Sheria ya Mirathi ya Kiislamu kwa mtoto wa nje ya ndoa ibadilishwe

Japo Quran haijataja mtoto wa nje ya ndoa popote Wala kusema asirithi,lakini nikujuze,kwenye sheria ya kiislam 'sharia' ni kwamba hakuna mwenye mamlaka ya kutoa au kuongeza kitu,ni wahyi/revelation,Ila sheria hiyo mtoto wa nje ya ndoa asimrithi baba yake siyo sheria ya uislam,uislam unatambua ni mwanao,inaita watoto wenu waluotoka migongoni mwenu,suala la mtoto wa nje ya ndoa limeeingizwa na wayahudi katika uislam
 
Nina swali moja linaleta utata.Nimeshuhudia kuna Mzee mmoja alikuwa ni Mwislamu(ameshatangulia mbele za haki),aliwajengea wanawake wawili nyumba mbili,kila mwanamke na nyumba yake,ila hakufunga nao ndoa alikuwa anaishi hivyohivyo na kuzaa nao watoto.Hadi anakufa hakuwahi kufunga ndoa..Sasa swali ni kwamba hapo watoto ni haki ya Baba yao au Mama zao.? Naomba jibu hapa tafadhali maana watoto wamegawanyika,wengine wamefuata Imani kwa Baba na wengine upande wa Mama zao maana akina Mama sio Waislamu.
 
Kama nyumba zina majina ya mama zao, watoto watarithi
 
kwanza huyo mzee ni smart zaidi na ndio inatakiwa kufanya ukiwa na watoto wa nje ...Kipind akiwa hai kuwajengea wote na kuwagaiya mali kabisa ni jambo zuri kawaida kwa vile mtoto ataweza kuchukua sehemu ya mali aliyopewa isipokuwa kurithi .

Ndio maana mtoto wa nje ya ndoa ataendelea kupewa huduma isipokuwa kurithi ,a anachopewa mzazi akiwa hai ni halali yake .

Jambo jingine, baada ya kufa kuna nafasi ya wosia mtoto huyo atapewa sehemu tu urithi ila hawezi kupata sawa na watoto wa ndani ya ndoa , mambo mengine ni familia kutoa kama ndugu yao anaweza kupata zaidi.

Kurithi na urithi inakuja baada ya mzazi kufa, ili kuruka mtego mape ma wape chao . Jamii nyingi zinafanay hivyo kaangalie watu wa Asia iwe hata kwa watoto ndoa wanapewa chao mapema . Kurithi ni kwa mtoto halali anayetambulika ukirejea ktk uislamu mtoto anapatikana baada ya ndoa , nje ya ndoa ni mtoto aliyepatika nje ya ndoa ni mali ya mama sio baba kwa hyo hana haki ya kurithi kwa baba kutokana hamna uhalali ya kuonyesha ni mwanae .

Kufuata dini inategemea na malezi yao na uelewa ila watoto hao wana uhalali kufauta kwa mama yao ,kutunzwa na mama zao .​
 
Upande wako unaona ni sawa kufanya hivo??
 
Sheria zao huwez kubadilisha as because ni tayari ruled out. Ila nimewah kusikia kwamba mtoto kama mtoto yeye hana kosa,na kosa litakuwa kwa wazaz na baba kamq anataka kumpa mwanae ampe akiwa hai kisiwe included kwenye malibya mirathi kama kumsomesha n.k
 

Wewe vipi sio kumpa bali ni haki yake maana yeye ndo kamleta duniani.
 
Ukristo hauelezi Mali za marehemu zitagawanywa vipi wala mahali italipwa vipi na kama kuna maelezo hayo kwenye biblia ni utamaduni wa eneo ilipoandikwa Biblia.

Ukristo sio utamaduni ila uislamu ni utamaduni wa sehemu flani ambao umekua ni dini.

Hivyo ishu za mgawanyo wa Mali kwenye ukristo zinategemea na Mkristo husika Yuko eneo lenye utamaduni gani kwani sio suala la dini.

Ukristo hauna habari ya mahali ila utamaduni wa eneo husika ndio unamahali.

Mkristo kama Alizaa nnje ya ndoa Mungu anaweza kumsamehe.
 
kubadilisha huwezi, kwasababu ipo ndani ya kuran. mtoto wa kambo ni mtoto haramu. kwahiyo ninyi nyote mliopo humu mliozaliwa nje ya ndoa, uislam unawatambua kama watoto haram. na hamstahili kurithi, labda kama mdingi atatoa 1/3 kama wasia, ila kwenye fungu kubwa hutakiwi hata kusogea.

dawa pekee ni kuukimbia uislam, njooni kwenye Ukristo, huku watoto wote ni sawa, wanapata mgao sawa, hakuna mwanadamu haramu. kila mtu kaletwa na Mungu kwa makusudi maalumu, hata kama alipatikana na changudoa, hata kama alipatikana guest house kwa namna yeyote, umezaliwa, jua Mungu wa wakristo anakupenda, anakuhesabia sawa na wengine, na wewe sio haram.
 
mtoto wa nje ya ndoa hana chake,ila baba anaweza kumkatia chochote kitu kwa huruma yake
 
Muongo wa Mungu unauhakika kwamba Mungu liwawambia hao wahuni waandike hio qurani au nikikundi kilikaa kikafikilia kuandika sheria zao binafsi tu
Sina neno, mambo ya Imani siji maana huyo mungu wa kuoa wake wanne na kukata watu shindi kwa lazma ili waende mbingu yao ndio nashangaa!
 
Hii nchi sio ya kidini kwaio hakuna ulazima wa kufuata waarabu walichoandika mirathi inagawanywa kiukoo fullstop
Umedandia treni kwa mbele, soma kichwa cha habari, jamaa kazungumzia "sheria za mirathi za kiislam" na sio za taifa la tanzania kiujumla..
 
Quran ni Version ya Biblia hasa Toratî.
Nikupe kîfungu kwenye Biblia kinachoonyesha mtoto wa nje hapewi

Na wewe lete ushahidi wa maneno yako, bado unaongea kwa utashi wa nafsi yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…