mswada huu hauna maslahi kwa taifa letu lakini CCM wataupitisha
Bujibuji,
Let me say this: Muswada huu kama ulivyo hauna maslahi yoyote kwa Taifa isipokuwa UNA MASLAHI MAPANA NA MAKUBWA SANA KWA CHAMA TWAWALA CCM. Nitaeleza:
Watanzania lazima tuamuke na tuwe macho. Haihitaji kwenda chuo au shule ili kujua kwanini serikali ya CCM imepeleka muswada huu kwa hati ya dharura. Kwanza kabisa lazima tujue kuwa tarehe 30 Aprili ilikuwa iwe siku kupiga KURA YA MAONI kwa ajili Katiba Pendekezwa lakini pia mwezi Oktoba ni siku ya Uchaguzi Mkuu.Tunajua kura ya maoni imeahirishwa mpaka itakapotangazwa vinginevyo na Tume isiyohuru!!
Sasa basi kwa vile CCM wanajua kuwa ili WASHINDE LAZIMA waibe kura/kuchakachua au kughushi matokeo lazima waaandae MAZINGIRA ya kudhibiti na kuhalalalisha wizi,uchakachuaji na kughushi matokeo hayo kwa kutishia media zote zisiweze kutangaza matokeo tofauti na yale watakayokuwa wametengeneza wao. Kumbukeni kuna kifungu kinachozungumzia TAKWIMU kwenye muswada huuhuu!Nitatoa mfano: Tuseme kuwa jimbo la Uchaguzi la Ubongo matokeo halisi ni CHADEMA: kura 38,000, CCM: kura 1,200 na msimamizi wa Uchaguzi atatangaza hivo na kuweka kwenye mbao za matangazo au asiweke. Lakini kwa kuchakachua wakasema CCM ni 120,000 NA CHADEMA: 38,000 na hivo aliyeshinda ni CCM na tume isiyo huru itatakiwa itangaze hivo. Sasa kwa media au chanzo kingine cha habari kitakachosema ukweli wa matokeo haya ndiyo kitaambiwa kimevunja sheria ya Mitandao!!!Mpo hapo?? kwa hiyo hii itakuwa hivo kwenye kura ya maoni na achaguzi Mkuu ili kuhakikisha Serikali ya CCM inabakia madarakani.
Lakini pia sheria hii inaenda moja kwa moja kugusa maswala mazima ya Ufisadi kwa maana ya kulinda siri za Kifisadi. Watu watakumbuka sekeseke la Escrow Account hivi karibuni. KUlikuwa na mgongano wa kiasi cha fedha iliyoibwa na kina Lugemarila/IPTL na washirika wake kuwa ni zaidi ya Bilioni 300 au chini ya hapo na kama hiyo fedha ni ya Serikali au ni ya IPTL. Tuliona fedha iliyoingizwa kwenye akaunti za Watu binafsi kuanzia Milioni 40 mpaka Bilioni 1.6. Takwimu zote hizi tulikuwa tukizipata kupitia media na isingekuwa media tusingejua chochote tulichokijua. Hapa ndipo penye shida. Hawa MAFISADI kina Chenge,Tibaijuka, Ngeleja n.k wanataka kuhakikisha kuwa mambo kama haya hayawekwi hadharani kwasababu ni siri na zinawaumbua. Kwa hiyo lazima CCM na maswihiba wake/Mafisadi waweke sheria au mazingira ya kuhakikisha kuwa UFISADI WAO HAUWEKWI HADHARANI kupitia media yoyote iwe TV, Redio, Magazeti na mitandao ya Kijamii!! Huu ni ukweli ambao CCM na serikali yao hawawezi kuukana hata mara moja.
Kwa hiyo basi Watanzania lazima tuipinge sheria hii kandamizi kwa nguvu zetu zote ikibidi hata kuandamana achilia mbali kuweka saini zetu kwenye mitandao au SMS. Hatuwezi kukubali sheria inayominya uhuru wa Vyombo vya habari kwa maslahi ya wachache yaani CCM na mafisadi wenzao.
Nitaendelea.............