Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,307
- 25,932
Sawa mkuuNaomba usisahau mkuu, najua umeanzisha thread hii ili watu wapate elimu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sawa mkuuNaomba usisahau mkuu, najua umeanzisha thread hii ili watu wapate elimu.
Vyote sawa mbele ya sheria. Tenganisha sheria na imani tafadhaliCheti gani cha ndoa ni bora kuliko kingine...
Cha serikali
Au cha Kanisan..?
Shukrani za dhati mkuu, naomba kuuliza tena je sheria zingine naweza kuzipataje kwa mfumo huo wa PDF?
Mkuu,kila jambo la kisheria hufanywa ndani ya muda fulani. Kuhusu hati ya usuluhishi,hakuna muda ulioandikwa kisheria. Lakini,katika mazoea yapasa kuwa siku zisizozidi thelathini tangu hati kutolewa.Wakuu, usuluhishi wa mabaraza ya kata una expiry date au hauna? Mfano ndoa imepata misukosuko sana mpaka mkapelekana baraza la usuluhishi na likakiri kwamba limeshindwa muende mahakamani, then somehow kwa sbabau mbalimbali mkajikuta mmeendelea kuishi kama wanandoa mfano kwa mwaka au zaidi hata mkaongeza mtoto/watoto na matatizo ya ugomvi yakatokea tena, je unaweza kutumia hati ile ya baraza la kata kuanzisha mchakato wa talaka mahakamani? c. c. Petro E. Mselewa
Mkuu,unaweza ku-google na kupataShukrani za dhati mkuu, naomba kuuliza tena je sheria zingine naweza kuzipataje kwa mfumo huo wa PDF?
Asante kwa maelezo hayo. Swali la nyongeza ni je, naweza kutumia hiyo nakala ya maamuzi ya baraza la usuluhishi ya Enzi hizo (kama miaka 2 hivi nyuma) kuanzisha mchakato wa Talaka mahakamani bila kulazimika kurudia tena kupeleka kesi upya baraza la usuluhishi? Mahakama itayakubali hayo maamuzi? Pia naomba kufahamishwa kama aliyepeleka kesi baraza la usuluhishi anaweza kubadilika kuwa mshitakiwa badala ya mshitaki. Samahani hii ni real case inayoendelea, naomba msaada wako wa ufafanuzi. Petro E. MselewaMkuu,kila jambo la kisheria hufanywa ndani ya muda fulani. Kuhusu hati ya usuluhishi,hakuna muda ulioandikwa kisheria. Lakini,katika mazoea yapasa kuwa siku zisizozidi thelathini tangu hati kutolewa.
Asante kwa maelezo hayo. Swali la nyongeza ni je, naweza kutumia hiyo nakala ya maamuzi ya baraza la usuluhishi ya Enzi hizo (kama miaka 2 hivi nyuma) kuanzisha mchakato wa Talaka mahakamani bila kulazimika kurudia tena kupeleka kesi upya baraza la usuluhishi? Mahakama itayakubali hayo maamuzi? Pia naomba kufahamishwa kama aliyepeleka kesi baraza la usuluhishi anaweza kubadilika kuwa mshitakiwa badala ya mshitaki. Samahani hii ni real case inayoendelea, naomba msaada wako wa ufafanuzi. Petro E. Mselewa
Wana-JF,
Karibuni hapa kwa maswali mbalimbali yahusuyo Sheria ya Ndoa,1971.Wale wote waliopo kwenye ndoa na wanaotarajia kuwa kwenye ndoa wanakaribishwa hapa kuuliza na kujibiwa. Nitashirikiana na Mawakili Wasomi wenzangu waliopo humu kuwajibu maswali yenu.
Asanteni na karibuni!
Nashukuru sana mkuu kwa darasa murua. Mimi nina kesi yangu ambayo iko mahakamani ambayo nimefuata taratibu zote za kutaka kuomba talaka na mgawanyo wa mali. Mume wangu aliondoka nyumbani zaidi ya miezi miwili na kwenda kuishi na kimada hapahapa Dar. Tumekuwa kwenye ndoa zaidi ya miaka minne na mwaka jana mwezi wa tisa niliondoka pale nyumbani baada ya yeye kunitishia kwamba angenifanyia kitu mbaya kama ninngeendela kukaa pale. Nyumba aliipangisha siku mbili baada ya mimi kuondoka.
