Sheria ya Ndoa: Maswali na majibu mbalimbali

Sheria ya Ndoa: Maswali na majibu mbalimbali

Mh. Kuna kesi moja ya dada yangu ambayo mume alitelekeza familia ya watoto wawili akaenda kuishi kwingine na kimada. Mume yule akaenda mahakamani kufungua kesi ya talaka ili aweze kuoa yule kimada. Alifungua kesi 3 na zote talaka hakupata, Ya kwanza alitumia hati ya usuluhishi imepitwa na wakati, ya pili hakuhudhuria kesi ikafutwa, ya tatu akaomba restoration baada ya miaka kama mitatu kupita. Suprisingly, eti hakimu akakubali restoration!!!! (najua 90 days ndiyo utaratibu). Hata hivyo mdai hakufika mahakamani huku mdaiwa akiwa anahudhuria for 3 good years. Mwishowe ikafutwa tena. Sasa mdai ameamua kugeukia kanisani akiomba ndoa ibatilishwe!! Huko nako najua itagonga mwamba!!! Sasa kisheria mdai anaweza tena kurudi mahakama ya serikali kufungua tena kesi ya nne? Je kwa kuwa mdai alitelekeza familia bila sababu i.e he is not clean before the law) je anaweza kufungua kesi ya madai ya talaka? Je kati ya mke na mume huyu ni nani mwenye haki ya kufungua kesi ya talaka?

Mkuu Zogwale, mtiririko wa kesi hizo umejaa ukakasi na giza kisheria. Ieleweke kuwa,kufungua kesi/shauri ni haki ya kila mtu mwenye malalamiko dhidi ya mwingine au Serikali.Baada ya kufunguliwa kwa shauri,mfunguzji anakuwa na wajibu wa kuhakikisha shauri lake linafikia mwisho-ikiwa ni pamoja na kuhudhuria Mahakamani.

Kufunguafungua kesi bila ya mpango na utaratibu ni usumbufu kwa unayemlalamikia na Mahakama kwa ujumla.Lazima kuwe na sababu na hoja za kila kesi. Ningekuwa mimi,ningemuandama kwa mapingamizi huyo mume hadi akome.

Kimsingi, mume na mke wote wana haki ya kufungua kesi ya kudai talaka.Jambo la muhimu ni kuwa na sababu za kudai talaka zinazotambuliwa na kuainishwa kisheria.Sababu kuu za kudai talaka ni uasherati,mateso na kutelekeza. Pia,lazima taratibu za shauri husika zifuatwe ipasavyo-muda,kupitia Bodi ya Usuluhishi na kadhalika.
 
Last edited by a moderator:
kama ndiyo hivyo mbona wanamsakama Dr. Slaa kwamba kapora mke wa mtu kumbe sheria ziko wazi namna hii? Nawaomba MACCM yajifunze sheria hii ili wasiendelee kudhalilisha watu wenye matatizo ya kutokusimamisha. Au unaweza kuniambia kuna kosa lolote mtu anaweza kutenda kwa kumdhalilisha mtu asiyesimamisha?

Mkuu,bahati mbaya sijui vyema kilichojiri kuhusu shauri la Mchumba wa Dr.Slaa.Lakini,ndoa ikishabatilishwa na Mahakama,aliyekuwa mume au mke,ana haki ya kuoa au kuolewa tena.Nasisitiza kuwa,lazima maombi ya kubatilisha yawepo na ndoa husika ibatilishwe kweli na Mahakama baada ya kusikilizwa hoja wakati mzima wa shauri.
 
Vipi waliofunga ndoa kanisani 'mpaka kifo kiwatenganishe' Wanaweza funga ndoa nyingine baada ya ndoa ya kwanza kubatilishwa na mahakama?
 
Vipi waliofunga ndoa kanisani 'mpaka kifo kiwatenganishe' Wanaweza funga ndoa nyingine baada ya ndoa ya kwanza kubatilishwa na mahakama?

Ndiyo.Sheria ya Ndoa iko wazi kabisa.Kwamba,talaka hutolewa Mahakamani tu na huonesha ndiyo mwisho wa ndoa. Kama kanisa lina taratibu zake za hadi mmoja afe,hizo taratibu si sheria. Naogopa kuchanganya sheria na imani hapa.Nikuombe Mkuu nameless girl mimi niishie hapa.
 
Usiogope mkuu, please tuendelee kujifunza.
Mimi nijuavyo, Mahakama ina uwezo wa kuwatenganisha wanandoa ila si kuvunja ndoa kwani mahakama haina mamlaka ya kuingilia taratibu za kidini zilizowekwa. So utaseparate ila hautaweza kufunga ndoa kanisani mpaka mmojawapo anapofariki.
 
Nilichokiongea hapo juu,kinashadidiwa na kifungu hiki:

12.​
A marriage, whether contracted in Tanganyika or elsewhere,shall for all purposes of the law of Tanganyika subsist untildetermined-

(a) by the death of either party thereto;(b) by a decree declaring that the death of either party thereto ispresumed;(c) by a decree of annulment;(d) by a decree of divorce; or(e) by an extra-judicial divorce outside Tanganyika which is​
recognized in Tanganyika under the provisions of section 92.

Mkuu nameless girl, ndoa huvunjwa kwa talaka Mahakamani.Hilo ndilo jicho la kisheria. Kuhusu dini,hizo ni taratibu tu.Kila dini ina taratibu zake. Hata talaka tatu za kiislam,kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa ya Tanzania,hazivunji ndoa. Ni moja ya taratibu tu za kuelekea kwenye kuvunja ndoa. Ni Mahakama tu,kwa mujibu wa Sheria,yenye uwezo wa kuvunja ndoa. Ndiyo maana Waislam wanataka Mahakama ya Kadhi ambayo itatambua,pamoja na mambo mengine,kuvunjwa kwa ndoa ya kiislam kufuatia kutolewa kwa talaka tatu.
 
Sole mkuu uwepo wako nautambua sema kidole kilitereza nikiwa nataka kusema wewe ulimjibu Humble African. Nisamee bure uzee nao jamani!!
Mkuu, kwani nimeshadondosha kaswali hapa? Ama umemis uwepo wangu huku!!!
 
Nilichokiongea hapo juu,kinashadidiwa na kifungu hiki:

12.​
A marriage, whether contracted in Tanganyika or elsewhere,shall for all purposes of the law of Tanganyika subsist untildetermined-

(a) by the death of either party thereto;(b) by a decree declaring that the death of either party thereto ispresumed;(c) by a decree of annulment;(d) by a decree of divorce; or(e) by an extra-judicial divorce outside Tanganyika which is​
recognized in Tanganyika under the provisions of section 92.

Mkuu nameless girl, ndoa huvunjwa kwa talaka Mahakamani.Hilo ndilo jicho la kisheria. Kuhusu dini,hizo ni taratibu tu.Kila dini ina taratibu zake. Hata talaka tatu za kiislam,kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa ya Tanzania,hazivunji ndoa. Ni moja ya taratibu tu za kuelekea kwenye kuvunja ndoa. Ni Mahakama tu,kwa mujibu wa Sheria,yenye uwezo wa kuvunja ndoa. Ndiyo maana Waislam wanataka Mahakama ya Kadhi ambayo itatambua,pamoja na mambo mengine,kuvunjwa kwa ndoa ya kiislam kufuatia kutolewa kwa talaka tatu.

Kuna kesi fulani ilisimamiwa na Mh. Lamwai, kumradhi, jina limenitoka ilibeba facts kama hizo... anyway nikiipata nitarudi...
 
Swali kidogo Petro E. Mselewa, nameless girl na Nyani Ngabu, labda mme ameoa na wamekaa wote na kuzaa watoto lakini mke amekuwa chanzo cha kutoelewana ndani ya ndoa kwa miaka, na ugomvi husioisha ukianzishwa na mke na mme akaamua kukaa naye bila mahusiano kwa miaka 5 na hataki kwenda mahamakani, je anaweza kuoa mke mwingine akiwa ndani ya inactive marriage hiyo? Je Mke wake halali akikataa kuruhusu ndoa hiyo mpya kuna sheria itamzuia mme kuoa kwa kutumia lazima?
 
Mkuu, ngoja nikugawie kile ninachokijua, ni hivi:

Kutokana na kifungu cha 107 cha sheria za ndoa (LMA Cap 29), kinatoa sababu ambazo zinaweza kufanya ndoa hiyo kuvunjika. Sababu zenyewe ni Uzinzi ama Ugoni, Ukatili, Kutengana, kifungo cha jela, mental illness.

Kabla ya kwenda mahakamani, mnapaswa kwenda kwenye Baraza la usuluhishi wa Ndoa kwanza exception ni pale mmoja wapo anapogoma kwa makusudi kwenda huko. Kifungu cha 101(c). Hapo utahamia mahakamani ambapo utaiomba mahakama kutoa talaka, kugawanya mali za wanandoa kama zipo, matunzo ya watoto kama wapo.

Mahakama itatoa amri ya kumuita mwenzako ili kujibu hayo uliyolalamikia. Kama utaamua kufunga ndoa na mtu mwingine ilihali talaka haijatika mahakamani, mkeo anayo haki ya kupinga ndoa hiyo kwani ndoa inakua bado inatambulika kisheria. Na pia ikumbukwe, ndoa inaweza kubatilishwa mahakamani ikiwa ni ya miaka miwili au na zaidi.

Natumaini umenielewa Mkuu.
 
Hiyo naelewa lakini swali langu la msingi ni kwamba wameshindwa kuelewana na kisa ni mke ambaye anamburuza mme katika maisha yao ya ndoa na mme sasa kachoka. Mahakamani hataki kwenda akijua usumbufu na milolongo iliyopo. Kile alichoamua ni kukaa bila kujamiana kwa miaka kadhaa na sasa anahamua kuoa mke mwingine. Je mke halali anaweza kuingilia ndoa isiwepo? Chukulia ndoa inayotaka kufanya ni ndoa ya kimila ambayo haina masharti mengi kama ya kutangazwa. Na je mke akiizuia mme anaweza kukaa na huyu mke mpya?
Mkuu, ngoja nikugawie kile ninachokijua.. ni ivi:
Kutokana na kifungu cha 107 cha sheria za ndoa (LMA Cap 29), kinatoa sababu ambazo zinaweza kufanya ndoa hiyo kuvunjika. Sababu zenyewe ni Uzinzi ama Ugoni, Ukatili, Kutengana, kifungo cha jela, mental illness...
Kabla ya kwenda mahakamani, mnapaswa kwenda kwenye Baraza la usuluhishi wa Ndoa kwanza exception ni pale mmoja wapo anapogoma kwa makusudi kwenda huko. Kifungu cha 101(c).
Hapo utahamia mahakamani ambapo utaiomba mahakama kutoa talaka, kugawanya mali za wanandoa kama zipo, matunzo ya watoto kama wapo...
Mahakama itatoa amri ya kumuita mwenzako ili kujibu hayo uliyolalamikia.
Kama utaamua kufunga ndoa na mtu mwingine ilihali talaka haijatika mahakamani, mkeo anayo haki ya kupinga ndoa hiyo kwani ndoa inakua bado inatambulika kisheria.
Na pia ikumbukwe, ndoa inaweza kubatilishwa mahakamani ikiwa ni ya miaka miwili au na zaidi.
Natumaini umenielewa Mkuu.
 
Hiyo naelewa lakini swali langu la msingi ni kwamba wameshindwa kuelewana na kisa ni mke ambaye anamburuza mme katika maisha yao ya ndoa na mme sasa kachoka. Mahakamani hataki kwenda akijua usumbufu na milolongo iliyopo. Kile alichoamua ni kukaa bila kujamiana kwa miaka kadhaa na sasa anahamua kuoa mke mwingine. Je mke halali anaweza kuingilia ndoa isiwepo? Chukulia ndoa inayotaka kufanya ni ndoa ya kimila ambayo haina masharti mengi kama ya kutangazwa. Na je mke akiizuia mme anaweza kukaa na huyu mke mpya?

Hapo nadhani itadepend na mila husika. Hao wanandoa watakaa na wazee wao ambao wao watatoa maamuzi kulingana na mila husika.
Mfano, kuna mila zingine, mwanaume anapotaka kumuacha mkewe basi anapaswa kurudisha mahari. So inategemea na mila husika.
 
