Accumen Mo
JF-Expert Member
- May 15, 2022
- 18,036
- 39,882
Suala hili limeondolewa mushkeri kwa sababu ni moja mtoto wa zinaa kuna kubambikiwa unawez kufikiria ni wao ila kwa kiasi kikubwa sio wako...Leo tunaona hawa wanawake wanaozaa bila ya ndoa wanachanganya watu tena wale ambao mtoto unakuta kafanana na mama.Katika Uislamu kitendo hicho cha zinaa ambacho kimefanywa na mwanaume na mwanamke ndio makosa na waliofanya wanafaa waadhibiwe hapa duniani ili wasafishwe kwa kosa lao hilo hadharani. Na Allah (Subhaanahu Wa Ta’ala) Ametuagizia Tusikaribie kabisa zinaa (17: 32). Lakini tufahamu ya kwamba yule mtoto anayezaliwa hana hatia yoyote. Allah (Subhaanahu Wa Ta’ala) Anasema:
“Na kila nafsi haichumii ila nafsi yake. Na habebi mwenye kubeba mzigo wa mwenziwe. Kisha marejeo yenu ni kwa Mola wenu Naye Atakuambieni mliyo kuwa mkitofautiana” (6: 164).
Na Mtume (Swalla Allaahu ‘Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam) amesema: ((Kila kinachozaliwa kinazaliwa katika Uislamu .....)) l-Bukhaariy).
Na haifai kwa Muislamu kumuita mtoto aliyezaliwa kwa jina la mwana-haramu kwa sababu mtoto mwenyewe si wa haramu bali kitendo chenyewe ndicho haramu. Na ieleweke kuwa mtoto huyu hataitwa kwa jina la huyu mwanaume aliyezini na mamake kwa sababu kisheria si mtoto wake wala hawa wawili hawarithiani kabisa. Mtoto huyu hatamrithi huyo mwanaume na huyo baba hatamrithi mtoto huyo. Lakini mtoto anaweza kumrithi mama yake na mama kumrithi mtoto wake.
Tanbihi kwa kila mmoja wetu ajichunge sana ili asiingie katika madhambi haya ya zinaa. Na ndio sheria ikafanya ndoa kuwa rahisi na ikaweka adhabu kali kwa wenye kuzini.
Mwanamke kama ni mzinifu basi hata mtoto atakudanganya tu , wapo watoto wana kadi za clinic zina majina ya baba tofauti hata watatu. Zinaa ni mbaya sana watoto hawa mara nyingi ni chanzo cha ugomvi ndani ya ndoa ingawa watoto hawana kosa .
Utafiti : Waliozaa nje ya ndoa wengi wanatengenisha watoto wao binafsi na kukosa umoja , juzi tu hapa kifo cha yule mtangaaji clouds yule mwanae mkubwa hana uhusiano mzuri na mdogo wake kisa hawajuani ila wanapendana .