Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,307
- 25,932
Mh. Kuna kesi moja ya dada yangu ambayo mume alitelekeza familia ya watoto wawili akaenda kuishi kwingine na kimada. Mume yule akaenda mahakamani kufungua kesi ya talaka ili aweze kuoa yule kimada. Alifungua kesi 3 na zote talaka hakupata, Ya kwanza alitumia hati ya usuluhishi imepitwa na wakati, ya pili hakuhudhuria kesi ikafutwa, ya tatu akaomba restoration baada ya miaka kama mitatu kupita. Suprisingly, eti hakimu akakubali restoration!!!! (najua 90 days ndiyo utaratibu). Hata hivyo mdai hakufika mahakamani huku mdaiwa akiwa anahudhuria for 3 good years. Mwishowe ikafutwa tena. Sasa mdai ameamua kugeukia kanisani akiomba ndoa ibatilishwe!! Huko nako najua itagonga mwamba!!! Sasa kisheria mdai anaweza tena kurudi mahakama ya serikali kufungua tena kesi ya nne? Je kwa kuwa mdai alitelekeza familia bila sababu i.e he is not clean before the law) je anaweza kufungua kesi ya madai ya talaka? Je kati ya mke na mume huyu ni nani mwenye haki ya kufungua kesi ya talaka?
Mkuu Zogwale, mtiririko wa kesi hizo umejaa ukakasi na giza kisheria. Ieleweke kuwa,kufungua kesi/shauri ni haki ya kila mtu mwenye malalamiko dhidi ya mwingine au Serikali.Baada ya kufunguliwa kwa shauri,mfunguzji anakuwa na wajibu wa kuhakikisha shauri lake linafikia mwisho-ikiwa ni pamoja na kuhudhuria Mahakamani.
Kufunguafungua kesi bila ya mpango na utaratibu ni usumbufu kwa unayemlalamikia na Mahakama kwa ujumla.Lazima kuwe na sababu na hoja za kila kesi. Ningekuwa mimi,ningemuandama kwa mapingamizi huyo mume hadi akome.
Kimsingi, mume na mke wote wana haki ya kufungua kesi ya kudai talaka.Jambo la muhimu ni kuwa na sababu za kudai talaka zinazotambuliwa na kuainishwa kisheria.Sababu kuu za kudai talaka ni uasherati,mateso na kutelekeza. Pia,lazima taratibu za shauri husika zifuatwe ipasavyo-muda,kupitia Bodi ya Usuluhishi na kadhalika.
Last edited by a moderator: