Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015: Kwa mkakati huu wa Serikali, Watumiaji wa Mitandao tutapona?

Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015: Kwa mkakati huu wa Serikali, Watumiaji wa Mitandao tutapona?

Ninataka UHURU wangu bila masharti...................Nani amekwambia uje huku?
 
Pale bungeni wanatukanana live mitusi mikubwa, watoto wa miaka mitatu wanasikia na kutizama ktk tv, je wametunga sheria ya kuwabana? Au wanaangalia jinsi ya kuwakandamiza wananchi, kuna mtoto mdogo anamiliki cm?

Tena umenena kweli maana wakati wa lile Bunge letu lililopitisha ile Katiba ya Chenge............Ilikuwa inabidi TBC na Star uzifunge wakati wa BUNGE amasivyo utakuta watoto wameangalia SINEMA ya KIKUBWA..........................
 
Naunga mkono hoja, kura yangu ni ndio rais aweke sahihi haraka sana huu muswada. Sheria kama hii imefanikisha sana serikali ya libya ya khaddafi. Ilimpatia sifa kubwa ya kuwa mmoja wa madikteta wanaopatikana duniani.

Ngalizo tu kwa mh rais wakati unaidhinisha mswada huu kuwa sheria uwe vilevile umesha angalia hospitali za kwenda kuangalia afya yako china au urusi. Baada ya sheria hii kupita sitashangaa kuingia kwako usa na ulaya mangaribi kuwa matatani. Ni hilo tu, mfano wa mbayuwai unakuhusu sana hapa.
 
Kwa hiyo hapa JF umefuata nini Michael Chairman ?

Kura km hiyo kaianzishe kwenye redio au gazeti
Tena hiyo mada yake angeipeleka TBCCM au Uhuru media, angepata full support ya asililmia 100.

Kuileta huku JF, alivyofanya huyo Michael Chairman ni sawa sawa na mtu aliyevaa kanzu na baraghashia, halafu akatinga nayo hayo mavazi kanisani! wakati waumini wa kanisa husika wakiendelea na ibada!
 
Last edited by a moderator:
Huo ndio uelewa wenu watz,,inasikitisha sheria hatari kama hii ambayo hata mkoloni mzungu hakuthubutu kuitunga,,eti kuna watz tena wasomi wamejivua ufahamu wanaishabikia kama majuha inatisha sana.hivi nchi hii tunaenda wapi!?
 
mswada huu hauna maslahi kwa taifa letu lakini CCM wataupitisha

Bujibuji,

Let me say this: Muswada huu kama ulivyo hauna maslahi yoyote kwa Taifa isipokuwa UNA MASLAHI MAPANA NA MAKUBWA SANA KWA CHAMA TWAWALA CCM. Nitaeleza:

Watanzania lazima tuamuke na tuwe macho. Haihitaji kwenda chuo au shule ili kujua kwanini serikali ya CCM imepeleka muswada huu kwa hati ya dharura. Kwanza kabisa lazima tujue kuwa tarehe 30 Aprili ilikuwa iwe siku kupiga KURA YA MAONI kwa ajili Katiba Pendekezwa lakini pia mwezi Oktoba ni siku ya Uchaguzi Mkuu.Tunajua kura ya maoni imeahirishwa mpaka itakapotangazwa vinginevyo na Tume isiyohuru!!

Sasa basi kwa vile CCM wanajua kuwa ili WASHINDE LAZIMA waibe kura/kuchakachua au kughushi matokeo lazima waaandae MAZINGIRA ya kudhibiti na kuhalalalisha wizi,uchakachuaji na kughushi matokeo hayo kwa kutishia media zote zisiweze kutangaza matokeo tofauti na yale watakayokuwa wametengeneza wao. Kumbukeni kuna kifungu kinachozungumzia TAKWIMU kwenye muswada huuhuu!Nitatoa mfano: Tuseme kuwa jimbo la Uchaguzi la Ubongo matokeo halisi ni CHADEMA: kura 38,000, CCM: kura 1,200 na msimamizi wa Uchaguzi atatangaza hivo na kuweka kwenye mbao za matangazo au asiweke. Lakini kwa kuchakachua wakasema CCM ni 120,000 NA CHADEMA: 38,000 na hivo aliyeshinda ni CCM na tume isiyo huru itatakiwa itangaze hivo. Sasa kwa media au chanzo kingine cha habari kitakachosema ukweli wa matokeo haya ndiyo kitaambiwa kimevunja sheria ya Mitandao!!!Mpo hapo?? kwa hiyo hii itakuwa hivo kwenye kura ya maoni na achaguzi Mkuu ili kuhakikisha Serikali ya CCM inabakia madarakani.

Lakini pia sheria hii inaenda moja kwa moja kugusa maswala mazima ya Ufisadi kwa maana ya kulinda siri za Kifisadi. Watu watakumbuka sekeseke la Escrow Account hivi karibuni. KUlikuwa na mgongano wa kiasi cha fedha iliyoibwa na kina Lugemarila/IPTL na washirika wake kuwa ni zaidi ya Bilioni 300 au chini ya hapo na kama hiyo fedha ni ya Serikali au ni ya IPTL. Tuliona fedha iliyoingizwa kwenye akaunti za Watu binafsi kuanzia Milioni 40 mpaka Bilioni 1.6. Takwimu zote hizi tulikuwa tukizipata kupitia media na isingekuwa media tusingejua chochote tulichokijua. Hapa ndipo penye shida. Hawa MAFISADI kina Chenge,Tibaijuka, Ngeleja n.k wanataka kuhakikisha kuwa mambo kama haya hayawekwi hadharani kwasababu ni siri na zinawaumbua. Kwa hiyo lazima CCM na maswihiba wake/Mafisadi waweke sheria au mazingira ya kuhakikisha kuwa UFISADI WAO HAUWEKWI HADHARANI kupitia media yoyote iwe TV, Redio, Magazeti na mitandao ya Kijamii!! Huu ni ukweli ambao CCM na serikali yao hawawezi kuukana hata mara moja.

Kwa hiyo basi Watanzania lazima tuipinge sheria hii kandamizi kwa nguvu zetu zote ikibidi hata kuandamana achilia mbali kuweka saini zetu kwenye mitandao au SMS. Hatuwezi kukubali sheria inayominya uhuru wa Vyombo vya habari kwa maslahi ya wachache yaani CCM na mafisadi wenzao.

Nitaendelea.............
 
sio bongo pekee hata n'gambo hakuna uhuru wa habari ila kuna uhuru wa mitambo na mwenye mari kama huwezi amini angalia hata IPP ahaiwezi ikampinga MENGI...me nafikiri hata ikiwepo haitokua na maana yoyote kwani watunga sheria ni wao na haohao ndio wavunja sheria...kwetu sisi wanatechnohama itatuongezea uwezo wa kufikiri na kuyafanya hayo wasiyoyataka kwa UFUNDI ZAIDI.... ....NOOOOO SURENDER.....
 
Hivi karibuni serikali ilileta bungeni mswaada wa dharura wa makosa ya mitandaoni.Katika mswaada huo ambao Rais Kikwete anatarajia kuusain hivi karibuni,kuna sheria kali sana ambazo zinawabana watumiaji wa mitandao.Nikiangalia watumiaji wengi wa mitandao hasa hapa jamii forum,wengi wamekuwa wakijitungia tu habari na kuileta hapa jamvini bila ushahidi wowote.Yaan hapa jamvini ni kama sehemu ya kutunga hadithi ili mradi mtu ajifurahishe.Kwa maana nyingine tumekuwa tunalishwa ujinga kila siku.Mfano leo mtu ameibuka na habar kuwa mwamnyange ametishia kujiudhuru na barua ipo kwa rais.Ameombwa ushaidi lakini mpaka sasa hakuna.Kutokana na vitu vingi kama hivyo nina amini ndo maana serikali inataka kwadhibiti watumiaji wengi wenye kuleta hadithi za uongo kwa faida yao.
 