Swali kidogo Petro E. Mselewa, nameless girl na Nyani Ngabu, labda mme ameoa na wamekaa wote na kuzaa watoto lakini mke amekuwa chanzo cha kutoelewana ndani ya ndoa kwa miaka, na ugomvi husioisha ukianzishwa na mke na mme akaamua kukaa naye bila mahusiano kwa miaka 5 na hataki kwenda mahamakani, je anaweza kuoa mke mwingine akiwa ndani ya inactive marriage hiyo? Je Mke wake halali akikataa kuruhusu ndoa hiyo mpya kuna sheria itamzuia mme kuoa kwa kutumia lazima?

Mkuu Mwananchi,asante kwa swali lako. Kwanza,inategemea namna ya ndoa iliyopo.Kama ya wake wengi,anaweza kuoa tena hata kama mkewe anakataa.Kama ni ndoa ya mke mmoja,hawezi kuoa tena isipokuwa tu kama ameshavunja ndoa ya mwanzo Mahakamani.
 
Last edited by a moderator:
Mambo ya ndoa magumu ni mkataba mkumu kuvunja kuliko mikataba mingine. Hata kama mwenzako anabreach contract masharti ni magumu kufikia kuvunja japo watu wengi uwa wanafikiri ni rahisi
Mkuu Mwananchi,asante kwa swali lako. Kwanza,inategemea namna ya ndoa iliyopo.Kama ya wake wengi,anaweza kuoa tena hata kama mkewe anakataa.Kama ni ndoa ya mke mmoja,hawezi kuoa tena isipokuwa tu kama ameshavunja ndoa ya mwanzo Mahakamani.
 
Wana-JF,karibuni hapa kwa maswali mbalimbali yahusuyo Sheria ya Ndoa,1971.Wale wote waliopo kwenye ndoa na wanaotarajia kuwa kwenye ndoa wanakaribishwa hapa kuuliza na kujibiwa. Nitashirikiana na Mawakili Wasomi wenzangu waliopo humu kuwajibu maswali yenu.

Mods, mnaweza kuufanya uzi huu kuwa 'sticky'? Asanteni na karibuni!

Swali, Je, mwanamke ambae hakufunga ndoa na mwanaume na wameishi zaidi ya miaka kumi kama mke na mume na kujaaliwa kupata watoto. Endapo mume kamchoka mke na kuamua kumfukuza je huyo mke ana haki zipi na kwa taratibu zipi
(a) Haki katika mali za ndoa walizo chuma au kuziendeleza pamoja?
(b) Haki za kuona, kuhudumia au kulea watoto?
(c) Haki ya kuolewa kama akipata mpiga show mwingine?
 
Mheshimiwa sana Tunashukuru kwa kujitolea kwako kuondoa wananchi Ukungu kuhusu sheria hii inayopelekea mkataba mgumu ambao wengi wetu huwa tunadumbukia kwa kizio cha Mapenzi,na baadae huwa ni kilio na kusaga meno.Umejitolea at No Cost but surely that will get compensanted.
Naomba nikuulize Maswali machache.
1)Ikiwa mmoja wa wanandoa anaingia kwenye ndoa ila nyuma yake ana ajenda ya siri mfano kufaidika na Mali au kwa namna yoyote je mwathirika hapa sheria hii ya Ndoa inamteteaje.
2)Ikiwa Mume amejenga na walipo oana wakaendelea kuishi hapo hapo so sheria ina badilisha nyumba hii from private owned to Matrimonial home?
3) Kutokana na (1)(2)above Je Vp mfano Mke akiondoka bila vigezo vyovyote kama Manyanyaso,Uasherati nk.nakurudi kwao kwa Muda wa zaidi ya mwaka mmoja?mf Mahakama ikivunja hii ndoa mke atakuwa na haki ya kudai share yake?
4)From na(3)above, mmoja akiamua kuwa na Mahusiano kwingine sheria inasemaje hapa?
5)Sheria inatambua mabaraza yapi ya usuluhishi?Kanisa,Misikiti au sinagogues zinakubalika pia?
Ninamaswali Mengi zaidi lakini kwa sasa huenda mengine yakajibiwa kutokana na Majibu hapo Juu.
 
Back
Top Bottom