Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015: Kwa mkakati huu wa Serikali, Watumiaji wa Mitandao tutapona?

Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015: Kwa mkakati huu wa Serikali, Watumiaji wa Mitandao tutapona?

Hiyo sheria kandamiz

Kama ni kandamizi, Je? umejiuliza matendo yote yaliyoainishwa katika sheria hiyo ni halali kwa manufaa ya kuanzia familia, jumuiya hadi taifa kwa ujumla? Unapotoa hoja uliza na fuatilia vitu vyote vilivyo ndani ya sheria hiyo. Tukubali kujali pia watoto wetu kwa kuzingatia maadili ya Kitanzania

Wamekuwa wakifafanua kwenye vyombo vya habari hasa TV....
Kikubwa kitakachoathiri wengi kwa ujumla ni ile kunyimwa taarifa,hasa za kiuchunguzi mfano zile za EPA na ESCROW.
Ila kwa wale wapenda pornografia,ufafanuzi wake ulivyotolewa ni kuwa itakuwa na madhara endapo itawekwa online. Ila ya kutumiana wenyewe kwa wenyewe,haina madhara yoyote.
Adios.

mfa maji haishi kutapatapa, the last days of ccm na mafisadi.

CDM na UKAWA kwa ujumla waliupitisha mswada na wakaufanyia marekebisho pale ilipohitajika....acheni ushabiki usiojenga....hii si kwa CCM hii ni kwa taifa zima ndugu..

CDM na UKAWA walilalamika lakini wapi massm yananapitisha ujinga wao. Ndo maana Lisu aliamua kuondoka na japo aliwambia hawata mpata mtu kwa sheria zao hizo mbovu.

Lakini mimi naona shida wabunge wengi hutetea miswaada yako mawaziri wao wa ccm Bila kujua hiki kinawafaa wananchi wangu au hakifai nakubali kua kuna wabunge wa ccm ambao wanaikoasoa wizara kutokana na miswaada mibovu lakini miongoni mwao ccm I naanza kuwanyooshea vidole

Upingaji wa hii sheria inahitaji ushiriki wa wadau wote ikiwemo wananchi wenyewe.
La sivyo kutakuwa kutengeneza ulaji wa rushwa kwa mapolisi na unyanyasaji wa haki za msingi za habari.
Ni hayo tu

Mimi naona sheria hii inafaa kwa kuwa nyie wenyewe humu hamzingatii mawazo ya watu wengine mkiona post ambazo sio mlengo wenu hamziruhusu.Naona bora serikali waingilie ili hata watu wengine wawe huru kutoa mawazo mubadala.

Ila hii sheria kwa kiasi fulani inahitajika kwasababu ujinga unaoendelea kwenye mitandao ni mwingi na hakuna njia nyingine ya kuudhibiti isipokuwa hii sheria. Mimi naisapoti kabisa hii sheria kama haufanyi makosa yaliyoanishwa katika hii sheria kwanini mnaiogopa?

Suala la kuikubali au kuikataa sasa lipo mikononi mwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Jakaya Kikwete. maoni yangu ni kwamba ni kama tunaelekea upande mmoja zaidi tukizungumzia muswada huu na kuuacha kabisa upande mwingine. Tunakuwa tunaonge kama vile ni mabaya tu yanayoweza kuletwa na sheria hii endapo itasainiwa, lakini tunasahau kwamba Tanzania sio nchi iliyoendelea kiteknelojia kama ilivyo kwa nchi nyingi za Ulaya na Magharibi ambapo wenzetu hata taasisizao za kiserikalizina uwezo wa kupambana kiteknolojia katika kudhibiti uhalifu na matumizi mabaya ya teknolojia.

Huku kwetu, vyombo vyetu vya dola kumudu mapambano ya aina hii kwani uwezo wa vyombo vyetu vya kiusalama bado vipo nyuma sana kiteknolojia. Kwa sababu hii, wale watu wenye utaalamu wa juu kwenye sekta hii wanaweza kutumia udhaifu huo kama fursa kwao kufanya uhalifu wao kama ambavyo imeshatokea kwenyematukio kadhaa sasa hapa nchini.

Nadhani maoni ya kupinga muswada huu wangekuwa sahihi sana endapo tungekuwa na nchi na vyombo vyenye maendeleo makubwa kiteknelojia kama nchi za magharibi. Nahisi kama tunataka uhuru kama waliokuwa nao Marekani katika mitandaowakati vyombovyetu havina spidi hiyo katika kuudhibitiuhalifu unnaoweza kujitokeza. Hii si sawa.

