Sheria ya Pasu Kwa Pasu ifutwe Kwa Hoja zifuatazo

Sheria ya Pasu Kwa Pasu ifutwe Kwa Hoja zifuatazo

Kama ni nyumba mnayoishi wanandoa huwezi kuigusa bila idhini ya mkeo kwa kuuza, ku rentisha, kugawa, kuchukulia mkopo, kurithisha, wala kuandika eti ukifa uzikwe mlango wa mbele.

CAP 29
Part IV
Sect 59
Sub-sect 1

Where any estate or interest in the matrimonial home is owned by the husband or the wife, he or she shall not, while the marriage subsists and without the consent of the other spouse, alienate it by way of sale, gift, lease, mortgage or otherwise
Kwani yeye ana nyaraka zipi za kuonyesha ni nyumba yake? Kwanza nyumba siandikishi jina langu Bali la ndugu yangu Ili baadae niseme sikujenga Mimi Bali alijenga Fulani then tulivyoachana ndio ametaka nyumba yake hata kama tumeishi humo maana pesa zilikuwa zake na mwanamke hajawahi changia chochote.
 
Hawawezi kugawa 50/50,hili hata Marekani halipo,
huna hakika na hayo ya Marekani, utapotosha bure...

kasome "community property States" ndo utajua kwamba Marekani zipo sheria kali za pasu kwa pasu... and worse! Mwanamme unaweza kuambiwa utoke mazima kwenye nyumba.

Sheria ya Tanzania inamlinda mwanamme kuliko ya huko Marekani, tatizo mahakama zetu ndio mbovu
 
huna hakika na hayo ya Marekani, utapotosha bure...

kasome "community property States" ndo utajua kwamba Marekani zipo sheria kali za pasu kwa pasu... and worse! Mwanamme unaweza kuambiwa utoke mazima kwenye nyumba.

Sheria ya Tanzania inamlinda mwanamme kuliko ya huko Marekani, tatizo mahakama zetu ndio mbovu
Community Property Law is not autonomous as you hereby feign savvy. Community Property Law is a presumption, presupposition, or a legal assumption and a general rule, that all properties acquired by spouses during subsistence of their marriage are deemed to be jointly owned. Be it as it may, presumptions can be rebutted and all general rules have exceptions. Even in radical state like California, before issuance of divorce decree courts will make considerations as to whether properties owned by couples were ex ante subject to community property law.

Mahakama haziamui-amui tu kama genge la wanywa kawaha kama ninyi mnavyokomaa kutulazimisha hapa. Hili liko hata kwenye hayo majimbo tisa ya Marekani. Exceptions are, properties under the corpus of prenuptial agreement, properties acquired before marriage, properties like gifts, inheritance, trust-benefits/funds are not subject to Community Property Law. Also, properties acquired through resources and efforts of a single spouse, and properties acquired by spouses individually when they are living apart. For, example a spouse is Military veteran whose most part of his life was spent in military barracks of backwater hell-holes like Afghanistan.

Mahakama haiwezi kugawa tu bila kuwasikiliza wahusika na kufanya upembuzi yakinifu. Nakubali kuna sehemu huko Marekani kunakuwa na shida kubwa, ila mara nyingi matukio haya yanakuwa ya watu maarufu na hutangazwa mno kwenye vyombo vya habari. Ila kiukweli ni matukio ya sehemu ndogo mno ya wanandoa wanaoachana (They are just sporadic and isolated incidents), kwasababu hii sheria iko kwenye majimbo tisa tu. Sehemu nyingine za Marekani inatumika Common Law ya Uingereza.

Halafu acha kujifanya mjuaji, sheria ya Tanzania inamlinda zaidi MWANAMKE kuliko MWANAMUME. Ungekuwa unayafahamu haya fika kama unavyojitanabaisha hapa usingediriki kuandika huu ujinga hata kidogo. Consider these good examples as food for thought, the corpus of marriage law in Tanzania mandates the following:

  • A husband to dutifully maintain a wife through entirety of their marriage, and not vice-versa.
  • A wife can pledge on her husband properties if not properly maintained.
  • Division of properties even when there's a presumption of marriage (Cohabitation with no marriage)
  • Child custody laws explicitly tilts in favour of women than men.

I could give you a mountain of examples, but I face two predicaments, time and your stubbornness.
 
sheria gani iko kwenye majimbo tisa tu ?
Community Property Law is only applicable within 9 American states. If you had bothered reading a little, all these facts wouldn't have been within a domain of your witts.

But like I said earlier, I could have given you a mountain of evidence but you wouldn't be able to comprehend nothing because you're stubborn like a Honey-Badger.
 
Community Property Law is only applicable within 9 American states.
anhaaa, kwa hiyo kumbe ipo huko Marekani sheria ya Community Property law ya pasu kwa pasu kama nilivyosema

nilitaka urudie maneno yangu uyaandike mwenyewe halafu umeze maneno yako potofu

siku nyingine never ever assume kwamba unaweza kuandika kitu kwenye jamvi la maelfu ya watu kutoka kila pembe ya dunia wenye upeo na visomo vya wa kila ngazi halafu ukadhani nobody would bother to check the facts of your cockamamie claims

pasu kwa pasu ipo all over the world
 
SHERIA YA PASU KWA PASU IFUTWE KWA HOJA ZIFUATAZO:

Anaandika, Robert Heriel

Kwa Dunia ya Haki Sawa hiyo sheria haijakaa vizuri Kabisa, Kwa Dunia hii yenye utapeli, dhulma, ubinafsi na Unyonyaji; sheria hiyo ipo haja ya kuipitia vinginevyo kizazi kijacho kitajikuta katika mazingira magumu sana.
Hiyo sheria haitendi HAKI Kwa namna moja ama nyingine, Kwa ufahamu wangu mdogo sheria zinatungwa ili kulinda Haki Fulani. Sheria inayotungwa kutetea HAKI ya MTU mmoja na kusigina Haki ya mtu mwingine sheria hiyo ni kandamizi.

Leo tujadili dhana au sheria ya pasu Kwa pasu katika kugawana Mali hasa Baada ya kuachana.

"Ooooh! Walichuma Mali pamoja" nini maana ya kuchuma Mali pamoja?
Hata mchume Mali pamoja au mfanye Jambo Kwa pamoja lazima kuna mmoja amefanya ziada, hiyo ipo popote pale katika uzalishaji.
Katika Kanuni za uzalishaji na malipo, anayezalisha zaidi ndiye anastahili kulipwa au kupewa zaidi. Hata kama wazalishaji mlikuwa wengi hiyo ni kanuni ya kiuchumi.

Kusema MKE na Mume ATI Kwa vile walizalisha Mali pamoja basi siku wakitengana wagawane Pasu Kwa Pasu ni uonevu na dhulma kubwa Kwa mmojawapo Kati Yao. Hiyo ni sheria kandamizi. Na ambayo inatakiwa ifanyiwe marekebisho yenye tija.

Sheria au dhana ya pasu Kwa pasu IFUTWE Kwa sababu zifuatazo;

1. Ni ukandamizaji, udhulumaji, na Unyonyaji.
Pasu Kwa Pasu kiaje? Tuache dhulma na ukandamizaji. Kama MKE alikuwa mzalishaji Mkuu apewe zaidi, kama mume alikuwa mzalishaji Mkuu apewe zaidi.
Huko ndiko tunakoenda bila Shaka.
Kama Ndoa inatalaka ni vizuri iwekwe sheria mapema yenye HAKI na sio sheria za upendeleo.
Kila MTU akinunua Mali yoyote anunue Kwa jina lake na aweke kumbukumbu, vielelezo au ushahidi.
Mke umenunua Jiko weka Risiti, umenunua nyumba au kiwanja weka Risiti
Siku mkigawana Mali mtendeane Kwa HAKI.

Sheria ya pasu Kwa pasu imeathiri na itaathiri zaidi kizazi hiki na kijacho kwani ni sheria yenye uonevu mkubwa Kwa moja ya wanandoa.
Mwanzoni MTU Kwa upofu WA mapenzi hataona tatizo, lakini kadiri migogoro ikianza kujitokeza ndipo ataona ameingia katika shimo Baya.

Ndoa iwe na mkataba kabisa wa maandishi unaoelezea makubaliano ya wanandoa kuanzia jinsi watakavyoishi, namna watakavyolea Watoto, Makosa ambayo hayatavumilika, namna watavyogawana Mali endapo wakitengana, Watoto wataishi kwa nani na kiwango cha Huduma cha kila mmoja wapo Kwa Watoto hao, majina ya Watoto yatoke upande gani" Hivyo yaani.

Mfano, Haiwezekani mtoto alelewe na Mama mwanzo mwisho alafu ATI maamuzi ya jina la mtoto yatoke Kwa Baba kisa alimzaa, huo ni UHUNI. Udhulumaji, ukandamizaji.
Mtoto akilelewa na Mama, majina yatoke kwenye Ukoo wa Mama, mfano. Hiyo ndio HAKI.
Kama Baba anataka Haki ya jina lake kuitwa Kwa mtoto basi alee mwanaye.

Uonevu, ukandamizaji, dhulma, Unyonyaji n.k ni mambo yakuangaliwa katika mahusiano ya ndoa.

2. Kuondoa Utegemezi na kuongeza uzalishaji katika Nchi.
Kila MTU akiwa mzalishaji katika familia, ni wazi kila MTU atachapa kazi ili kujihami na kujidhatiti kikamilifu. Ndani ya familia kila MTU atataka awe na mchango na achangie Mali kwani hizo ndizo zitagawanywa kama itatokea kuachana.
Mambo
Mambo ya Mario pamoja na kuvizia Mali za mwenza wako au kuachana Kwa Makusudi ili upate Mali zisizozako hayatakuwepo.

Kila mmoja atapambana, na hiyo ndio itaitwa Haki Sawa Kwa wote,
Sheria za kusema Mwanaume anaowajibu wa kuhudumia familia IFUTWE na isomeke kuwa Wanandoa, yaani Baba na Mama wanayohaki Sawa kuhudumia Familia katika kiwango Sawa.
Au isomeke kuwa, Wanandoa watatimiza majukumu na wajibu wao kulingana na Mkataba na makubaliano Yao waliosaini na kuandikishana Kabla ya Ndoa.

Pasiwe na mkataba wa Generally kama Ile mikataba ya Wakristo, unatakiwa uwe NI mkataba wa maandishi wenye kurasa za kutosha zitakazolinda Haki na Wajibu Wawili hao
Isomeke hivi;
Huu ni mkataba wa Ndoa baina ya Bw. James Dario na Bi. Alice Ndembo.
Mkataba huo upitiwe na wanasheria, usainiwe na wanasheria, kisha kama MTU atafunga ndoa hiyo Kanisani au msikitini au bomani au Mila kule anaenda kuchukua Cheti tuu.

Na sio ati Watu wasiohusika na ndoa yenu Kwa kile kiitwacho sijui Dini, sijui Serikali, au Mapokeo ya utamaduni ati wao ndio wawe na mchango mkubwa katika mkataba wenu.

Mkataba useme kabisa atakayetaka ndoa kuvunjika(atakayevunja mkataba) atawajibika Kwa kiwango gani?
Mfano atakayevunja ndoa Kwa namna yoyote atalipishwa Nusu ya Mali zake. Alafu mkataba ueleze ni mambo gani yatakayovunja ndoa hiyo.

4. Kupunguza hofu na woga Kwa Watu hasa vijana kuingia kwenye Ndoa.
Kuifuta sheria ya ajabu ambayo ni yauonevu, kuwa pasu Kwa pasu, kutachochea Vijana WA kizazi cha leo kuoa zaidi na kuiheshimu Ndoa.
Vijana wengi WA sasa wanaamini ndoa ni Utapeli, ukandamizaji Kwa wanaume, udhulumaji wa Haki zao.
Ninawafahamu baadhi ya Watu ambao hawataki kuoa Kwa sababu ya kuogopa migogoro hasa migogoro ya Mali Baada ya kutengana.

Na upo ushahidi WA kesi nyingi Mahakamani kuhusu migogoro ya kugawana Mali na mirathi.
Kama taifa kuna haja ya kuzipitia hizi Sheria upya ili kulijenga taifa hili.

Haiwezekani Pesa ya Mwanamke iwe ya Mwanamke, ahudumie kwao na wewe pia uhudumie kwao, tena uhudumie familia yako, alafu bado mkiachana atake mgawane Mali, huo ni UHUNI, Utapeli, dhulma kubwa, na ukandamizaji.
Kijana akifikiria hivyo hawezi kuwa na sababu ya kuoa ikiwa Hana uhakika mzuri wa matokeo/hatma yake.

