Sheria ya Ndoa: Maswali na majibu mbalimbali

Sheria ya Ndoa: Maswali na majibu mbalimbali

Usiumize kichwa nakazi ,soma kitu kinaitwa family law.ukimaliza uje unambie utakuta kunavifungu huko namahakama inasimamia.soma

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo family law ipo chini ya marriage act au? Hapa tunaongelea sheria za ndoa, yaani ingekuwa miezi mi au 6 umekaa na mtu halafu majirani wakatambua kwamba ni mke na mume mi nadhani wanawake wote wangekuwa ni wake za watu muda huu, again weka link ya hicho kipengele hapa kila mtu aone, hicho kitu hakipo.
 
Hiyo sheria imeshapitwa na wakati. Hivi nikiishi na mwanamke kwa muda wa miezi 6 na majirani wakatutambua kama mume na mke hiyo inatambulika kwamba ni 'Presumption of marriage'?. Sheria iliyopo inforce currently inatamka wazi kwamba mkiishi kama mume na mke kwa muda wa miaka miwili chini ya paa moja. Kwahiyo udhibitishe kwamba mliishi kwa miaka miwili, dhibitisha kwamba mliishi chini ya paa moja, na dhibitisha kwamba mliishi kama mume na mke, hayo ndio matakwa ya sheria ya sasa.
Sheria ya sasa ni IPI hiyo maana sheria iliyopo ni ya 1971.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sio miaka miwil wala miez sita...ni miezi mitatu tu anakua mke kiserikali popote anasikilizwa kama majran wakithibitisha mlikua mkiishi kama mke na mume na anapata haki zote kama mke hyo nimeiskia juzi na kwel huyo dada alipata haki yake

ndoa ya kimila ni ile mahari wanayopokea ndug au wazaz...barua humaanisha uchumba lkn mahari humaanisha ndoa hyo ndo ndoa ya kimila...na huwa wanauliza mwenzako utamuacha au utaondoka naye?? wakimaanisha ndo mwenza wako tayar

Sent using Jamii Forums mobile app
 
neel ne,
Kwani tunajadili utashi au sheria, hayo unayoyasema yapo kwenye sheria ipi ya mwaka upi na kifungu kipi?
 
Inakuwa presumed ili mwanamke na watoto wasiondoke kapa na siyo kusema ni ndoa halali.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani ndoa kamili na ndoa presumed inatofauti gani katika kutalakiana? Kwamba ndoa kamili huwa wanatoka kapa na ndoa presumed ndio hawatoki kapa? Haiwezekani pakawa na sheria mbili juu ya jambo moja zinazokinzana, its illegal kuwa na sheria inayopingana na sheria. Na sheria ya presumption of marriage ipo na iko clear bila kupepesa macho.

Ni miaka miwili kama mume na mke chini ya paa moja, nothing more, nothing less. Sasa kama unadai kuna sheria nyingine inayodefine 'Presumption of marriage' otherwise basi hiyo sheria ni ya kihalifu, maana inakinzana na sheria nyingine halali juu ya jambo hilo hilo.

Hivi leo sheria iseme kwamba ndoa ni muunganiko kati ya wanamme na mwanamke, halafu sheria nyingine ije tena iseme ni muunganiko wa mwanamume na mwanamume au mwanamke na mwanamke au mwanaume na mwanamke, huoni sheria moja tayari inavunja sheria ya nyingine, hivyo its illegal.
 
Majirani kama waliwstambua kama mke na mume yatosha ila inakuwa presumed tu ili kila upande upate mgao kwenye mali mliyochuma kama IPO na matunzo ya watoto kama wapo.sheria ya ndoa 1971 kifungu 160.

Sent using Jamii Forums mobile app
Halafu kumbe wewe jamaa ni mpuuzi sana, nimetafuta hicho kifungu namba 160 cha Marriage act ya 1971, mbona ina re-affirm ninachosema kwamba ni miaka miwili kama mume na mke chini ya paa moja? Au lugha ya kiingereza inayotumika ndio inakusumbua?, sheria hiyo hapo chini, mwenye macho na asome. Hiyo ya majirani unayoisema sijui hata umeitoa wapi??!!!

==============================

160. Presumption of marriage
(1) Where it is proved that a man and woman have lived together for two years or
more,
in such circumstances as to have acquired the reputation of being husband and
wife, there shall be a rebuttable presumption that they were duly married.
(2) When a man and a woman have lived together in circumstances which give
rise to a presumption provided for in subsection (1) and such presumption is rebutted in
any court of competent jurisdiction, the woman shall be entitled to apply for maintenance
for herself and for every child of the union on satisfying the court that she and the man
did in fact live together as husband and wife for two years or more, and the court shall
have jurisdiction to make an order or orders for maintenance and, upon application
made therefor either by the woman or the man, to grant such other reliefs, including
custody of children, as it has jurisdiction under this Act to make or grant upon or
subsequent to the making of an order for the dissolution of a marriage or an order for
separation, as the court may think fit, and the provisions of this Act which regulate and
apply to proceedings for, and orders of, maintenance and other reliefs shall, in so far as
they may be applicable, regulate and apply to proceedings for and orders of
maintenance and other reliefs under this section.
 
Unaprove VP living under same roof bila kuhusisha majirani? Umeniita mpuuz ,stakutukana pambana na hill kwanza

Sent using Jamii Forums mobile app
Uliongea kauli hii..
===========================

"Majirani kama waliwstambua kama mke na mume yatosha ila inakuwa presumed tu ili kila upande upate mgao kwenye mali mliyochuma kama IPO na matunzo ya watoto kama wapo.sheria ya ndoa 1971 kifungu 160."
=============================
Kwani ulizungumzia sheria husika au kudhibitisha sheria husika? Wewe umedai sheria inasema kwamba majirani wakidhibitisha kwamba ni mume na mke, inatosha, meaning hata tukiishi kwa wiki 3, au hata tusipoishi chini ya paa moja, au hata tusipoishi kama mume na mke, ilimradi tu majirani wametutambua kama mume na mke hiyo inatosha kwa vigezo wanavyojua wao, wewe umedai sheria ndio ipo hivyo, wakati ni uongo! Sheria hiyo ya 1971 kifungu cha 160 hakisemi hivyo. Wewe ni mpotoshaji, sheria ni hiyo kama nilivyoiweka. Na kuhusu kudhibitisha nimefafsnua tayari post yangu na 7. Au la, kama hubishi, niambie tumekua tunabishana nini mimi na wewe from the beginning...
 
FRANCIS DA DON, Lengo la presumption of marriage liko hasa kwa ajili ya kutetea haki za mwanamke ( ambaye huchukuliwa kama mhanga wa unyanyasaji na unyonywaji na wanaume) za kindoa ambazo zinaweza kupokwa na mwanaume aliyeishi na mwanamke huyo kwa muda huo wa 2 years or 2+ na sasa mwanaume huyo anataka kumuacha bila chochote mwanamke.

Hivyo ikawekwa hiyo presumption of marrige kwenye Sheria yetu ya Ndoa,1971 ili kwa wale wanaume wanaotafuta kufaidika kutokana na jasho la wanawake kwa kuwaweka vimada na wanashiriki shughuli za uzalishaji au maendeleo yao pamoja halafu baadae mwanaume anamruka mwanamke ili afaidike peke yake wapigwe pin.

Hivyo mwanamke akipaza tu sauti mahakamani kuwa nimeishi na huyu mwanamume kwa miaka 2 au zaidi ya 2 ingawa hatujafunga ndoa, tukanunua kiwanja, na tukajenga etc, na sasa ananifukuza kama mbwa bila kunipa chochote, braza umeisha lazima mtagawana naye pasu. Ni simple sana mwanamke kuthibitisha hilo. Elements za Presumption of marriage zimetajwa kwenye kile kifungu wazi kabisa. Kama tu atazionesha, tayari.

Mfano 1. Miaka 2 au zaidi
2. Chini ya dari moja (kuna maendeleo hapa ya sheria. Mahakama zishatoa maamuzi kuwa siyo lazima wawe wanaishi chini ya dari moja kwa kuwa sasa hivi kuna teknolojia (tofauti na miaka ya 1971 sheria ilipotungwa) watu wanachati, wanaongea kwenye simu, wanafanya video call, video chat,etc, etc, hata kama watakuwa wanakutana mara moja moja chini ya one roof(dari moja) bado itasimama kama presumption of marriage) hivyo hata kama wakiwa nchi tofauti au mikoa tofauti bado itasimama.

3. Jamii inayowazunguka iwape heshima au utambuzi(reputation) kama mume na mke. Mfano mnaalikwa kwenye matukio ya hapo kama mume na mke e.g. harusi, mnahudhuria misiba kama mume na mke etc. Hawa ndo watakuwa mashahidi wake pia.

Etc.

Ni mara chache sana mwanaume ata-rase presumption of marriage mahakamani. Kwanza utaona aibu. Kwa nini usioe mpaka unatafuta huruma ya sheria iku-presume?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom