Cannabis
JF-Expert Member
- Jan 20, 2014
- 11,557
- 33,535
Gaming Board of Tanzania (GBT) yenye jukumu la kusimamia uendeshaji wa michezo ya kubahatisha hapa nchini imesema kuwa kifungu Na. 52 cha sheria ya michezo ya kubahatisha ya mwaka 2003, pool tables zote zinatakiwa kusajiliwa ili kuwezesha uendeshaji wa mchezo huo kihalali.
Taasisi hiyo imesema kuendesha mchezo huo bila usajili ni kinyume cha sheria na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watakaokaidi agizo hilo.