JFK wabongo
JF-Expert Member
- Aug 11, 2015
- 3,887
- 3,197
Petro E. Mselewa Hii comment hujaiona au bado unatafuta nondo?Je sheria inaruhusu kubadilisha ndoa kutoka kuwa ya mke mmoja kuwa ya wake wengi? Kama ndiyo, taratibu zikoje?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Petro E. Mselewa Hii comment hujaiona au bado unatafuta nondo?Je sheria inaruhusu kubadilisha ndoa kutoka kuwa ya mke mmoja kuwa ya wake wengi? Kama ndiyo, taratibu zikoje?
Habari zenu wadau
Wahenga walisema kwenye wengi hapaharibiki jambo, natumai humu wapo watalamu wa sheria kuhusu ndoa naomba tupeane uelewa kuhusu mambo mbali mbali kuhusu sheria za ndoa mfano
1) ili ndoa iwe halali kipi kinaitajika kufanyika
2)Je serikali ya Tanzania ina tambua ndoa za aina ngapi
3) Kuna maneno mitaani kuwa ukiishi na mwanamke miezi mitatu ni mkeo kisheria je hapo ikoje?
4)Je mwanamke ambaye umeishi naye bila ndoa ana haki ipi mkiachana
Karibuni wadau
Samahani kama huna cha kuchangia pita kimya kimya
Mkuu Peter, nirleweshe vizuri hapo kama tumejebga nyumba 3 na Mzee alafu kwenye wosia akamuandika mwanae wa nje? He nitawezaje kupinga?Mkuu Victoire, kwanza yategemea namna ya ndoa iliyofungwa baina yenu.Kama ni ya kiislam,kwa mfano,watoto wa nje ya ndoa hawawezi kurithi. Kama ni ndoa ya kimila,yategemea mila za kabila lenu husika. Kama ni ndoa ya Bomani, yategemea na makubaliano yenu katika ndoa yenu.Hii ni kwakuwa,kifungu cha 58 cha Sheria ya Ndoa kinaruhusu uwepo wa Makubaliano juu ya umiliki wa mali za ndoa.Umiliki ndio unaelekeza urithi hapo baadaye.
Nataka nieleweke kuwa, kama mali ni binafsi kama inavyoruhusiwa chini ya vifungu vya 56 na 57,urithi waweza kufuata sheria,mila au Wosia.Lakini,kama ni mali ya pamoja watoto wa nje ya ndoa (kwa ndoa za bomani na za kikristo) hurithi kutokana na matakwa ya wanandoa tu na si vinginevyo.
Mkuu, mimi naitwa Petro na wala si Peter. Wosia si jambo lisilopingwa. Utaupinga kama umejumuisha mali au warithi wasiotakiwa. Ni jambo la kuthibitisha tu. Kama unapinga kujumuishwa kwa mrithi fulani, utajenga hoja zako na kueleweka tu.Mkuu Peter, nirleweshe vizuri hapo kama tumejebga nyumba 3 na Mzee alafu kwenye wosia akamuandika mwanae wa nje? He nitawezaje kupinga?
Sorry petro simu inajiedit. Asante!Mkuu, mimi naitwa Petro na wala si Peter. Wosia si jambo lisilopingwa. Utaupinga kama umejumuisha mali au warithi wasiotakiwa. Ni jambo la kuthibitisha tu. Kama unapinga kujumuishwa kwa mrithi fulani, utajenga hoja zako na kueleweka tu.
Nenda Mahakama ya Watoto ukafungue shauri la Custody. Ni jambo jepesi na la kawaida kisheria.Sijafunga nae ndoa, Nataka nimchukue mwanangu, ana kazi na mimi nina kazi.
Umeshajijibu. Ha ha ha ha ha haMkuu, ina maana vigezo vya kutalakiana ndo ivyo vitatu tu? Mateso, uasherati na utelekezwaji?
Vipi kuhusu kutokua na maelewenao?
Presumption of marriage sec 160 of law of marriage act sheria imesema ni miaka 2 inakuwa ndoa na jamii inayo wazunguka itambue kuwa mnaishi km mke& Mme na hio ndoa haina taraka Ila INA mgao WA Mali na maintenance of children and custody km ikivunjika (broken down irreparably) obiter dictum#Mkuu Petro na wengine.
Ni kipindi gani ukiishi na mwanamke ambye hujamuoa ataesabika kuwa ni mkeo.
thanksPresumption of marriage sec 160 of law of marriage act sheria imesema ni miaka 2 inakuwa ndoa na jamii inayo wazunguka itambue kuwa mnaishi km mke& Mme na hio ndoa haina taraka Ila INA mgao WA Mali na maintenance of children and custody km ikivunjika (broken down irreparably) obiter dictum#
Sema kwa upande wa ndoa ya Kiislam, Sheria itakayotumika mahakamani ni Sheria ya Kiislam. Kwao hakuna kupitia mabaraza ya usuluhishi.Kwanza,talaka ni mwisho wa ndoa.Pili,talaka hutolewa na Mahakama tu na si vinginevyo.Tatu, talaka ina taratibu zake.Kwa mfano,ni lazima kwa mwombaji wa talaka apitie katika Baraza la Usuluhishi la Ndoa kabla ya kwenda Mahakamani kudai talaka. Pia,Baraza husika lazima litoe kibali cha kushindwa kuwasuluhisha wanandoa hao ambao mmoja wao anataka kutalikiwa. Nne, talaka hutolewa tu pale ambapo ndoa hiyo itaonekana kuwa haiwezi tena kubaki a kurekebishika.
Kimsingi,Mahakama hulenga hasa katika kuilinda ndoa.Ndiyo maana,mwombaji wa talaka lazima athibitishe uwepo wa sababu za talaka kwa mfano mateso,kutelekezwa na uasherati wa mwenza wake.Ieleweke kuwa talaka zitolewazo kiislam ni hatua tu.Hii ni kwakuwa ni Sheria ya Ndoa tu ndiyo inayotumika katika suala hilo.