Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Nimeweka hii snapshot inayoonesha muswada wa mabadiliko ya sheria ya chombo chetu cha Intelejensia.
Kwenye mapendekezo hususan kifungu cha 19 wanasema hapo kuwa, jinai inaweza kufanywa na TISS personels wakiwa wanatekeleza majukumu yao kwa uaminifu....
Jambo linalonistua ni kwamba, wengi hudhani jeshi kutawala ni mpaka pale jeshi linapopindua serikali ya kiraia. Huu muswada umeleta tafsiri mpya ya utawala wa kijeshi. Tufuatilie kwa akili kubwa sana haya mambo yanavyopangiliwa kwa uangalifu kuelekea imla ya kijeshi...
Nipate elimu kutoka kwenu wanaJF
- Kuna ukamilifu gani kwenye jinai?
- Kuna uaminifu gani kwenye jinai
- Kipimo gani kinatumika kufahamu kuwa jinai fulani imefanyika during utekelezaji wa majukumu kwa uaminifu
- Aina gani ya jinai inayoombewa mabadiliko? Ya kutesa au kuua?
- TISS ni jeshi au kitengo cha uraia kinachofanya shughuli za kijeshi? Sheria za kimataifa zinasemaje kuhusu utendaji wa jeshi kwa raia?
- Huu muswada nani wameomba hayo marekebisho yaani ni TISS au Rais (taasisi/sponsor)?
Kwa mahaba mema kwa nchi yangu, I submit
CC: Mzee Mwanakijiji Pascal Mayalla Retired raraa reree Extrovert Bujibuji Simba Nyamaume Mshana Jr zitto junior lumumbai Kiranga Erythrocyte mwanamwana MwanaWA Ebrania Gily Demi