Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015: Kwa mkakati huu wa Serikali, Watumiaji wa Mitandao tutapona?

Kama waliamua kutuletea hii sheria kwa nn walipunguza MB? Maana hapa wanatupa adhabu mara 2, ccm kweli ni janga.
 
Upitishaji wa sheria hizi mbovu mbovu ndio maana Nchi za wenzetu huwa kinanuka tu.

Waliokuwa wanaitikia ndioooo!! jana walikuwa wanaitikia tu kwani waliambiwa ndio kiitikio wanachopaswa kuitika, atakama inahitajika kupingwa, kwakuwa wamedanganywa kuwa sheria izi ni kwaajiri ya wapinzani, wafichua ufisadi, wanaharakati na wana JF, bila kujua kuwa sheria ikisha pita inalamba kotekote bila kujali wewe ni nani na unatoka kundi gani. NGOJA TUONE NIN KITATOKEA
 
Hizo zote ni harakati za kuzuia ukombozi wa kweli wa Mtanzania. Wame shindwa kabla hawajaanza. Meli imekwisha zama.
 
mi nimependa sana tulikofika kwa sababu mapinduzi ya Tanzania yapo karibu. Ili bomu lilipuke lazima ulichokonoe, ukitaka joka likung'ate kanyaga mkia sasa hapa ndo patamu manaake watz wengi wamepoa hii sheria itawachangamsha na soon watamjua mbaya wao. Kama lengo la watunga sheria hii ni kubaki madarakani basi tutawaondoa kama walivyoondolewa kina Gaddaf, bin ali, na wengineo. TIME WILL TELL
 
Hivi kwa sheria hii wenye internet cafee wataathirika vipi
 
Wao ni watoa huduma ya mtandao kwahyo chochote cha uhalifu kitakachobainika kupitia kompyuta zao bhasi watahitajika watoe hizo taarifa kwa polisi wakati watakapohitaji kipindi cha upelelezi na kama watafanya lolote kuficha kitendo hicho na wakabainika basi watatakiwa kulipa faini isiyozidi milioni kumi au kifungo cha miaka 3 au vyote.
 
jamani hivi hizi ID zetu itakuwaje :disapointed:

  • :disapointed:
 
Sheria haiendani na dhana yake. Cybercrime ni dhana kuu na pana zaidi.

Hapa nia ni kuwaziba mdomo wapiga filimbi waliopo JF na kwingineko.

Wale wanaotakatisha pesa na kukwiba pesa kwa njia ya mtandao hawataguswa.
 
Utekelezaji wa sheria hio ni mgumu ukizingatia nchi kubwa zilizo kuwa kiscience na technology zimeshindwa sembuse bongo! Tuache dhana kuwa CCM ndo inatunga akati bungeni kuna wapinzani pia lakini hawakuonesha kupingaa
 
1. Kifungu 7 (2b): Mpokeaji wa ujumbe (receiver) anaweza kushtakiwa kwa kosa la kupokea ujumbe ambao sheria imeufanya kuwa wa jinai. (Mfano: Mtu akikuforwadia ujumbe, ukiupokea na wewe umefanya kosa la jinai).

2. Kifungu 21(1): Mtumia mtandao wa Intaneti yeyote hayuko salama kwani mtoa huduma wake analazimika kutoa habari zake kwa serikali pale zitakapohitajika (kwa lazima).

3. Kifungu 8: Itakuwa ni kosa la jinai kama mtu ataweka wazi nyaraka za siri za serikali hata kama ni nyaraka ya kusaidia nchi kwa ujumla (Mfano: Matumizi mabaya ya mali ya umma)

4. Kifungu 14: Picha yoyote yenye mwelekeo unaoweza kuonekana kama ‘mchafu kingono’ inaweza kupelekea mtu kufungwa hadi miaka 10 au kulipa milioni 30; Sasa kama mtu kaweka picha yake Instagram ambayo sio ya ponografia lakini ‘ikatafsiriwa’ hivyo. Sheria haijatafsiri ponografia!

5. Kifungu 23: Je, ulijua kuwa ‘kusababisha maudhi ya hisia’ kwa mtu mwingine ni unyanyasaji na unaweza kufungwa kifungo kisichopungua mwaka mmoja?

6. Rejea adhabu ya ibara mbalimbali: Sheria hii kila kosa linaweza fanya mtu afungwe kifungo hadi cha maisha na kulipa pesa hadi zisizohesabika kwani hakijawekwa kikomo cha juu cha adhabu bali kikomo cha chini tu kwa kiingereza “not less than”

7. Sheria haijaeleza vizuri suala la kutumia jina lisilo lako kwenye mtandao na hivyo mtu anaweza kushitakiwa kama kuna mtu mwingine mwenye jina kama hilo katika maisha halisi.

