Dr. Msafiri
JF-Expert Member
- Feb 14, 2011
- 471
- 154
Kufifilisha kosa
50.-(1) Bila kuathiri sheria nyingine inayotumika Tanzania Bara, Mkurugenzi wa Mashtaka, muda wowote kabla ya mwenendo wa mahakama kuanza na kwa kuzingatia tamko la kukiri kosa kwa hiari la mshitakiwa anaweza kufifilisha kosa na kuamuru mtu huyo alipe kiasi cha pesa atakachokitaja ambacho hakitazidi kiasi cha faini kwa kosa hilo.
(2) Amri ya kufifilisha kosa chini ya kifungu kidogo cha (1) itakuwa -
(a) ya maandishi, ikiainisha kosa lililotendeka, kiasi cha fedha zitakazolipwa na tarehe ya kufanya malipo ikiambatanisha tamko la kukubali kosa lililorejewa chini ya kifungu kidogo cha (1);
(b) ni uamuzi wa mwisho na hautakatiwa rufaa; na
(c) na uwezo wa kutekelezwa katika namna sawa na amri ya Mahakama Kuu.
51. Waziri anaweza kutunga Kanuni kuhusiana na jambo lolote ambalo linatakiwa kuainishwa na Sheria hii au ambalo ni la umuhimu au uharaka kwa ajili ya utekelezaji wa masharti ya Sheria hii.
Kama Serikali ya ccm ingekuwa inatunga sheria kali kwa mafisadi, asingebaki hata mmoja. sheria zao kandamizi ni kwa walala hoi
Ikitokea hivyo nasi tuwapeleke kwa pilato.Watawala wenyewe wanapotosha mangapi kwa maslahi yao ya kisiasa?
Huu ni ushahidi kuwa CCM wana hali mbaya na si vinginevyo.
Ukiwa sio muongo, mdaku sheria ni murua Kabisa...
Itasaidia tusome vitu vya ukweli sasa sio mazagazaga. Sometimes we waste a lot of time kusoma maujinga ambayo mtu Hana hakika naye.
kenya ma-blogger mbalimbali waliingia kwenye mikono ya Pilato kwa kucheza na sheria kama hii.
Isomeni sheria nzima hapa - http://mst.go.tz/index.php/componen...wnloads?download=24:the-cybercrimes-bill-2015
Haya ni maneno ya mtoto wa kiume am a?
hata kama kuna uongo lakiniNi kweli mkuu, mitandao imekuwa na uongo na upotoshaji sana,
Nashindwa kumuelewa mleta mada anaposema sheria kama hii haiendan na demokrasia. Sijui ni demokrasia ipi inayoruhusu uongo na upotoshaji.
hata kama kuna uongo lakini
unadhani inastahili unyama huu wa January ? kama wanapotosha kwanini nyie msiweke ukweli ili kunyoosha mambo ? hivi kwa mfano chenge akiitwa fisadi ni kweli kwamba kuna upotoshaji ?