Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tutapike tu hawana hiyo technologia kutengeza kibiriti hawawezi wataweza kutu trap ktk media technology wanatutisha tu si walituonyesha panya wakasema watatumika ktk kuwapata majambaz mbona kimya kila siku twaibiwa
Unaonekan unatumika sasa hii sheria lazima ikuweke ndani ww....
Wezi tu hao miaka 50 bado paracetamol hospital hakuna
Na sisi wabeba box hii sheria yenu mtatupataje?
Cc: Nyani Ngabu
![]()
sheria hii inatarajiwa kupitishwa jumanne 31 machi na aprili 01, 2015 kwa hati ya dharura.
Wakuu,
baada ya kuisoma sheria tarajiwa ya makosa ya jinai kwa watumiaji wa mitandao (cybercrime) ambayo inapitishwa bungeni kwa hati ya dharura, napata shaka juu ya uhuru wa watanzania watumiao mtandao.
Serikali yetu imeamua kutuumiza watanzania kwa mara nyingine. Inauma, inasikitisha na hatuna wa kututetea.
Wameona kupunguza vifurushi pekee hakutoshi, wameamua kutupangia nini tuongee, nani aongee na aongee vipi. Watoa huduma watalazimishwa kutoa taarifa zetu na wakikataa wataadhibiwa "kwa mujibu wa sheria".
Kwa ufupi, serikali inataka kuamua upi ukweli na upi uwongo. Huu ni ubakaji mkubwa wa demokrasia. Wengi tutafungwa kwa uonevu wa kipengele hiki.
Napata shaka zaidi kwa watumiaji kutokujua hatari inayokuja mbele yao na hivyo kuchukua tahadhari.
Aidha, nina mashaka sana kama wabunge wetu wanaelewa athari yake kwao pia maana kama walidhani wanalengwa jf tu, basi hii ina upana zaidi ya hapo.
Kwa kiingereza:
Na pia, kipengele cha 21 kinaihusu jamiiforums au wengine wanaotoa huduma kama hizi. Serikali yetu tukufu inataka iwe ni lazima taarifa za watu zitolewe na watoa huduma ili iweze kufanya uchunguzi.
Wanaharakati, wapinzani na wengine ambao serikali yenu tukufu huenda inawahofia au kuwatilia shaka, itawalazimisha watoa huduma kutoa siri zenu. (email zenu hupita kwa isp na sio encrypted):
Soma pia kuhusiana na watoa huduma:
Aidha, serikali hii tukufu imeamua kutumia kifungu cha 22 kuonyesha dhamira yake si ya kutania endapo itataka kupata taarifa za mtu na mtoa huduma akataka kuua ushahidi kama inayosomeka:
Angalieni kipengele hiki pia:
Tupo salama?
Ni kutaka kudhibiti taarifa wakati wa uchaguzi? Ni kuwalinda kina nani?
Isomeni sheria nzima hapa - http://mst.go.tz/index.php/componen...wnloads?download=24:the-cybercrimes-bill-2015
nimeambatanisha kipengele ninachoona ni tatizo zaidi.
Cc emt, mzee mwanakijiji, nguruvi3, mchambuzi na wengine mnaoweza kututoa wasiwasi
Informer mbona unataka kushusha kiwango chako? Kama huoni mantic ya sheria hii basi kiwango chako cha kufikiri kitakuwa kipo chini sana mkuu.