Sheria ya Pasu Kwa Pasu ifutwe Kwa Hoja zifuatazo

Sheria ya Pasu Kwa Pasu ifutwe Kwa Hoja zifuatazo

Watoto ni wa kwetu sote , yeye hanywi hiyo chai , basi yeye kunywa hiyo chai ndio mchango wake. Turudi kwenye asili ya Mungu wetu

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Unalalamika nini wakati sheria za dini ya kiislamu inataka hata mwanaume alipe kodi ya meza kwa mke wake kila anapoondoka.

Mchango wa wanandoa ni zaidi ya hii mifano niliyotoa, ndoa haizingatii mchango wa fedha peka yake au kazi, kuna mambo lukuki yanazingatiwa.

Ndiyo maana leo hii unaweza ukawa na pesa dunia nzima lakini kwenye talaka ikaamuriwa mtoto akae na mama yake ambaye hana pesa kuliko wewe. Halafu wewe ukapewa sharti la kuwatunza wote. Unadhani kwanini mahakama inaamua hivi ???
 
Wewe ndio umeleta hoja za chai na watoto, sasa ulitaka nimjibu nani? Tetea hoja zako au piga kimya..
Kama umeshindwa kuelewa hoja rahisi kama hizo nilizotoa hapo juu hata nikikupa sababu milioni za kwanini bunge na mahakama ziliamua hivi kuhusu sheria ya ndoa huwezi kuelewa.

Hata hivyo siyo lazima uelewa kila kitu, wenye kuelewa washaelewa. Wewe ambaye hujaelewa endelea kupayuka-payuka kama Banshee ameona kifo.....
 
Unalalamika nini wakati sheria za dini ya kiislamu inataka hata mwanaume alipe kodi ya meza kwa mke wake kila anapoondoka.

Mchango wa wanandoa ni zaidi ya hii mifano niliyotoa, ndoa haizingatii mchango wa fedha peka yake au kazi, kuna mambo lukuki yanazingatiwa.

Ndiyo maana leo hii unaweza ukawa na pesa dunia nzima lakini kwenye talaka ikaamuriwa mtoto akae na mama yake ambaye hana pesa kuliko wewe. Halafu wewe ukapewa sharti la kuwatunza wote. Unadhani kwanini mahakama inaamua hivi ???
1.) Kwani hapa si tupo kujaribu kubadilisha hizo tataribu zilizopo? Kwahiyo haijalishi waislam au wakristo sheria zao zinasemaje, bali cha msingi ni kipi ambacho tungependelea sheria ziseme.

2.) Toa mifano hiyo mingine ya tofauti ya ‘Chai’ na ‘watoto’ tujadili.

3.) Suala la pesa na mtoto kukaa na mama yake ni natural kabisa, mtoto ni wa mama, na malezi ya kimahitaji ni ya baba, wala si tatizo wala si hoja.
 
Kama umeshindwa kuelewa hoja rahisi kama hizo nilizotoa hapo juu hata nikikupa sababu milioni za kwanini bunge na mahakama ziliamua hivi kuhusu sheria ya ndoa huwezi kuelewa.

Hata hivyo siyo lazima uelewa kila kitu, wenye kuelewa washaelewa. Wewe ambaye hujaelewa endelea kupayuka-payuka kama Banshee ameona kifo.....
1.) Hatupo hapa kujadili nini au nani aliamua nini huko nyuma, bali tujadili kwa hoja nini kinatakiwa kiwe vipi kwa siku za mbeleni, na ndio hoja iliyopo juu ya mgao wa mali, kwamba uweje na kwanini uwe hivyo, ukaleta hoja za Chai na watoto, umejibiwa una panic.., calm down brother, leta hoja zingine kama unazo...

2.)Usilazimishe watu kukuelewa, hatupo hapa kuelewana, bali kupeana hoja na kuzijibu.., sawa brother.., haya nenda kanywe chai upoe.
 
1.) Kwani hapa si tupo kujaribu kubadilisha hizo tataribu zilizopo? Kwahiyo haijalishi waislam au wakristo sheria zao zinasemaje, bali cha msingi ni kipi ambacho tungependelea sheria ziseme.

2.) Toa mifano hiyo mingine ya tofauti ya ‘Chai’ na ‘watoto’ tujadili.

3.) Suala la pesa na mtoto kukaa na mama yake ni natural kabisa, mtoto ni wa mama, na malezi ya kimahitaji ni ya baba, wala si tatizo wala si hoja.
Viti kama hivi hata mtanzania wa kawaida kule kijijini anavifahamu, sasa nikulezee mimi ni baba yako ???

Unajua kusoma na kuandika, nenda kasome SHERIA YA NDOA YA TANZANIA na kesi za MAHAKAMA KUU kuhusu talaka. Japo nafahamu wewe huwezi kufanya hivyo kwasababu wewe ni MPUMBAVU.
 
Viti kama hivi hata mtanzania wa kawaida kule kijijini anavifahamu, sasa nikulezee mimi ni baba yako ???

Unajia kusoma na kuandika, nenda kasome SHERIA YA NDOA YA TANZANIA na kesi za MAHAKAMA KUU kuhusu talaka. Japo nafahamu wewe huwezi kufanya hivyo kwasababu wewe ni MPUMBAVU WAYAWAYA.
Nenda kasome wewe halafu uje na hoja nyingine tofauti na ya ‘Chai’ na ya ‘watoto’ ambayo tumeshakujibu. Mwanzo ulikuja na hoja, which was good, na umejibwa, sasa unaleta vihoja, which is ridiculous. Hatupo hapa kufuata kilichofanyika au kuamuliwa nyuma, bali tumashauri kupitia mjadala kwamba nini kifanyike na kiamuliwe huko mbeleni, ili tusonge mbele
 
SHERIA YA PASU KWA PASU IFUTWE KWA HOJA ZIFUATAZO:

Anaandika, Robert Heriel

Kwa Dunia ya Haki Sawa hiyo sheria haijakaa vizuri Kabisa, Kwa Dunia hii yenye utapeli, dhulma, ubinafsi na Unyonyaji; sheria hiyo ipo haja ya kuipitia vinginevyo kizazi kijacho kitajikuta katika mazingira magumu sana.
Hiyo sheria haitendi HAKI Kwa namna moja ama nyingine, Kwa ufahamu wangu mdogo sheria zinatungwa ili kulinda Haki Fulani. Sheria inayotungwa kutetea HAKI ya MTU mmoja na kusigina Haki ya mtu mwingine sheria hiyo ni kandamizi.

Leo tujadili dhana au sheria ya pasu Kwa pasu katika kugawana Mali hasa Baada ya kuachana.

"Ooooh! Walichuma Mali pamoja" nini maana ya kuchuma Mali pamoja?
Hata mchume Mali pamoja au mfanye Jambo Kwa pamoja lazima kuna mmoja amefanya ziada, hiyo ipo popote pale katika uzalishaji.
Katika Kanuni za uzalishaji na malipo, anayezalisha zaidi ndiye anastahili kulipwa au kupewa zaidi. Hata kama wazalishaji mlikuwa wengi hiyo ni kanuni ya kiuchumi.

Kusema MKE na Mume ATI Kwa vile walizalisha Mali pamoja basi siku wakitengana wagawane Pasu Kwa Pasu ni uonevu na dhulma kubwa Kwa mmojawapo Kati Yao. Hiyo ni sheria kandamizi. Na ambayo inatakiwa ifanyiwe marekebisho yenye tija.

Sheria au dhana ya pasu Kwa pasu IFUTWE Kwa sababu zifuatazo;

1. Ni ukandamizaji, udhulumaji, na Unyonyaji.
Pasu Kwa Pasu kiaje? Tuache dhulma na ukandamizaji. Kama MKE alikuwa mzalishaji Mkuu apewe zaidi, kama mume alikuwa mzalishaji Mkuu apewe zaidi.
Huko ndiko tunakoenda bila Shaka.
Kama Ndoa inatalaka ni vizuri iwekwe sheria mapema yenye HAKI na sio sheria za upendeleo.
Kila MTU akinunua Mali yoyote anunue Kwa jina lake na aweke kumbukumbu, vielelezo au ushahidi.
Mke umenunua Jiko weka Risiti, umenunua nyumba au kiwanja weka Risiti
Siku mkigawana Mali mtendeane Kwa HAKI.

Sheria ya pasu Kwa pasu imeathiri na itaathiri zaidi kizazi hiki na kijacho kwani ni sheria yenye uonevu mkubwa Kwa moja ya wanandoa.
Mwanzoni MTU Kwa upofu WA mapenzi hataona tatizo, lakini kadiri migogoro ikianza kujitokeza ndipo ataona ameingia katika shimo Baya.

Ndoa iwe na mkataba kabisa wa maandishi unaoelezea makubaliano ya wanandoa kuanzia jinsi watakavyoishi, namna watakavyolea Watoto, Makosa ambayo hayatavumilika, namna watavyogawana Mali endapo wakitengana, Watoto wataishi kwa nani na kiwango cha Huduma cha kila mmoja wapo Kwa Watoto hao, majina ya Watoto yatoke upande gani" Hivyo yaani.

Mfano, Haiwezekani mtoto alelewe na Mama mwanzo mwisho alafu ATI maamuzi ya jina la mtoto yatoke Kwa Baba kisa alimzaa, huo ni UHUNI. Udhulumaji, ukandamizaji.
Mtoto akilelewa na Mama, majina yatoke kwenye Ukoo wa Mama, mfano. Hiyo ndio HAKI.
Kama Baba anataka Haki ya jina lake kuitwa Kwa mtoto basi alee mwanaye.

Uonevu, ukandamizaji, dhulma, Unyonyaji n.k ni mambo yakuangaliwa katika mahusiano ya ndoa.

2. Kuondoa Utegemezi na kuongeza uzalishaji katika Nchi.
Kila MTU akiwa mzalishaji katika familia, ni wazi kila MTU atachapa kazi ili kujihami na kujidhatiti kikamilifu. Ndani ya familia kila MTU atataka awe na mchango na achangie Mali kwani hizo ndizo zitagawanywa kama itatokea kuachana.
Mambo
Mambo ya Mario pamoja na kuvizia Mali za mwenza wako au kuachana Kwa Makusudi ili upate Mali zisizozako hayatakuwepo.

Kila mmoja atapambana, na hiyo ndio itaitwa Haki Sawa Kwa wote,
Sheria za kusema Mwanaume anaowajibu wa kuhudumia familia IFUTWE na isomeke kuwa Wanandoa, yaani Baba na Mama wanayohaki Sawa kuhudumia Familia katika kiwango Sawa.
Au isomeke kuwa, Wanandoa watatimiza majukumu na wajibu wao kulingana na Mkataba na makubaliano Yao waliosaini na kuandikishana Kabla ya Ndoa.

Pasiwe na mkataba wa Generally kama Ile mikataba ya Wakristo, unatakiwa uwe NI mkataba wa maandishi wenye kurasa za kutosha zitakazolinda Haki na Wajibu Wawili hao
Isomeke hivi;
Huu ni mkataba wa Ndoa baina ya Bw. James Dario na Bi. Alice Ndembo.
Mkataba huo upitiwe na wanasheria, usainiwe na wanasheria, kisha kama MTU atafunga ndoa hiyo Kanisani au msikitini au bomani au Mila kule anaenda kuchukua Cheti tuu.

Na sio ati Watu wasiohusika na ndoa yenu Kwa kile kiitwacho sijui Dini, sijui Serikali, au Mapokeo ya utamaduni ati wao ndio wawe na mchango mkubwa katika mkataba wenu.

Mkataba useme kabisa atakayetaka ndoa kuvunjika(atakayevunja mkataba) atawajibika Kwa kiwango gani?
Mfano atakayevunja ndoa Kwa namna yoyote atalipishwa Nusu ya Mali zake. Alafu mkataba ueleze ni mambo gani yatakayovunja ndoa hiyo.

4. Kupunguza hofu na woga Kwa Watu hasa vijana kuingia kwenye Ndoa.
Kuifuta sheria ya ajabu ambayo ni yauonevu, kuwa pasu Kwa pasu, kutachochea Vijana WA kizazi cha leo kuoa zaidi na kuiheshimu Ndoa.
Vijana wengi WA sasa wanaamini ndoa ni Utapeli, ukandamizaji Kwa wanaume, udhulumaji wa Haki zao.
Ninawafahamu baadhi ya Watu ambao hawataki kuoa Kwa sababu ya kuogopa migogoro hasa migogoro ya Mali Baada ya kutengana.

Na upo ushahidi WA kesi nyingi Mahakamani kuhusu migogoro ya kugawana Mali na mirathi.
Kama taifa kuna haja ya kuzipitia hizi Sheria upya ili kulijenga taifa hili.

Haiwezekani Pesa ya Mwanamke iwe ya Mwanamke, ahudumie kwao na wewe pia uhudumie kwao, tena uhudumie familia yako, alafu bado mkiachana atake mgawane Mali, huo ni UHUNI, Utapeli, dhulma kubwa, na ukandamizaji.
Kijana akifikiria hivyo hawezi kuwa na sababu ya kuoa ikiwa Hana uhakika mzuri wa matokeo/hatma yake.

5. Mali itakayogawanywa pasu Kwa pasu iwe Ile iliyonunuliwa na kuchangiwa na kila mmoja pasu Kwa pasu.
Mfano, Mlinunua nyumba Milioni 20, kila mmoja akatoa Milioni 10, basi Mali hiyo ni Hali yenu kugawana Nusu Kwa Nusu.

Masuala ya kusema nilitoa mawazo sijui nilishauri hapo hayapo, kama ushauri ungekuwa na nguvu basi kila familia ingekuwa na nyumba na hayo magari. Kushauri ndio kitu gani bhana!
Kama nyumba imenunuliwa milioni Ishirini, alafu Mume akatoa Milioni 6 alafu MKE akatoa milioni 14 basi kama siku mkiachana Nyumba ikauzwa labda milioni 18. Basi MKE atachukua 74% ya mauzo huku Mume akichukua 26% ya mapato.
Hiyo ndio inaitwa Haki.
Hapo hajaonewa yeyote.

Tuelewe kuwa Mapenzi na upendo haviongozwi na sheria Ila ndoa lazima iongozwe na Sheria, Kanuni, na taratibu.
Hii ni Kwa sababu ndoa ni taasisi, haiongozwi Kwa hisia Bali Akili, na Akili lazima iwekewe sheria, Kanuni, na utaratibu.

Ni Yule Mtibeli

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Andiko lako kwangu Mimi nimeona ni kama mtu ambaye alitaka kushare mawazo yake na matamanio yake

Lakini

Halina uhalisia katika Maisha halisi kabisa,labda Kule Hollywood linaweza likafaa.
 
Ficha upumbavu wako! Kama unataka mabadiliko nenda kafungue kesi ya kikatiba mahakamani kupinga sheria ya ndoa, siyo kuja kulia-lia hapa jukwaani.

Eti, mijadala! Wewe na hiyo akili yako fupi unaifahamu mijadala kweli ? Unaweza kufanya mijadala ya mambo mazito kama haya ? Wewe endelea kuwa shabiki wa siasa za UVCCM huku mitandaoni, mijadala mikubwa kama hii waachie akili kubwa.

Uwe na siku njema..
1.) https://www.jamiiforums.com/threads...llion-moja-kwa-kuanzisha-tra-efd-app.1330951/

2.) https://www.jamiiforums.com/threads/hivi-ni-kwanini-road-license-isilipiwe-kwenye-mafuta.1120896/

3.) https://www.jamiiforums.com/threads...a-zege-hazitumiki-kama-nguzo-za-umeme.986440/

4.) https://www.jamiiforums.com/threads...umba-ya-sh-10-000-ni-akili-au-matope.1541510/

5.) https://www.jamiiforums.com/threads...zifungwe-kwenye-nguzo-za-umeme.1661406/?amp=1

6.) https://www.jamiiforums.com/threads...-nchi-zinazotumia-mifuko-ya-plastiki.1347961/

7.) https://www.jamiiforums.com/threads...-na-vyote-ulipie-kwa-mara-moja.1972467/?amp=1

Wewe endelea kupapaswa makalio hayo.., sisi ni kumwaga hoja tu..., ona kipi hapo hakijatekelezwa
 
Unapenda sana kuzungumzia mambo ya ushoga na makalio wewe jamaa. Ukizingatia na hizi tabia zako za kuwaonea wivu watoto wa kike hapa jukwaani napata sana wasiwasi na wewe.

Haya unaniletea nyuzi zako hapa, unataka nikusifie, nikupende au nije kwenu kutoa mali ?? Mtoto wa kiume hujiamini, unataka mwaume mwenzako nisifie michango yako!

Usipoteze muda wako, siwezi kusoma upumbavu wako maana nishakupuuza kitambo mno. Hivyo wewe endelea kutukana, kuwa chawa na kulia-lia tu, maana huna unaloweza zaidi ya hilo. Mijadala mikubwa waachie akili kubwa.
 
Calm down brother, umeniita mimi mjinga mkubwa, kwamba sina akili ya kujadili mjadala kama huu wa mgawanyo wa mali, hivyo nimekutolea mifano hai kukuinyesha kwamba mimi si mjinga na sishindwi kujadili mijadala kama hii. Sasa leta hoja nyingine tofauti na hiyo ya ‘Chai’ na ‘watoto’ tuendelee. Otherwise piga kimya.
 
Hakuna hiyo sheria ya pasu kwa pasu, ni porojo tu umeandika hapa. Mali inapogawanywa mahakamani kuna vigezo vingi vinazingatiwa.
Umenena vyema! Japo umefanya makosa kuwaambia ukweli. Ungewaacha waendelee kuamini hizi porojo zao.
 
Calm down brother, umeniita mimi mjinga mkubwa, kwamba sina akili ya kujadili mjadala kama huu wa mgawanyo wa mali, hivyo nimekutolea mifano hai kukuinyesha kwamba mimi si mjinga na sishindwi kujadili mijadala kama hii. Sasa leta hoja nyingine tofauti na hiyo ya ‘Chai’ na ‘watoto’ tuendelee. Otherwise piga kimya.
Umeacha kuharisha matusi! Vizuri sana, naona unaanza kujirekebisha. Siku nyingine usirudie kuleta upumbavu wako wa kujibu-jibu hovyo kila mtu hapa jukwaani ukidhani ni mtoto mwenzako au mjinga. Shika sana adabu yako, tena ishike sana!
 
Leta hoja achana na vihoja, hiyo ya Chai na Watoto ushajibiwa, leta nyingine au piga kimya.
 
Leta hoja achana na vihoja, hiyo ya Chai na Watoto ushajibiwa, leta nyingine au piga kimya.
Endelea kukomaa hapa ili kuua noma kwa kujionesha mwerevu. Ila mimi mtu mzima nafahamu fika, kwamba leo umejifunza kitu kipya na siku nyingine utakuwa mtu makini zaidi.

Bwana Yoda ameshawamegea kitu cha msingi kabisa kuhusu Sheria ya ndoa, hivyo kazi kwenu kwenda kuchunguza na kufanya tafiti.

Intellectual Discourse is not a popularity contest. So grow up...

Nakutakia wakati mwema...
 
Kama ulijua hayo huo utetezi wa Chai na Watoto ulikuwa unatetea nini..., issue ya kilichopo kisheria na kinachotekelezwa kwa kile ulichoita ‘falsafa ya sheria ya ndoa’ ni vitu viwili tofauti, hivyo mjadala unalenga kuondoa mazoea ambayo si ya kisheria ya pasu pasu ambayo msingi wake wewe umeita ni ‘falsafsa’, sasa tunajadili ili kudrive mahakama kutoka kwenye kile ulichoita ‘falsafa’ na twende kwenye ‘sheria’ sasa, kama Yoda alivyoeleza ilivyo, simples as that; ila wewe unaruka ruka kama kuku aliyekatwa kichwa, mara huku mara kule, stay put and state your motion ili mjadala uendlee, au piga kimya.
 
Siku mkifika mahakamani ndo utajua mke achuke ngapi. Hiyo ni kazi ya wanasheria, wahasibu na auditors. Mwingine anaweza kupata 55, 40, 30, 20 10 n.k wanawake wote kwenye ndoa hawachangii viwango sawa na hivyo hakuwezi kuwa na kiwango kimoja tu.
Huo mchango thamani yake ni sh ngapi, au tufanye ni asilimia ngapi..mfano imeuzwa mali million 100 mke achukue ngapi hapo?
 
Back
Top Bottom