Sheria ya Pasu Kwa Pasu ifutwe Kwa Hoja zifuatazo

Sheria ya Pasu Kwa Pasu ifutwe Kwa Hoja zifuatazo

Mwanamke anayejitambua hawezi kukaa nyumbani tu hata siku moja bila kuongeza kipato cha familia.
Ndo wanamwita feminist. Uwe unafatilia nyuzi za wanaume humu uone wengi walivyo madepe tupu..

Wanakwambia mwanamke anaefanya kazi anapata ujeuri wa hela so ili akunyenyekee lazima umwachishe kazi. We wasikilize tu mada zao unaona kabisa utindio ni janga kubwa
 
huna hakika na hayo ya Marekani, utapotosha bure...

kasome "community property States" ndo utajua kwamba Marekani zipo sheria kali za pasu kwa pasu... and worse! Mwanamme unaweza kuambiwa utoke mazima kwenye nyumba.

Sheria ya Tanzania inamlinda mwanamme kuliko ya huko Marekani, tatizo mahakama zetu ndio mbovu
Ulaya na marekani wanawake wanachangia kwenye pato la familia.
 
Hivi kwa nini Demi unanipenda alafu hutaki kukubali hilo?
Mie nikimpenda mtu sijivungi namfata live kumwambia, hata hapa ningekwambia tu wala sijivungi...siwezi kuumia nikae kimya, haipo hiyo.😅😅

Wewe nionyeshe hiyo sheria niisome ili nione kama nakubaliana na wewe au la!
 
Ndo wanamwita feminist. Uwe unafatilia nyuzi za wanaume humu uone wengi walivyo madepe tupu..

Wanakwambia mwanamke anaefanya kazi anapata ujeuri wa hela so ili akunyenyekee lazima umwachishe kazi. We wasikilize tu mada zao unaona kabisa utindio ni janga kubwa
Waendelee kutuita tu hivyo, wanawake wasiojitambua ndio wanakubali huo ujinga. Siku mkiachana unaondoka na furniture tu
 
SHERIA YA PASU KWA PASU IFUTWE KWA HOJA ZIFUATAZO:

Anaandika, Robert Heriel

Kwa Dunia ya Haki Sawa hiyo sheria haijakaa vizuri Kabisa, Kwa Dunia hii yenye utapeli, dhulma, ubinafsi na Unyonyaji; sheria hiyo ipo haja ya kuipitia vinginevyo kizazi kijacho kitajikuta katika mazingira magumu sana.
Hiyo sheria haitendi HAKI Kwa namna moja ama nyingine, Kwa ufahamu wangu mdogo sheria zinatungwa ili kulinda Haki Fulani. Sheria inayotungwa kutetea HAKI ya MTU mmoja na kusigina Haki ya mtu mwingine sheria hiyo ni kandamizi.

Leo tujadili dhana au sheria ya pasu Kwa pasu katika kugawana Mali hasa Baada ya kuachana.

"Ooooh! Walichuma Mali pamoja" nini maana ya kuchuma Mali pamoja?
Hata mchume Mali pamoja au mfanye Jambo Kwa pamoja lazima kuna mmoja amefanya ziada, hiyo ipo popote pale katika uzalishaji.
Katika Kanuni za uzalishaji na malipo, anayezalisha zaidi ndiye anastahili kulipwa au kupewa zaidi. Hata kama wazalishaji mlikuwa wengi hiyo ni kanuni ya kiuchumi.

Kusema MKE na Mume ATI Kwa vile walizalisha Mali pamoja basi siku wakitengana wagawane Pasu Kwa Pasu ni uonevu na dhulma kubwa Kwa mmojawapo Kati Yao. Hiyo ni sheria kandamizi. Na ambayo inatakiwa ifanyiwe marekebisho yenye tija.

Sheria au dhana ya pasu Kwa pasu IFUTWE Kwa sababu zifuatazo;

1. Ni ukandamizaji, udhulumaji, na Unyonyaji.
Pasu Kwa Pasu kiaje? Tuache dhulma na ukandamizaji. Kama MKE alikuwa mzalishaji Mkuu apewe zaidi, kama mume alikuwa mzalishaji Mkuu apewe zaidi.
Huko ndiko tunakoenda bila Shaka.
Kama Ndoa inatalaka ni vizuri iwekwe sheria mapema yenye HAKI na sio sheria za upendeleo.
Kila MTU akinunua Mali yoyote anunue Kwa jina lake na aweke kumbukumbu, vielelezo au ushahidi.
Mke umenunua Jiko weka Risiti, umenunua nyumba au kiwanja weka Risiti
Siku mkigawana Mali mtendeane Kwa HAKI.

Sheria ya pasu Kwa pasu imeathiri na itaathiri zaidi kizazi hiki na kijacho kwani ni sheria yenye uonevu mkubwa Kwa moja ya wanandoa.
Mwanzoni MTU Kwa upofu WA mapenzi hataona tatizo, lakini kadiri migogoro ikianza kujitokeza ndipo ataona ameingia katika shimo Baya.

Ndoa iwe na mkataba kabisa wa maandishi unaoelezea makubaliano ya wanandoa kuanzia jinsi watakavyoishi, namna watakavyolea Watoto, Makosa ambayo hayatavumilika, namna watavyogawana Mali endapo wakitengana, Watoto wataishi kwa nani na kiwango cha Huduma cha kila mmoja wapo Kwa Watoto hao, majina ya Watoto yatoke upande gani" Hivyo yaani.

Mfano, Haiwezekani mtoto alelewe na Mama mwanzo mwisho alafu ATI maamuzi ya jina la mtoto yatoke Kwa Baba kisa alimzaa, huo ni UHUNI. Udhulumaji, ukandamizaji.
Mtoto akilelewa na Mama, majina yatoke kwenye Ukoo wa Mama, mfano. Hiyo ndio HAKI.
Kama Baba anataka Haki ya jina lake kuitwa Kwa mtoto basi alee mwanaye.

Uonevu, ukandamizaji, dhulma, Unyonyaji n.k ni mambo yakuangaliwa katika mahusiano ya ndoa.

2. Kuondoa Utegemezi na kuongeza uzalishaji katika Nchi.
Kila MTU akiwa mzalishaji katika familia, ni wazi kila MTU atachapa kazi ili kujihami na kujidhatiti kikamilifu. Ndani ya familia kila MTU atataka awe na mchango na achangie Mali kwani hizo ndizo zitagawanywa kama itatokea kuachana.
Mambo
Mambo ya Mario pamoja na kuvizia Mali za mwenza wako au kuachana Kwa Makusudi ili upate Mali zisizozako hayatakuwepo.

Kila mmoja atapambana, na hiyo ndio itaitwa Haki Sawa Kwa wote,
Sheria za kusema Mwanaume anaowajibu wa kuhudumia familia IFUTWE na isomeke kuwa Wanandoa, yaani Baba na Mama wanayohaki Sawa kuhudumia Familia katika kiwango Sawa.
Au isomeke kuwa, Wanandoa watatimiza majukumu na wajibu wao kulingana na Mkataba na makubaliano Yao waliosaini na kuandikishana Kabla ya Ndoa.

Pasiwe na mkataba wa Generally kama Ile mikataba ya Wakristo, unatakiwa uwe NI mkataba wa maandishi wenye kurasa za kutosha zitakazolinda Haki na Wajibu Wawili hao
Isomeke hivi;
Huu ni mkataba wa Ndoa baina ya Bw. James Dario na Bi. Alice Ndembo.
Mkataba huo upitiwe na wanasheria, usainiwe na wanasheria, kisha kama MTU atafunga ndoa hiyo Kanisani au msikitini au bomani au Mila kule anaenda kuchukua Cheti tuu.

Na sio ati Watu wasiohusika na ndoa yenu Kwa kile kiitwacho sijui Dini, sijui Serikali, au Mapokeo ya utamaduni ati wao ndio wawe na mchango mkubwa katika mkataba wenu.

Mkataba useme kabisa atakayetaka ndoa kuvunjika(atakayevunja mkataba) atawajibika Kwa kiwango gani?
Mfano atakayevunja ndoa Kwa namna yoyote atalipishwa Nusu ya Mali zake. Alafu mkataba ueleze ni mambo gani yatakayovunja ndoa hiyo.

4. Kupunguza hofu na woga Kwa Watu hasa vijana kuingia kwenye Ndoa.
Kuifuta sheria ya ajabu ambayo ni yauonevu, kuwa pasu Kwa pasu, kutachochea Vijana WA kizazi cha leo kuoa zaidi na kuiheshimu Ndoa.
Vijana wengi WA sasa wanaamini ndoa ni Utapeli, ukandamizaji Kwa wanaume, udhulumaji wa Haki zao.
Ninawafahamu baadhi ya Watu ambao hawataki kuoa Kwa sababu ya kuogopa migogoro hasa migogoro ya Mali Baada ya kutengana.

Na upo ushahidi WA kesi nyingi Mahakamani kuhusu migogoro ya kugawana Mali na mirathi.
Kama taifa kuna haja ya kuzipitia hizi Sheria upya ili kulijenga taifa hili.

Haiwezekani Pesa ya Mwanamke iwe ya Mwanamke, ahudumie kwao na wewe pia uhudumie kwao, tena uhudumie familia yako, alafu bado mkiachana atake mgawane Mali, huo ni UHUNI, Utapeli, dhulma kubwa, na ukandamizaji.
Kijana akifikiria hivyo hawezi kuwa na sababu ya kuoa ikiwa Hana uhakika mzuri wa matokeo/hatma yake.

5. Mali itakayogawanywa pasu Kwa pasu iwe Ile iliyonunuliwa na kuchangiwa na kila mmoja pasu Kwa pasu.
Mfano, Mlinunua nyumba Milioni 20, kila mmoja akatoa Milioni 10, basi Mali hiyo ni Hali yenu kugawana Nusu Kwa Nusu.

Masuala ya kusema nilitoa mawazo sijui nilishauri hapo hayapo, kama ushauri ungekuwa na nguvu basi kila familia ingekuwa na nyumba na hayo magari. Kushauri ndio kitu gani bhana!
Kama nyumba imenunuliwa milioni Ishirini, alafu Mume akatoa Milioni 6 alafu MKE akatoa milioni 14 basi kama siku mkiachana Nyumba ikauzwa labda milioni 18. Basi MKE atachukua 74% ya mauzo huku Mume akichukua 26% ya mapato.
Hiyo ndio inaitwa Haki.
Hapo hajaonewa yeyote.

Tuelewe kuwa Mapenzi na upendo haviongozwi na sheria Ila ndoa lazima iongozwe na Sheria, Kanuni, na taratibu.
Hii ni Kwa sababu ndoa ni taasisi, haiongozwi Kwa hisia Bali Akili, na Akili lazima iwekewe sheria, Kanuni, na utaratibu.

Ni Yule Mtibeli

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
mkuu unakurupukaga sana, kwani kuna sheria ya pasu kwa pasu?
ni namba ngapi
 
Mie nikimpenda mtu sijivungi namfata live kumwambia, hata hapa ningekwambia tu wala sijivungi...siwezi kuumia nikae kimya, haipo hiyo.😅😅

Wewe nionyeshe hiyo sheria niisome ili nione kama nakubaliana na wewe au la!

😀😀😀

Na Mimi sitaki uumie ndio maana nimekurahisishia kazi.
Wanawake kama ninyi mnaopenda harakari Sisi kina Taikon ndio Dawa yenu.
Hao wengine mnawaonea tuu😂😂

Hakuna sheria ya hivyo, hapo nimeitaja sheria kama kiwakilishi cha dhana iliyopo ndani ya jamii
 
Kumbe umejiropokea, haya kwaheri. Nimekosa cha kuchangia
 
Waendelee kutuita tu hivyo, wanawake wasiojitambua ndio wanakubali huo ujinga. Siku mkiachana unaondoka na furniture tu
Si bora furniture. Wanaondokaga na vijora tu. Mimi nimekataa huo ujinga. Kwanza unanioa unanikuta nna viwanja, kwako siji kizembe, sikai kizembe. Kila kitu naandikisha mwanangu. We vya kwako peleka unakojua ila sijaja hapa kusubiri tugawane mali. Ntatafuta niachie wanangu. Mwanaume anatafuta anamjengea hawara. Nani kichaa hapo.

Wanaume Wengi wanatabia ya kuzaa kama kumbikumbi huko nje, na anaweza tu akaamka akajiskia kwenda kumuoa mwajuma, wewe huku ulisshajiwekeza mzima mzima kwake utakuja kulia.

Wanawake jipambanieni, tafutieni watoto wenu maisha, mwanaume anaweza asiwe na uchungu na mtoto, atakutelekeza akaoe mwanamke mwengine unabaki na wanao mweupee huna mia
 
😀😀😀
Oooh!
Bado unasafari ndefu kujua na kung'amua kile kilichoandikwa na ujumbe uliopo
mimi nina ushahidi na kesi ilyoamriwa mwanamke apewe 30% na mwanaume 70% ya thamani ya nyumba, ila huyo demu alijua ni pasupasu. aliangua kilio mahakamani.
sikutegemea uwe na uelewa sawa na huyo demu
 
Lakini mali inabaki ya mmiliki. Anamhusisha tu kama anataka kuuza etc.
HUWEZI kusema hili shati ni langu kama huruhusiwi kulikata mikono bila idhini ya mjombaako! Shati ni lako kama unaweza kulichana ddkio bila kuomba idhini. Simplest logic there is.

Kiwanja ambacho huwezi kukopea mkopo ufanye mambo mengine au kuuza uhame uswahilini au kugawia mtoto wako anaelala kwa shemeji yake, mpaka kwanza upate idhini, hiyo nyumba sio yako!
 
Mwanamke anayejitambua hawezi kukaa nyumbani tu hata siku moja bila kuongeza kipato cha familia.
Hapo unakosea. Wengine hawaoi wanawake kwa lengo la kusaidiana maisha. Na ktk imani za watu kuoa ni ibada na wanawatumikia wake zao kwa Kila hali hata km wake hao wana kazi tena za heshima.

Tusipende kulazimisha matamanio au malengo ya mmoja yawe ya wote. Kwa wale wanao abudu (Waislam na Wakristu) hoja ya mwanamke kuwa na kazi/kutokuwa na kazi wanaijua vizuri. Kwa Wakristu kipengele Cha kusaidiana hakikumaanisha wote mkafanye kazi/muwe wafanyakazi/muwe na vipato. Kwa Waislam hii ndio iko wazi kabisa, hata mkeo akiwa Rais wa nchi wewe ni mpiga debe una LAZIMIKA kumhudumia hadi nguo za ndani.

Mwisho, hao unao waita wajinga ndio wanaishi kwa amani na waume zao kuliko hao unaoona werevu. Wanaume mnataka wanawake wawe na kazi ili wawasaidie majukumu. Kumbe ndio maana ndoa za sasa ni kimbembe. Sikatai wasiwe na kazi, la hasha, wawe na kazi kwa manufaa yao binafsi. Wewe mume ubaki mume Yani mtafutaji na mhudumiaji wa familia. Suala la kulazimisha kujua mshahara wa mkeo/kukaa na ATM card ya mkeo au kumlazimisha kuweka mezani mshahara wake ili uufanyie matumizi km wako ni upuuzi na unyanyasaji na ni dalili za kuyakwepa majukumu yako km mume. Kumbe ndio maana wanawake wengi Wana chepuka sababu hawatunzwi na waume zao kisa kila mtu ana kazi au kipato!!

Vijana wa kiume tambueni kazi/ nafasi ya mwanamke ktk familia kabla ya kuoa. Mwanamke haolewi kwa lengo lakuja kukusaidia maisha. Na wala usioe kwa lengo hilo, na km utaoa kwa lengo hilo jua ipo siku utajuta. Tafuteni pesa acha kuwategemea wake zenu kwani hayo sio makusudio ya Mungu kumuumba mwanamke.
 
Kwa taarifa ya zipo ndoa nyingi zenye matatizo ambao wake zao ni wamama wa nyumbani. Na kuna ndoa ambazo wote wanafanya kazi na ziko stable kabisa. Unayoongelea yamepitwa na wakati.
 
HUWEZI kusema hili shati ni langu kama huruhusiwi kulikata mikono bila idhini ya mjombaako! Shati ni lako kama unaweza kulichana ddkio bila kuomba idhini. Simplest logic there is.

Kiwanja ambacho huwezi kukopea mkopo ufanye mambo mengine au kuuza uhame uswahilini au kugawia mtoto wako anaelala kwa shemeji yake, mpaka kwanza upate idhini, hiyo nyumba sio yako!
Ni yako, na siku mkiachana inabaki kuwa yako. Nina experience na hilo.
 
Unalalamika nini wakati sheria za dini ya kiislamu inataka hata mwanaume alipe kodi ya meza kwa mke wake kila anapoondoka.

Mchango wa wanandoa ni zaidi ya hii mifano niliyotoa, ndoa haizingatii mchango wa fedha peka yake au kazi, kuna mambo lukuki yanazingatiwa.

Ndiyo maana leo hii unaweza ukawa na pesa dunia nzima lakini kwenye talaka ikaamuriwa mtoto akae na mama yake ambaye hana pesa kuliko wewe. Halafu wewe ukapewa sharti la kuwatunza wote. Unadhani kwanini mahakama inaamua hivi ???
Kuwatunza wote au kumtunza mtoto? Toa mfano hai kwa hapo. Uache uongo... kuwatunza wote my foot?
 
Umeacha kuharisha matusi! Vizuri sana, naona unaanza kujirekebisha. Siku nyingine usirudie kuleta upumbavu wako wa kujibu-jibu hovyo kila mtu hapa jukwaani ukidhani ni mtoto mwenzako au mjinga. Shika sana adabu yako, tena ishike sana!
Kama wewe ni baba nafikiri wanao wana hasara sana. Hustahili kuheshimiwa kwa sababu kwa majibu yako kwenye uzi huu ni kuwa HUJIHESHIMU.
 
Back
Top Bottom