Nilienda polisi kutoa taarifa za kutishiwa , nikapewa namba namba ya kumbukumbu ambayo nimeambatanisha kwenye madai yangu pamoja na ushahidi mwingine. Kuna gari yangu ambayo imetokana na mali yangu binafsi ambayo aliondoka nayo. Hiyo gari nililipwa na bima baada ya gari ambayo niliipata kabla ya ndoa kupata ajali, na yeye ndio alisababisha ajali hiyo. Kabla ya kubadilisha jina aliondoka na mkataba wangu pamoja na kadi ya gari na akakataa kunirudishia akidai kwamba ile ni mali yetu sote.
Nimepata taarifa kwamba gari ile ameshaiuza na emenunua gari jingine. Je mahakama inaweza kuamuru gari ile iliyouzwa ikamatwe? baada ya mimi kuomba hata ya kuikamata ile gari?
Nawasilisha mkuu
Mkuu Nacherewa unapaswa kuthibitisha tu mahakamani kuwa gari hilo lilikuwa mali yako binafsi. Amri zingine zitafuata zikiombwa.
Karibu tena mkuu. Kukiwa na zaidi tuwasilianeAsante sana
Asante kwa kutuelimisha,naona Uzi huu kwangu umekuja muda sahihi maana nnakesi ipo ngazi ya baraza la kata,Mkuu chanika holdings,mgawanyo wa mali (machumo) utahusu mali zile za pamoja tu.Hii ni kwasababu,katika ndoa kuna mali za pamoja za wanandoa na zile binafsi.Ushahidi wa mali binafsi ukitolewa,mali husika hazitakuwa katika mgawanyo. Fahamu ya kwamba,katika mgawanyo wa mali mtoto/watoto hawahusiki.Sababu ni rahisi mno.Ni kuwa wao hawakuwa wanandoa. Masuala ya ndoa ni tofauti ya masuala ya mirathi.
Katika mgawanyo wa mali,Mahakama huangalia mchango wa kila mwanandoa katika kupatikana kwa mali hiyo. Katika kesi maarufu ya kindoa kati ya Bi Hawa Mohamedi na Bwana Ally Sefu, Mahakama ilitambua mchango wa mama wa nyumbani katika machumo. Hivyobasi, hata kama mke alikuwa ni mama wa nyumbani,atapata mgawanyo kadiri ambavyo Mahakama itaona inafaa kwa kuzingatia mchango wake na mambo mengineyo yaliyojitokeza kwa wanandoa hao kuhusiana na mali.
Hamuwezi kuacjana hadi ipite miaka 2 ya kuishi pamoja according to Sect 160 of marriage Act.1970Mkuu Daata, kulingana na Sheria tajwa,ndoa ni muungano wa mwanaume na mwanamke wenye lengo la kuwafanya waishi pamoja katika maisha yao yote na katika kujitenga na wengine wote waliobaki. Ndoa ina taratibu zake Mkuu.Hakuna aina au namna yoyote ya ndoa inayotokana na kuishi na mwanamke au mwanaume kwa muda fulani. Dhanio la ndoa lililopo chini ya kifungu cha 160 cha Sheria ya Ndoa huwahusu wau waliohitilafiana na ambao waliishi kwa miaka miwili au zaidi.
Naomba kuuliza utaratibu wa kupata hati ya talaka upojeWana-JF,
Karibuni hapa kwa maswali mbalimbali yahusuyo Sheria ya Ndoa,1971.Wale wote waliopo kwenye ndoa na wanaotarajia kuwa kwenye ndoa wanakaribishwa hapa kuuliza na kujibiwa. Nitashirikiana na Mawakili Wasomi wenzangu waliopo humu kuwajibu maswali yenu.
Asanteni na karibuni!