Mimi mwenyewe najiuliza kwa nini sheria hii iletwe kipindi hiki? Ina maana hawa jamaa wana lengo la kuzuia tusiseme mambo yao kwenye mitandao? Halafu tulivyo wavivu kusoma twaweza kushabikia mswaada huu upite lakini kwa hii inji mswada huu ukipita sijui itakuaje.
 
Kujitia ushujaa wa kwenye keyboard ni ujinga tu.Wanaume wa kazi wakianza kazi zao itabidi mapanya wote wafuate sheria. Utashindana na sheria wewe nani?Ohh waongeze magereza my foot! Utafyata tu huo mkia.
 
Sheria iwekwe wazi to every one coz the victim are citizens not the leaders at all japo wakati wa utungaji wa hizi sheria ushirikishaji wa wadau ni zero this show that our government is real impotent
 
Kazi ipo.

Ilza wasisahau kuwa sheria ni "Msemeno" Hivyo aita kula kwetu tu bali ata kwao pia. Wapi Kova na mtekaji wa Dr. Ulimboka? Mwigulu na kauli zake za Ugaidi?

Zaidi naona itakula sana kwa Nape Nnauye maana yule bila kuongea uongo na kusingizia watu hawezi fanya uenezi.

Time will tell

Tunasubiri muda tu MKUU JK agonge saini kubwaaaa iwe lesson kwa wale wanaotumia vibaya na hii itasaidia kuwepo na heshima na kuondoa manyanyaso maana hata humu ndani JF baadhi ya watu wananyanyasika.
 
Mimi mwenyewe najiuliza kwa nini sheria hii iletwe kipindi hiki? Ina maana hawa jamaa wana lengo la kuzuia tusiseme mambo yao kwenye mitandao? Halafu tulivyo wavivu kusoma twaweza kushabikia mswaada huu upite lakini kwa hii inji mswada huu ukipita sijui itakuaje.

Kaka umeshaambiwa kuwa Rais atasaini hiyo miswada yote miwili sasa unauliza nini kuhusu kupita kwake? itapita na itakuwa sheria maana haiko kwa lengho la kumkomoa mtu fulani, hii itasaidia kuheshimiana.
 
Tena hiyo mada yake angeipeleka TBCCM au Uhuru media, angepata full support ya asililmia 100.

Kuileta huku JF, alivyofanya huyo Michael Chairman ni sawa sawa na mtu aliyevaa kanzu na baraghashia, halafu akatinga nayo hayo mavazi kanisani! wakati waumini wa kanisa husika wakiendelea na ibada!

Itasainiwa na itakuwa sheria, wewe ombea porojo zako siku ije kukubana ndo ujue.
 
dalili za dola inayohofia kuanguka ndio hizi.Mtawabana sana wananchi ila hamjui ndio mnazidi kupalilia chuki dhidi yenu!
 
Serikali tuliyoiweka wenyewe madarakani sasa inafanya uasi dhidi yetu sisi wenye nchi. Inakiuka katiba. Sheria hii inakinzana na Ibara ya 18 ya Katiba inayoainisha Uhuru wa maoni.

Kwa kusema fulani amepotosha, ilhali ni maoni yake, hapo haki yake ya kujieleza inaingiliwa. Sheria hii ni mfu. Tusipoipinga kwa nguvu zetu zote itakula kwetu!

Na zitakuja nyingine mbaya zaidi.

Ushabiki wa vyama uwekwe kando kwa hili kwa kuwa ni suala la haki na halijaainisha iwapo litamlenga mwanachama wa upinzani au chama tawala, bali mtu yeyote... Mtanzania au asiye Mtanzania.

#TupingeUdhalimu
 
Nadhani wadau, JamiiForums kati kuhakikisha ukweli wa habari tuko mbele sana na ndiyo maana tunaona wana-Jamiiforums wako mstari wa mbele kuhoji uhalali wa habari /thread kwa ku-demand source, picha, video, nyaraka, kuchallenge data, trends n.k hii yote ni katika kuhakikisha thread imebeba habari za kweli na za kuaminika.

Thanks!
Handmade Cards
 
Waziri Sophia Simba amekanusha Rais kusaini huo mswada kuwa sheria, bado haujasainiwa
 
Back
Top Bottom