Sheria ya Mirathi ya Kiislamu kwa mtoto wa nje ya ndoa ibadilishwe

Sheria ya Mirathi ya Kiislamu kwa mtoto wa nje ya ndoa ibadilishwe

Hio sheria ingekuwa inamtambua mtoto wa nje ya ndoa kungekuwa na ugomvi na mtafaruku mkubwa sana kwenye misiba kwasababu anayeweza kuthibitisha ni mtoto wake ameshatangulia mbele ya haki hvyo watu ingekuwa wanafanya usanii sana kuna watu wangekuja na watoto kwenye bajaji ili tu wapate mali hvyo naona ipo sahihi ili kuepusha malumbano.
 
Niende Moja Kwa Moja kwenye mada, enyi waislamu kwanini hamtambui uwepo wa mtoto wa nje ya ndoa wakati wa mirathi?

Eti mtoto wa nje ya ndoa hana haki ya kirithi mali za baba ake mzazi hivi sheria gani hizi ambazo zinamkandamiza mtoto?

Mtoto ni mtoto tu haijalishi ni kambo au wandoa.

Wanasema kwamba mtoto wa kambo ni mali ya mama hii inakuaje aisee?

Sheria hizi zibadilishwe ili kulinda haki ya mtoto katika taifa hili kwasababu inamharibu mtoto kisaikolojia anajiona kama amelaaniwa kuja duniani .
Kumbuka, mali za baba zimetafutwa na kusimamiwa kwa msaada wa mke mwenye watoto wa ndoa pamoja na msaada wa watoto wa ndoa. Sasa we utoke ulipotoka uje udai kivipi?
 
Usiongelee kwenye jukwaa hili. Katafute maiki usimame wakuone ndio Utajua rangi zao
Kwa akili watanisome dua kuwa naharibu dini Yao ila ukweli ni kwamba wanavofanya sio basi watoto wote majina ya baba zao yafutwe yawekwe ya Babu zao upande wa mama maana tayari dini Yao inamkana mtoto
 
DAWA NA NYIE MABINTI KABLA YA KUZAA ULIZEN WANASHERIA WATOTO WENU WATAKUJA KURITHI AMA LAH

USIJISHADADUE OOH ANANIPENDA ANA HELA AKINGOKA MTAISHIA KUHUDHURIA MSIBA NA KUWEKA SHADA TU MENGINE B MKUBWA ANAYAMALIZA

DINI ILE WANARITHI KAMA KAWAIDA
 
sio kila mtu wa kuzaa nae mtazaa wakifa mtelea wenyewe imetoka hio

m dadazangu niwamwagia maji na mafuta ya mwaposaa kamwe msizae bna waume za watu wamebaki wawili hawa nawapigia maombi saa nane usiku waolewe tu waondoke ndan
 
Mtoto Hana makosa na akifanikiwa mzee anaanza kujisogeza yaani kama mm utakula vichwa live anilaani tu
 
DAWA NA NYIE MABINTI KABLA YA KUZAA ULIZEN WANASHERIA WATOTO WENU WATAKUJA KURITHI AMA LAH

USIJISHADADUE OOH ANANIPENDA ANA HELA AKINGOKA MTAISHIA KUHUDHURIA MSIBA NA KUWEKA SHADA TU MENGINE B MKUBWA ANAYAMALIZA

DINI ILE WANARITHI KAMA KAWAIDA
Wanawake hawana makosa wenye makosa ni sisi kwanini umtongoze afu umuahidi utamuoa. Huu ni shetani mtoto anakuwa kama nunda vile
 
Mtoto ni mtoto tu haijalishi ni kambo au wandoa.
mtoto wa kambo ni tafauti na nje ya ndoa. Wa kambo ni wa mama tafauti lakini amemzaa ndani ya ndoa.

Kwa bahati nzuri au mbaya kwako hatuwezi kubadilisha sheria kwenye Qur'ani.

Hiyo itakuwa imekula kwako au kwa mpwa wako.

Lakini anaweza kuruka kipengele hichi kwa kumpa chake kabisa wakati yuko hai. Au sheria ya mirathi inaruhusu yule asiyekurithi umuandikie mpaka moja kwa tatu ya mirathi yako. Na hii ni kuwa mtu anao uwezo wa kumuandikia urithi yeyote yule lakini isizidi moja kwa tatu ya thamani ya mali yake.

Ikiwa anao hata watoto kumi wa nje basi itakuwa hiyo hiyo moja kwa tatu.
 
je ushawahi kutunza mtotommpaka la saba ukaamua kupimq dna na kukuta si wako??

je wa nje kwa mwanamke nae anarithi
Wa nje kwa mwanamke pia hawezi kurithi, alimradi umethibitisha kama siyo wa kwako.

Kwa imani ya kwetu inabidi uende msikitini, siku ya Ijumaa ambapo kwa kawaida kunakuwa na watu wengi, halafu usimame hadharani umkane yule mtoto kuwa siyo wa kwako. Hapo watu walioko ndiyo watakuwa mashahidi wako.

Siku hizi wanataka uweke kwa maandishi siyo kujisemea tu.

Kumbuka huku kwetu bado DNA haijatambulika vijijini.
 
Kwa akili watanisome dua kuwa naharibu dini Yao ila ukweli ni kwamba wanavofanya sio basi watoto wote majina ya baba zao yafutwe yawekwe ya Babu zao upande wa mama maana tayari dini Yao inamkana mtoto
kwa sheria ya dini mtoto wa nje ya ndoa hawezi kuitwa kwa jina lako kama binti fulani au bin fulani.

Ataiwa jina la babu yake mzaa mama.
 
mtoto wa kambo ni tafauti na nje ya ndoa. Wa kambo ni wa mama tafauti lakini amemzaa ndani ya ndoa.

Kwa bahati nzuri au mbaya kwako hatuwezi kubadilisha sheria kwenye Qur'ani.

Hiyo itakuwa imekula kwako au kwa mpwa wako.

Lakini anaweza kuruka kipengele hichi kwa kumpa chake kabisa wakati yuko hai. Au sheria ya mirathi inaruhusu yule asiyekurithi umuandikie mpaka moja kwa tatu ya mirathi yako. Na hii ni kuwa mtu anao uwezo wa kumuandikia urithi yeyote yule lakini isizidi moja kwa tatu ya thamani ya mali yake.

Ikiwa anao hata watoto kumi wa nje basi itakuwa hiyo hiyo moja kwa tatu.
JE?Kwa upande wa ukoo hawawezi kukataa maana Kwa kiukoo mtoto wa kwanza ndie mrithi haijarishi niwa nje au ndani wao hawajui hayo
 
kwa sheria ya dini mtoto wa nje ya ndoa hawezi kuitwa kwa jina lako kama binti fulani au bin fulani.

Ataiwa jina la babu yake mzaa mama.
Sio kweli wengine wanaitwa majina ya baba zao kbs
 
Back
Top Bottom