Na sio uislamu tu ambao umeweka sheria hiyo bali hadi ukristo nao umeweka wazi juu ya suala hilo.
Kama wewe ni mkristo basi unawakilisha zaidi ya 80% ya wenzako ambao hawana muda wa kusoma maandiko ya biblia na maelezo kuhusu ukristo wao.
Na ndio maana zikija mada za kidini wengi wa wakristo wanapenda kuelezea matamanio ya nafsi zao kuliko ukweli wa mambo ulivyo, mfano mzuri ni mgogoro wa Israel na palestina, yaani wakristo wapo radhi kusikia waisrael ambao ni wayahudi wanawazuia waumini wa kikristo kufanya ibada kanisani na wao wanaoshabikia manyanyaso wanayokumbana nayo wenzao, kwa kweli inasikitisha halafu kuthibitisha Kuwa ninyi ni wavivu wa kusoma huwa mnashindwa hata kugugo mambo machache kuhusu hiyo Israel mñayoishabikia, ukisoma kwa wikipedia maelezo kuhusu Israel kwenye suala la kidini ni Kuwa asilimia kubwa ya waisrael ni wayahudi then wanafuata waislamu na waliobakia kwa uchache wao ni wakristo na waumini wa dini nyinginezo, lakini hali ni tofauti huko ghaza ambapo majority ni waislamu then wakristo wapo nafasi ya pili kwa uwingi ila unalikuta jitu kutoka tz anasema bora tu hao wapalestina wafe bila kujua Kuwa wakristo wenzake nao pia ni wahanga wa vita.