KERO Sheria inayompa mamlaka makubwa DPP, kuwa apeleke au asipeleke kesi mahakamani, ni mbaya na inafaa ifutwe

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Miongoni mwa sheria mbovu sana zilizopo nchini ni inayompa mamlaka DPP ya kuweza kupeleka au kutopeleka kesi yoyote ya jinai, inayomkabili mwananchi yeyote na asitoe sababu za kutoipeleka kesi yoyote Ile mahakamani!

Hii ni sheria mbovu sana, ambayo ilitungwa Kwa nia ya kuwafanya baadhi ya wananchi kuwa ni "untouchables"

Nalielezea hili baada ya Jeshi la Polisi, kutamka hadharani, kuwa limeshakamilisha uchunguzi wake wa kesi inayomkabili yule Mama anayetambukika Kwa jina la "afande" na wamelipeleka jalada la kesi hiyo Kwa DPP, Ili eti aamue kuipeleka au kutoipeleka kesi hiyo mahakamani!

Hivi Kwa kosa kubwa kama hili la kuagiza vijana watano waende wakambake yule Binti Kwa kile kinachoitea " rape gang" ambayo Kwa Kila mwananchi aliyesikia huu mkasa anahuzunika sana, sasa inashangaza kusikia kuwa Jeshi la Polisi, limeshakamilisha upelelezi wake, lakini limepeleka jalada la kesi hiyo Kwa DPP, Ili akiamua apeleke kesi hiyo mahakamani na vile vile akiamua asiipeleke kesi hiyo mahakamani na hakuna raia yeyote mwenye mamlaka ya kumuhoji, Kwa nini hajapeleka kesi hiyo mahakamani!😚

Hii sheria ni mbovu sana, ambayo ilitungwa maalum Kwa kuwakinga baadhi ya watu mashuhuli nchini, Ili hata wakitenda makosa makubwa ya jinai ya aina Gani, Ili wajue kuwa wanayo kinga Kwa DPP.

Eti sheria hiyo imempa mamlaka hayo ya kupeleka au kutoipeleka kesi yoyote Ile na Wala asiulizwe sababu za kutoipeleka kesi yoyote mahakamani!

Hawa watawala wetu, wasitufanye sisi watanzania wote kuwa ni wajinga sana, kiasi Cha kututungia sheria za aina hiyo za ubaguzi wa dhahiri ambapo DPP ataangalia hadhi ya mtuhumiwa na kuamua kutoipeleka kesi yake mahakamani na kuamua kupeleka kesi za walala hoi pekee wasio na kinga hiyo ya DPP na kupeleka kesi zao mahakamani!

Hii sheria inaji-contradict na sheria mama ya Katiba ya nchi, inayosema kuwa watu wote nchini, wako sawa mbele ya sheria.

Nitoe wito Kwa waheshimiwa wabunge wetu, wapeleke muswada wa dharura Bungeni, Ili kuibadili sheria hii, ambayo inaonyesha upendekeo wa dhahiri Kwa watu wachache, wenye hadhi mbalimbali hapa nchini.

Mungu ibariki Tanzania
Sheria kama hizi huwa haziondoki labda kwa machafuko ya kumwaga damu, au mapinduzi ya kijeshi na wakaamua ipatikane katiba ya wananchi.
 
Bunge limepitisha visheria na mambo kibao,sijui kama wananchi wanayajuwa

Ova
 
Ni kweli awe na limitations,

Maana kuna uwezekano wa kuabuse powers alizonazo.

Checks and balances ni muhimu sio vyema mtu kuwa na absolute power.
 
Kama kauli hiyo inatolewa hata na wewe ambaye ni mwanachama mwaminifu wa chama Cha kijani, basi ujue kweli Hilo jambo halikubaliki katika jamii ya kitanzania😁
 
Miongoni mwa sheria mbovu sana zilizopo nchini ni inayompa mamlaka DPP ya kuweza kupeleka au kutopeleka kesi yoyote ya jinai, inayomkabili mwananchi yeyote na asitoe sababu za kutoipeleka kesi yoyote Ile mahakamani!

Hii ni sheria mbovu sana, ambayo ilitungwa Kwa nia ya kuwafanya baadhi ya wananchi kuwa ni "untouchables"

Nalielezea hili baada ya Jeshi la Polisi, kutamka hadharani, kuwa limeshakamilisha uchunguzi wake wa kesi inayomkabili yule Mama anayetambukika Kwa jina la "afande" na wamelipeleka jalada la kesi hiyo Kwa DPP, Ili eti aamue kuipeleka au kutoipeleka kesi hiyo mahakamani!

Hivi Kwa kosa kubwa kama hili la kuagiza vijana watano waende wakambake yule Binti Kwa kile kinachoitea " rape gang" ambayo Kwa Kila mwananchi aliyesikia huu mkasa anahuzunika sana, sasa inashangaza kusikia kuwa Jeshi la Polisi, limeshakamilisha upelelezi wake, lakini limepeleka jalada la kesi hiyo Kwa DPP, Ili akiamua apeleke kesi hiyo mahakamani na vile vile akiamua asiipeleke kesi hiyo mahakamani na hakuna raia yeyote mwenye mamlaka ya kumuhoji, Kwa nini hajapeleka kesi hiyo mahakamani!😚

Hii sheria ni mbovu sana, ambayo ilitungwa maalum Kwa kuwakinga baadhi ya watu mashuhuli nchini, Ili hata wakitenda makosa makubwa ya jinai ya aina Gani, Ili wajue kuwa wanayo kinga Kwa DPP.

Eti sheria hiyo imempa mamlaka hayo ya kupeleka au kutoipeleka kesi yoyote Ile na Wala asiulizwe sababu za kutoipeleka kesi yoyote mahakamani!

Hawa watawala wetu, wasitufanye sisi watanzania wote kuwa ni wajinga sana, kiasi Cha kututungia sheria za aina hiyo za ubaguzi wa dhahiri ambapo DPP ataangalia hadhi ya mtuhumiwa na kuamua kutoipeleka kesi yake mahakamani na kuamua kupeleka kesi za walala hoi pekee wasio na kinga hiyo ya DPP na kupeleka kesi zao mahakamani!

Hii sheria inaji-contradict na sheria mama ya Katiba ya nchi, inayosema kuwa watu wote nchini, wako sawa mbele ya sheria.

Nitoe wito Kwa waheshimiwa wabunge wetu, wapeleke muswada wa dharura Bungeni, Ili kuibadili sheria hii, ambayo inaonyesha upendekeo wa dhahiri Kwa watu wachache, wenye hadhi mbalimbali hapa nchini.

Mungu ibariki Tanzania
kwahiyo wewe hapo mtu akitunga uzushi, usio na mashiko, akaupeleka kwa DPP akalazimisha wewe ushitakiwe, hutaki DPP awe na mamlaka kuamua kukushitaki au aseme hapa hamna ushahidi asikushitaki? unachotafuta hapo ni nini? na pia, kwa waliosoma sheria wote wanajua, DPP ni wewe mwenyewe (Jamhuri), anasimama badala ya wananchi wote nchini, hivyo dpp akishitaki ni jamhuri imeshitaki, yaani wewe umeshtaki, ungepeka mashauri hata yasiyo na maana yaende mahakamani asiwepo mtu wa kuamua kwa niaba ya jamhuri kwamba hili liende au hili linatupotezea muda au hili ni la maonezi? nilishapita huko nawajua.
 
Pascal, kwa bahati mbaya, waliounga mkono hoja hii wote sio wanasheria, wewe ukiwa mmojawapo (though najua ulisoma sheria). Hili suala lipo kwenye katiba, mipaka ya kipi DPP azingatie anapotaka kushitaki. kasome tu ibara ya 59 ya katiba. Pia, tulivyosoma chuo, DPP ni Jamhuri, na jamhuri haiwezi kuruhusu kila shitaka liende mahakamani, mengine yanapoteza muda tu hayana ushahidi, mengine ya maonezi, mengine yakutunga n.k, lazima awepo mtu wa kuamua badala ya wote, hatuwezi wote tukawa DPP anatuwakilisha tu. Paschal tulivyosoma chuo miaka ile, nadhani wewe ulitutangulia, ulimaliza 2007 udsm kama sikosei na lile pikipiki lako, (kidding) nakumbuka, tulikuwa wote, tulifundishwa haya, sisi wenzio tuliamua kuingia kufanya kazi hukohuko kwa DPP tukafahamu hayo yote kabla hatujaondoka, nadhani wewe pia kabla haujaja mtaani ulitakiwa upitie kwenye practice kwanza. samahani kama nimekukwaza.
 
Mkuu Yesu Anakuja , kwanza nimefurahi sana kujua kuwa niko humu na mdogo wangu wa UDSM sheria, ni kweli nilimaliza LL.B mwaka 2007 Dean akiwa Dr. Ibrahim Juma. Ni kweli nilikuwa biker na 2008 ile pikipiki imenifanya kitu mbaya.

Hongera kwa kufanya kazi Ofisi ya DPP.
Mimi ni muumini wa haki bin haki, baadhi ya mamlaka, sheria zetu, taratibu na kanuni sio za haki bin haki.

Moja ya mamlaka hayo ni ile mamlaka presidential preventive detention order, ya rais wa JMT anapoelezwa mtu fulani ni hatari kwa usalama wa Taifa, ana mamlaka ya kukukamata na kuwekwa kizuizini indefinitely bila kuambiwa kosa wala kufikishwa mahakamani. Kina Prof. Shivji, Kanywani, Mgongo Fimbo, Chris Peter, wakaichallenge kwa mandamus na sechorari, Mahakama Kuu ikatengua power hiyo na sasa Rais akimtia mtu kizuizini kwa sheria hiyo, has to give reasons na lazima mtuhumiwa afikishwe mahakamani.

Everything happens for a reason, mamlaka ya DPP kwenye Nolle bado yapo, DPP hapaswi kutoa sababu yoyote kwa yeyote na hakuna mamlaka ya kuhoji nolle!.

Naunga mkono kuwa kwenye Nolle DPP has to give reasons.
P
 
kwahiyo wewe hapo mtu akitunga uzushi, usio na mashiko, akaupeleka kwa DPP akalazimisha wewe ushitakiwe, hutaki DPP awe na mamlaka kuamua kukushitaki au aseme hapa hamna ushahidi asikushitaki? unachotafuta hapo ni nini? na pia, kwa waliosoma sheria wote wanajua, DPP ni wewe mwenyewe (Jamhuri), anasimama badala ya wananchi wote nchini, hivyo dpp akishitaki ni jamhuri imeshitaki, yaani wewe umeshtaki, ungepeka mashauri hata yasiyo na maana yaende mahakamani asiwepo mtu wa kuamua kwa niaba ya jamhuri kwamba hili liende au hili linatupotezea muda au hili ni la maonezi? nilishapita huko nawajua.
Hebu nieleze huyo mwendesha mashitaka alikuwa na ushahidi Gani wa ugaidi, Hadi aidhinishe Freeman Mbowe, ashitakiwe Kwa kosa kubwa la jinai la ugaidi??

Nikuuluze swali jingine, unaweza kuniambia, hivi ushahidi aliokuwa nao DPP "uliyeyuka" ghafla na kumlamisha yeye DPP aiondoe kesi hiyo ya ugaidi, iliyokuwa ikimkabili Mbowe??

Tuwe wakweli, nyinyi watawala wa CCM mkishirikiana na Jeshi la Polisi nchini na Mkurugenzi wenu wa mashtaka (DPP) mmezoea mno kuwabambikia kesi, hususani wapinzani wa "dizaini" ya Chama kikuu Cha upinzani nchini Cha Chadema!😗
 
Hata wakivunja tatizo lipo wapi, siku zinasonga na wanakula bata madarakani.

As long as wananchi aka wenye nchi wamelala fofofo kama ilivyo sasa tatizo litoke wapi.

Kutawala watu wasiojielewa huwa si kazi ngumu.
Shida ipo hapa
 
Mkuu Yesu Anakuja , kwanza nimefurahi sana kujua kuwa niko humu na mdogo wangu wa UDSM sheria, ni kweli nilimaliza LL.B mwaka 2007 Dean akiwa Dr. Ibrahim Juma. Ni kweli nilikuwa biker na 2008 ile pikipiki imenifanya kitu mbaya.

Hongera kwa kufanya kazi Ofisi ya DPP.
Mimi ni muumini wa haki bin haki, baadhi ya mamlaka, sheria zetu, taratibu na kanuni sio za haki bin haki.

