Sheria inasemaje kuhusu mtu kujitengenezea pombe ya kunywa nyumbani?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
11,884
Reaction score
21,175
Wakuu Sheria yetu inasemaje kuhusu mtu kujitengenezea hombwa ya kunywa home? Nchi kama US nyumba inaruhusiwa kutengeneza hadi lita 1000 kwa mwaka. Hapa Tz muongozo ukoje? Na vipi mtu akifungua baa na kutengeneza bia yake hapo hapo?
 
Actually hii idea nimekuwa nayo mda mrefu ,hii nchi za wenzetu kama USA waita craft beer , unakuta bar wanatengeneza pombe zao na spirits au wine wanazipa majina na rated zao unique kwa ajili ya customer wao wanaofika hapo , kama tunavyotengeneza pombe za kienyeji tu kitaa , sema hizi craft beer and spirits unatumia vifaa vya kisasa na usafi zaidi .Ila kwa hawa vinyamkera na bandits wetu wa hapa wanaojiita serikali utapewa kesi ya uhujumu uchumi
 
Ikikuletea madhara utashitakiwa kwa jaribio la kutaka kujiua na kumiliki vinywaji visivyozingatia sheria za mamlaka ya dawa na vyakula. Ole wako
 
Sijui kuhusu sheria inasemaje kwa hapa kwetu ila inawezekana kutengeneza pombe nyumbani ila kwa kigezo hichi.. pombe aina ya wine na beer hutengenezwa kupitia process ya fermentation ambayo hii ni rahisi tu mtu anaweza jufanya hata nyumbani kwake fresh tu ikiiva unakuwa unajimwaya mwaya mwenyewe!.

Ila kwa pombe aina ya spirits ukishafanya process ya fermentation utahitaji kuifanyia Distillation process ili iwe spirit na hii process inahitaji mtambo na utaalum kwaajili yakufanya hivyo, sasa kwa hili hapa ndio serikali huingia sasa maana huu mchakato bila utaalum unaweza kutengeneza sumu badala ya pombe!.
vilevile huo mtambo wakufanyia Distillation lazima ukaguliwe uwe na viwango stahiki na usiweze kuleta shida!.

Kwa pombe za usindikaji (fermentation) unaweza kutengeneza nafikiri kwa matumizi yako tu ila ukianza kufanya biashara, hapo ndo nafikiri mkemia mkuu lazima aje afanye ukaguzi na atoe go ahead, na akishatoa go ahead ndo utaanza kukutana na akina wazee wa kodi TRA na wengine wengine huko wanaohusika na hayo mambo!.

wanasheria nao watakuja kumalizia sasa mimi naishia hapo.
 
Mbona mimi najitengenezea wanzuki hapa home najinywea zangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…