8. Serikali kupitia waziri husika ndio ina mamlaka ya kusema jambo lililowekwa kwenye mtandao ni la kweli, uongo au la kupotosha. Kumbuka hata ESCROW, EPA walisema ni uwongo; ni wangapi katika mtandao wangeshtakiwa kiuonevu kwa hili?

9. Kifungu 22: Ukiweka ujumbe katika mtandao na ukaufuta au kuuboresha, kama ukishtakiwa kwa kuweka ujumbe huo unaweza kuhukumiwa pia kwa adhabu ya kuuboresha au kuufuta. Ni mara ngapi unafuta status zako za WhatsApp? Unaweza shtakiwa kwa kuchelewesha ushahidi kisa tu ulifuta na hamna mtu anayeweza kujua ulifuta kwa kusudi au la.

10. Mkuu wa kituo cha Polisi chochote kile nchini anaweza kuagiza wewe umpatie simu/laptop yako au taarifa zako zote (kwenye email, chats n.k) au hata vifaa vyako au ofisi yako kwa ajili ya upelelezi bila oda ya Mahakama.

11. Kifungu 31 (3a): “As soon as practicable” the law states.

Askari Polisi wakichukua vitu vyako wanaweza kukupatia listi ya vitu walivyovipokea muda watakaoona kwao inawezekana kufanya hivyo. Jiulize, inaweza chukua muda gani?

12. Kifungu 31-35 & 39-45: Kama wewe ni Blogger au Mtoa Huduma ya mtandao, pale unapobaini kosa ukalitoa na uko katika mikakati ya kuitaarifu mamlaka husika (Kama sheria inavyosema) askari naye anaweza kwa wakati huohuo akaja kukagua na kuchukua vitu vya kazi zako (kama sheria inavyosema), hivyo sheria inakinzana yenyewe kwa yenyewe. Blogger yuko sawa kisheria na askari yuko sawa kisheria.

Lissu & mnyika walijitahidi sana kututetea wananchi bt sauti za Ndio zilikuwa zinazidi,bt for sure wengi tutafungwa.

MWISHO WA SIKU WATAFANIKIWA KUZUIA MASWALA YA KUCHAFUANA BT MASWALA YA VIDEO ZA NGONO NA PICHA ZA MAGHARIBI WASAHAU LABDA MTU AMSAMBAZIE MTU PASIPO RIDHAA WAMESHINDWA KINA NANIII SEMBUSE HAWA.
 
Hapo wametengeneza dili la kuadimika kwa CD za ngono na zitakuwa zinauzwa kwa being kubwa
 
Kifungu cha kwanza...unamrushia picha ya porno waziri ili mfungwe nae!
 
Unataka kutuambia kwamba upinzani bungeni una uwezo wa kukataa muswada wowote ule usipite?

Ccm waliutaka muswada wa katiba mpya. Umepingwa na raia.

Tundu Lissu na Mnyika, wabunge wa upinzani, wamelikalisha bunge mpaka saa 6 usiku juzi, lakini wabunge wa CCM wameupitisha muswada huo.

Miswada yote mibovu itafutwa upinzani utakapochukua dola. Tambueni hilo.
 
Mtoa post anaonesha ana wasiwasi mkubwa, hata hivyo wasiwasi wake unadhihirisha wazi pasipo shaka Kuwa Yeye binafsi ni mmoja wa watu wanaotumia Vibaya mitandao ya kijamii, na hususan kuidhalilisha Serikali kwa kuikashfu na kuipaka matope kupitia kisingizio cha Upinzani wa kisiasa na uhuru wa vyombo vya habari. Ikumbukwe kuwa ibara zote alizozikosoa ziko sawa kabisa, Zinamlinda mwananchi yeyote mwenye mapenzi mema na Taifa hili. Lakini kuupinga mswada ni kuitakia nchi hii kuharibikiwa, Mswada ukipitishwa akumbuke utatungiwa sheria na kanuni, hivyo wasiwasi wa mtoa post utajibiwa na sheria na kanuni. muswada Oyeeeeere.
 
Waungwana wacha na mimi nitapike yangu kuhusu mswada huu wa sheria ya Cyber. Kwa mtazamo wangu huu mswada umechelewa ulitakiwa uje kitambo sana.. tumechoka kutukanwa kubezwa kukejeliwa... mtu anakutukani wazazi wako kisa tu mmepishana hoja za kisiasa... kuambiwa kakojoe ukalale... toa uharo wako hapa!! na mengine kama hayo na mtoto saizi ya mwanao kisa tu mmepishana kisiasa sio haki kabisa.... tumekua tukiumizana humu kwa matusi na kejeli hasa za kidini.. baadhi yetu wamefika hata kuichukia serekari kwa kuhisi labda inaupendelao na dini flani,,, yote hii tu kwa sababu uhuru wa kupitliza. Wazee wa kunasa data sijui itakuwaje sasa,,,, tafuteni agenda nyingine mtuachie staha na utu wetu.
 
Back
Top Bottom