Moja ya mamlaka hayo ni ile mamlaka presidential preventive detention order, ya rais wa JMT anapoelezwa mtu fulani ni hatari kwa usalama wa Taifa, ana mamlaka ya kukukamata na kuwekwa kizuizini indefinitely bila kuambiwa kosa wala kufikishwa mahakamani. Kina Prof. Shivji, Kanywani, Mgongo Fimbo, Chris Peter, wakaichallenge kwa mandamus na sechorari, Mahakama Kuu ikatengua power hiyo na sasa Rais akimtia mtu kizuizini kwa sheria hiyo, has to give reasons na lazima mtuhumiwa afikishwe mahakamani.

Everything happens for a reason, mamlaka ya DPP kwenye Nolle bado yapo, DPP hapaswi kutoa sababu yoyote kwa yeyote na hakuna mamlaka ya kuhoji nolle!.

Naunga mkono kuwa kwenye Nolle DPP has to give reasons.
P
DPP ni kada wa CCM
 
Hebu nieleze huyo mwendesha mashitaka alikuwa na ushahidi Gani wa ugaidi, Hadi aidhinishe Freeman Mbowe, ashitakiwe Kwa kosa kubwa la jinai la ugaidi??

Nikuuluze swali jingine, unaweza kuniambia, hivi ushahidi aliokuwa nao DPP "uliyeyuka" ghafla na kumlamisha yeye DPP aiondoe kesi hiyo ya ugaidi, iliyokuwa ikimkabili Mbowe??

Tuwe wakweli, nyinyi watawala wa CCM mkishirikiana na Jeshi la Polisi nchini na Mkurugenzi wenu wa mashtaka (DPP) mmezoea mno kuwabambikia kesi, hususani wapinzani wa "dizaini" ya Chadema!😗
DPP anasubiri maelekezo ya viongozi wa CCM ndiyo afanye kazi
 
Kwa maana hiyo hafai hata kidogo kuwa Kwenye nafasi hiyo ya DPP, Kwa kuwa katika kiapo chake, wakati anakabidhiwa madaraka hayo, aliapa kuwa atakitumikia cheo hicho Kwa usawa bila ya upendeleo Kwa mtu yeyote
 
Hata sisi huwa wanaapa na bibilia lakini wizi wanaofanya ni tofauti na viapo vyao, nani ameshitakiwa kwa kukiuka kiapo chake?
 
kwahiyo wewe hapo mtu akitunga uzushi, usio na mashiko, akaupeleka kwa DPP akalazimisha wewe ushitakiwe, hutaki DPP awe na mamlaka kuamua kukushitaki au aseme hapa hamna ushahidi asikushitaki? unachotafuta hapo ni nini? na pia, kwa waliosoma sheria wote wanajua, DPP ni wewe mwenyewe (Jamhuri), anasimama badala ya wananchi wote nchini, hivyo dpp akishitaki ni jamhuri imeshitaki, yaani wewe umeshtaki, ungepeka mashauri hata yasiyo na maana yaende mahakamani asiwepo mtu wa kuamua kwa niaba ya jamhuri kwamba hili liende au hili linatupotezea muda au hili ni la maonezi? nilishapita huko nawajua.
Hizi sheria wakati zinatungwa huwa mnakuja na maelezo haya ili kufanya ziweze kupita, lakini kiuhalisia huwa zinaacha mianya mikubwa hadi kutumika na kikundi hasa cha viongozi kutekeleza nia ovu. Ni nani asiyeona haya mamlaka ya DPP jinsi yanavyotumika kunyima haki za watu, na jinsi mamlaka haya yalivyogeuka kinga kwa viongozi wanasiofuata sheria? Acha kutetea uovu ukidhani kila sheria ni sheria halali kisa zimepitishwa na bunge.
 
Hata sisi huwa wanaapa na bibilia lakini wizi wanaofanya ni tofauti na viapo vyao, nani ameshitakiwa kwa kukiuka kiapo chake?
Hakuna aliyeshitakiwa Kwa kukiuka Kutii kiapo chake..............

Na hiyo inaanzia Kwa nafasi ya juu kabisa ya Rais wa nchi Hadi huku chini Kwa wasaidizi wake
 
Back
Top Bottom