Yaaani ambaye anaogopa sheria hii ndo wakwanza kuivunja coz wagmtu tumekosa ustaarabu siku iziii yani kudhalilishwa ni kitu cha kawaida tuu me sjui wewe ambaye hauitaki unawachukuliaje dada zetu wanavyodhalilishwa mitandaoni

Musihofu wakuu baada ya October serikali chini ya chama kingine hayo mambo yatafutiliwa mbali,hizo ni juhudi za mwishomwisho za watawala kutaka kujinasua na jinamizi la kuangushwa!

utapona kama ukitumia mtandao vizuri na pia kuwaeleza marafiki zako msimamo wa kimaisha, waeleze hupendi kutumiwa mambo ya ajabu na hakikisha wanaliheshimu hilo;

Watanzania tunalalamika sana muda mwengine mpaka tunasahau mema ambayo viongozi wetu wanatufanyia. Watanzania ni kama tayari tumesahau kwamba ilikuwa tuwe tunalipishwa kodi ya kila mwezi kwa laini za simu tunazotumia, ila kwa kuwa Ndugu January Makamba aliamua kulisimamia hili na kufanikiwa kumshawishi Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kukubali kusaini hati ya dharura kufanya marekebisho ya muswada wa fedha na kuondoa kodi ya tozo kwa laini za simu. Bonyeza link hii ya gazeti la "The Citizen" ujikumbushe na hiyo habari tafadhali.

http://www.matukiotz.co.tz/2013/12/angalia-post-ya-january-makamba-kuhusu.html

au hii kwa wale wanaojua lugha ya Kiingereza:
http://www.thecitizen.co.tz/News/national/SIM-card-monthly-charge-to-go--at-last/-/1840392/2119258/-/ay6k6a/-/index.html

Upuuzi , kwani unataka kusema kwemba ametutetea?? Kwani aliesema tulipe kodi hiyo ni nani. Na kwanini tulipe. Kodi zingine hazifai? Na mambo hayo ya kipuuzi ndiyo yanayo wagharimu sasa. Tazama wengi hawatarudi bungeni sababu ya ujinga huo. Kama kuna mambo kumi wamefanya basi tambua saba ni mabaya, machafu,maovu na matatu ndiyo walau yana maelezo.

katika ujinga serikali ya ccm imewahi kuthubutu ni huu! puuuuuuuu hii ccm na itoke sasa, enough is enough!

[COLOR=rgba(0, 0, 0, 0.54902)]In Africa, where a free press is often more of an ideal than a reality, humorists have sometimes been able to speak truth to power a little more fearlessly than conventional reporters. And the continent’s political cartoonists have been contextualizing the reality of public life to great effect, and in their way, documenting Africa’s history.

Which is why the decision by Nigerian researcher Tejumola Olaniyan to create an online archive of some of the continent’s best cartoons is so invaluable.

For more, please read here: You can read the history of Africa through this online trove of political cartoons - Quartz
[/COLOR]
[COLOR=rgba(0, 0, 0, 0.701961)]For more, please read here.
[/COLOR]

Hii sheria ni kali sana sijui tunaoshinda kwenye mitandao tutabaki! Jamani namshauri miss Chagga atangulie gerezani.

Nchi hii! wengine tunauza nyanya wateja hakuna tunabaki kukaa JF tu, kutoa hisia zetu na mitazamo yetu!

Kwa Mfano!!Mpaka 25 October 2015 wanaharakati wote watakuwa wamefungwa! Alafu wanamuapisha magufuri kama alivyoapishwa Kibaki! Hahahahaha asubuhi asubuhi wakati ukawa wanashangilia ushindi! Magufuri ana apishwa. Wanaharakati wote wapo segerea 😂😂😂🎬🎬🎬

ha ha haha mkuu ngoja nitumie hii nafasi kutoa hisia zote na gerezani siendi... na october tunawapiga chini waende huko wao

ha ha haha mkuu ngoja nitumie hii nafasi kutoa hisia zote na gerezani siendi... na october tunawapiga chini waende huko wao

Mimi nakuona kwa mbali umevaa nguo za Orange unakata kuni! Kwa kosa la kushare ujumbe wa tuhuma za kifisadi eti JK ni taijiri zaidi ya Rostam azizi!

Mimi itabidi nifanye maamuzi magumu ya kutokujiunga vifurushi vya Internet au nikijiunga niwe nasoma tu.
La sivyo nondo inanihusu.

Back
Top Bottom