Sheria ya Ndoa: Maswali na majibu mbalimbali

Cheti gani cha ndoa ni bora kuliko kingine...
Cha serikali
Au cha Kanisan..?
 
Nilimanisha labda kikazi au kisomi
Unaombwa ulete cheti cha ndoa.

Alie peleka cheti kutoka serikalini ni bora
Kuliko aliepeleka cheti kutoka Kanisani
 
Wakuu, usuluhishi wa mabaraza ya kata una expiry date au hauna? Mfano ndoa imepata misukosuko sana mpaka mkapelekana baraza la usuluhishi na likakiri kwamba limeshindwa muende mahakamani, then somehow kwa sbabau mbalimbali mkajikuta mmeendelea kuishi kama wanandoa mfano kwa mwaka au zaidi hata mkaongeza mtoto/watoto na matatizo ya ugomvi yakatokea tena, je unaweza kutumia hati ile ya baraza la kati kuanzisha mchakato wa talaka mahakamani?
 
Wakuu, usuluhishi wa mabaraza ya kata una expiry date au hauna? Mfano ndoa imepata misukosuko sana mpaka mkapelekana baraza la usuluhishi na likakiri kwamba limeshindwa muende mahakamani, then somehow kwa sbabau mbalimbali mkajikuta mmeendelea kuishi kama wanandoa mfano kwa mwaka au zaidi hata mkaongeza mtoto/watoto na matatizo ya ugomvi yakatokea tena, je unaweza kutumia hati ile ya baraza la kata kuanzisha mchakato wa talaka mahakamani? c. c. Petro E. Mselewa
 
Mkuu,kila jambo la kisheria hufanywa ndani ya muda fulani. Kuhusu hati ya usuluhishi,hakuna muda ulioandikwa kisheria. Lakini,katika mazoea yapasa kuwa siku zisizozidi thelathini tangu hati kutolewa.
 
Mkuu,kila jambo la kisheria hufanywa ndani ya muda fulani. Kuhusu hati ya usuluhishi,hakuna muda ulioandikwa kisheria. Lakini,katika mazoea yapasa kuwa siku zisizozidi thelathini tangu hati kutolewa.
Asante kwa maelezo hayo. Swali la nyongeza ni je, naweza kutumia hiyo nakala ya maamuzi ya baraza la usuluhishi ya Enzi hizo (kama miaka 2 hivi nyuma) kuanzisha mchakato wa Talaka mahakamani bila kulazimika kurudia tena kupeleka kesi upya baraza la usuluhishi? Mahakama itayakubali hayo maamuzi? Pia naomba kufahamishwa kama aliyepeleka kesi baraza la usuluhishi anaweza kubadilika kuwa mshitakiwa badala ya mshitaki. Samahani hii ni real case inayoendelea, naomba msaada wako wa ufafanuzi. Petro E. Mselewa
 

Hauwezi mkuu. Yakupasa kuanza upya mchakato
 


Nashukuru sana mkuu kwa darasa murua. Mimi nina kesi yangu ambayo iko mahakamani ambayo nimefuata taratibu zote za kutaka kuomba talaka na mgawanyo wa mali. Mume wangu aliondoka nyumbani zaidi ya miezi miwili na kwenda kuishi na kimada hapahapa Dar. Tumekuwa kwenye ndoa zaidi ya miaka minne na mwaka jana mwezi wa tisa niliondoka pale nyumbani baada ya yeye kunitishia kwamba angenifanyia kitu mbaya kama ninngeendela kukaa pale. Nyumba aliipangisha siku mbili baada ya mimi kuondoka.

Nilienda polisi kutoa taarifa za kutishiwa , nikapewa namba namba ya kumbukumbu ambayo nimeambatanisha kwenye madai yangu pamoja na ushahidi mwingine. Kuna gari yangu ambayo imetokana na mali yangu binafsi ambayo aliondoka nayo. Hiyo gari nililipwa na bima baada ya gari ambayo niliipata kabla ya ndoa kupata ajali, na yeye ndio alisababisha ajali hiyo. Kabla ya kubadilisha jina aliondoka na mkataba wangu pamoja na kadi ya gari na akakataa kunirudishia akidai kwamba ile ni mali yetu sote.

Nimepata taarifa kwamba gari ile ameshaiuza na emenunua gari jingine. Je mahakama inaweza kuamuru gari ile iliyouzwa ikamatwe? baada ya mimi kuomba hata ya kuikamata ile gari?

Nawasilisha mkuu
 

Mkuu Nacherewa unapaswa kuthibitisha tu mahakamani kuwa gari hilo lilikuwa mali yako binafsi. Amri zingine zitafuata zikiombwa.
 
Asante kwa kutuelimisha,naona Uzi huu kwangu umekuja muda sahihi maana nnakesi ipo ngazi ya baraza la kata,
Nilioa nikiwa na watoto wa nje,baadae nkapata mtoto mmoja na mke wangu,tuliingia mgogoro,kila mtu akawa anajihudumia japo tuliishi nyumba moja,mm nikanunua kiwanja na kuanza kufyatua tofali,mwenzangu wakati nipo kazini akauza baadhi ya samani za ndani na kutoroka,nikatoa taarifa polisi,nikaendelea na ujenzi nikamaliza na kuhamia,baadae akarudi,baada ya miezi mitatu kuna hela akachukua kitapeli kwangu na akaondoka tena,safari hii akaniachia mtoto ana miaka mitatu,nikakaa nae mwaka,baadae nikamfuata na wazazi wakaomba nimsamehe,sasa naanza vurugu,anawafukuza wale watoto alonikuta nao,anawatukana na kunitolea matusi makubwa mbele yao, nilimrekodi baadhi ya matusi yake,kifupi anadai nyumba iuzwe agawiwe chake aanze maisha yake,
Ni mama wa nyumba ni tu,aliporudi alikuta nimejenga na kununua samani za ndani,
Nimeenda kanisani na sasa nipo baraza la kata,nnacho taka ni kuomba talaka kuepusha matusi kwangu na watoto na kikubwa nifanyeje kuokoa nyumba isiuzwe ibaki Mali yangu ama ya watoto,jina la hati na risiti za ununuzi vifaa ni langu,na hajui hata kiwanja nlinunua kwa nani na sh ngapi,mtoto nlozaa nae ana miaka saba sasa,niishie hapa kwanza,nataka nyumba na mtoto nibaki navyo salama,msaada tafadhari,
 
Hamuwezi kuacjana hadi ipite miaka 2 ya kuishi pamoja according to Sect 160 of marriage Act.1970
 
Naomba kuuliza utaratibu wa kupata hati ya talaka upoje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…