5. Mali itakayogawanywa pasu Kwa pasu iwe Ile iliyonunuliwa na kuchangiwa na kila mmoja pasu Kwa pasu.
Mfano, Mlinunua nyumba Milioni 20, kila mmoja akatoa Milioni 10, basi Mali hiyo ni Hali yenu kugawana Nusu Kwa Nusu.

Masuala ya kusema nilitoa mawazo sijui nilishauri hapo hayapo, kama ushauri ungekuwa na nguvu basi kila familia ingekuwa na nyumba na hayo magari. Kushauri ndio kitu gani bhana!
Kama nyumba imenunuliwa milioni Ishirini, alafu Mume akatoa Milioni 6 alafu MKE akatoa milioni 14 basi kama siku mkiachana Nyumba ikauzwa labda milioni 18. Basi MKE atachukua 74% ya mauzo huku Mume akichukua 26% ya mapato.
Hiyo ndio inaitwa Haki.
Hapo hajaonewa yeyote.

Tuelewe kuwa Mapenzi na upendo haviongozwi na sheria Ila ndoa lazima iongozwe na Sheria, Kanuni, na taratibu.
Hii ni Kwa sababu ndoa ni taasisi, haiongozwi Kwa hisia Bali Akili, na Akili lazima iwekewe sheria, Kanuni, na utaratibu.

Ni Yule Mtibeli

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Mwanamke inabidi apate zaidi ya nusu endapo mna watoto. Wanaume huwa si watunzaji wa watoto labda wachache sana
 
Kijana kataa ndoa.

Ndoa ni ubadhilifu.

Yeye aweke miguu juu na remote.

Mwisho wa siku ghorofa langu Atake tugawane.

Akwende
 
anhaaa, kwa hiyo kumbe ipo huko Marekani sheria ya Community Property law ya pasu kwa pasu kama nilivyosema

nilitaka urudie maneno yangu uyaandike mwenyewe halafu umeze maneno yako potofu

siku nyingine never ever assume kwamba unaweza kuandika kitu kwenye jamvi la maelfu ya watu kutoka kila pembe ya dunia wenye upeo na visomo vya wa kila ngazi halafu ukadhani nobody would bother to check the facts of your cockamamie claims

pasu kwa pasu ipo all over the world
Community Property Law is a presumption that can be rebutted. If you can't comprehend a meaning of a phrase "presumption of law", then not even the angelic host of heaven can ever make you understand.
 
Nimeisoma kwa kuruka rukia (sijasoma yote) lakini Kuna sehemu hapo nimeona umeandika eti "Mfano, Haiwezekani mtoto alelewe na Mama mwanzo mwisho alafu ATI maamuzi ya jina la mtoto yatoke Kwa Baba kisa alimzaa, huo ni UHUNI. Udhulumaji, ukandamizaji."

Niliposoma hicho kipande magoti yakalegea kabisa
 
Wala hakuna kitu kama hicho kwangu
Hahahahaa unaonekana unamisimamo sanaa safiii kabisaaa
Mabinti wengne hawataki kazi/kujishughulisha wanatumia mpk nguvu za giza kuingia kwenye maisha ya vijana waliosimama kiuchumi kwa kigezo kwamba watapata mali
Hii sheria iwe na mkazo kwelikweli italeta uwajibikaji ukiamua kulala tu nyumban unachart mkiachana utaondoka na simuyako
 
Mwanamke sehemu yeyote akienda hata kama yeye ndiyo mwenye makosa ataonewa huruma si dawati la jinsia ,si mahakamani ,si bakwata si kwa paroko.
Na wana ile tabia yao ya kujiliza liza.., itabidi na wanaume nao waanze kulia lia kama watoto ili kupata huruma, maana mahakama zinaendeshwa kwa hisia badala ya ushahidi misingi ya sheria
 
Mkuu, kwenye sheria za ndoa nchini Tanzania hakuna 50/50 ila sheria inamlinda mwanamke apewe gawio la mchango wake kwenye ndoa hata kama hakuwa na kazi. Hii ndiyo falsafa ya sheria ya ndoa.

Kama mwanaume unaamka asubuhi, unakuta nguo na chai mezani vimewekwa na unaacha watoto wadogo unarudi unakuta wako salama huo ni mchango wa mwanamke ambao mahakama ni lazima ziuzingatie kwenye mgawanyo wa mali.
Haya mambo yenu ya sijui mchango wa mwanamke kwenye ndoa na sheria izingatiwe ni kwa ndoa zenu za kikiristu, kwenye uislam hamna kitu kama hicho.
 
Mkuu, kwenye sheria za ndoa nchini Tanzania hakuna 50/50 ila sheria inamlinda mwanamke apewe gawio la mchango wake kwenye ndoa hata kama hakuwa na kazi. Hii ndiyo falsafa ya sheria ya ndoa.

Kama mwanaume unaamka asubuhi, unakuta nguo na chai mezani vimewekwa na unaacha watoto wadogo unarudi unakuta wako salama huo ni mchango wa mwanamke ambao mahakama ni lazima ziuzingatie kwenye mgawanyo wa mali.
Huo wajb haufanyw na wote kama unavyo generalize.....mana kuna ilivyo na inavyotakiwa kuwa.....
 
Huo wajb haufanyw na wote kama unavyo generalize.....mana kuna ilivyo na inavyotakiwa kuwa.....
Tafadhali usinipachikie maneno, hakuna sehemu yoyote ile nimesema huu wajibu unatimizwa na wote. Nilichosema ni kwamba mahakama itapima na kuzingatia utekelezaji wa majukumu ya nyumbani kama moja ya kigezo.

Ugumu uko wapi ???
 
Haya mambo yenu ya sijui mchango wa mwanamke kwenye ndoa na sheria izingatiwe ni kwa ndoa zenu za kikiristu, kwenye uislam hamna kitu kama hicho.
Hayo ya waislamu na wakristo baki nayo mwenyewe kwasababu hayanihusu. Binafsi kinachonihusu hapa ni sheria za nchi na falsafa yake tu.
 
Watanzania wawe macho na 'Matapeli'

Maadili na tamaduni ngeni mara nyingi, ndizo zenye kuleta tafrani ndani ya Jamii haswa pale Unapo shauriwa kwa hila! Na unapokubali bila kufanya udadisi wa kina.

Ndoa iwe na mkataba kabisa wa maandishi unaoelezea makubaliano ya wanandoa kuanzia jinsi watakavyoishi, namna watakavyolea Watoto, Makosa ambayo hayatavumilika,
???
Sheria za kusema Mwanaume anaowajibu wa kuhudumia familia IFUTWE na isomeke kuwa Wanandoa, yaani Baba na Mama wanayohaki Sawa kuhudumia Familia
??? hiyo Sheria ipo wapi?
Watu wasiohusika na ndoa yenu Kwa kile kiitwacho sijui Dini, sijui Serikali, au Mapokeo ya utamaduni ati wao ndio wawe na mchango mkubwa katika mkataba wenu.
Unachokifanya....(unajihusisha).ndii hayo unayokataza, kwanini?
Na upo ushahidi WA kesi nyingi Mahakamani kuhusu migogoro ya kugawana Mali na mirathi.
Kama taifa kuna haja ya kuzipitia hizi Sheria upya ili kulijenga taifa hili.
Tutajie moja, ipo wapi, Mahakama gani Tanzania, hususani pale hiyo "pasu pasu" ilipotajwa na kutumika kuendesha kesi hizo
Mapenzi na upendo haviongozwi na sheria Ila ndoa lazima iongozwe na Sheria, Kanuni..
Aiseee


Cyber crimes act inasemaje kuhusu vitu kama hivi....yaani Watu au Taasisi kujiamulia kutunga "Sheria" inayowafaa Jamii na kuibandika mtandaoni kama ndio sheria yenyewe.
Aisee
 
Hayo ya waislamu na wakristo baki nayo mwenyewe kwasababu hayanihusu. Binafsi kinachonihusu hapa ni sheria za nchi na falsafa yake tu.
Unapiga maktaimu hapo kijana, issue ya Ndoa ni tofauti na hayo unayosimamia, acha kabisa!.
 
Back
Top Bottom