya pombe!.
vilevile huo mtambo wakufanyia Distillation lazima ukaguliwe uwe na viwango stahiki na usiweze kuleta shida!.
Kwa pombe za usindikaji (fermentation) unaweza kutengeneza nafikiri kwa matumizi yako tu ila ukianza kufanya biashara, hapo ndo nafikiri mkemia mkuu lazima aje afanye ukaguzi na atoe go ahead, na akishatoa go ahead ndo utaanza kukutana na akina wazee wa kodi TRA na wengine wengine huko wanaohusika na hayo mambo!.
wanasheria nao watakuja kumalizia sasa mimi naishia hapo.