Sheria ya Pasu Kwa Pasu ifutwe Kwa Hoja zifuatazo

Mwanamke anayejitambua hawezi kukaa nyumbani tu hata siku moja bila kuongeza kipato cha familia.
Ndo wanamwita feminist. Uwe unafatilia nyuzi za wanaume humu uone wengi walivyo madepe tupu..

Wanakwambia mwanamke anaefanya kazi anapata ujeuri wa hela so ili akunyenyekee lazima umwachishe kazi. We wasikilize tu mada zao unaona kabisa utindio ni janga kubwa
 
Ulaya na marekani wanawake wanachangia kwenye pato la familia.
 
Hivi kwa nini Demi unanipenda alafu hutaki kukubali hilo?
Mie nikimpenda mtu sijivungi namfata live kumwambia, hata hapa ningekwambia tu wala sijivungi...siwezi kuumia nikae kimya, haipo hiyo.πŸ˜…πŸ˜…

Wewe nionyeshe hiyo sheria niisome ili nione kama nakubaliana na wewe au la!
 
Waendelee kutuita tu hivyo, wanawake wasiojitambua ndio wanakubali huo ujinga. Siku mkiachana unaondoka na furniture tu
 
mkuu unakurupukaga sana, kwani kuna sheria ya pasu kwa pasu?
ni namba ngapi
 
Mie nikimpenda mtu sijivungi namfata live kumwambia, hata hapa ningekwambia tu wala sijivungi...siwezi kuumia nikae kimya, haipo hiyo.πŸ˜…πŸ˜…

Wewe nionyeshe hiyo sheria niisome ili nione kama nakubaliana na wewe au la!

πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€

Na Mimi sitaki uumie ndio maana nimekurahisishia kazi.
Wanawake kama ninyi mnaopenda harakari Sisi kina Taikon ndio Dawa yenu.
Hao wengine mnawaonea tuuπŸ˜‚πŸ˜‚

Hakuna sheria ya hivyo, hapo nimeitaja sheria kama kiwakilishi cha dhana iliyopo ndani ya jamii
 
Kumbe umejiropokea, haya kwaheri. Nimekosa cha kuchangia
 
Waendelee kutuita tu hivyo, wanawake wasiojitambua ndio wanakubali huo ujinga. Siku mkiachana unaondoka na furniture tu
Si bora furniture. Wanaondokaga na vijora tu. Mimi nimekataa huo ujinga. Kwanza unanioa unanikuta nna viwanja, kwako siji kizembe, sikai kizembe. Kila kitu naandikisha mwanangu. We vya kwako peleka unakojua ila sijaja hapa kusubiri tugawane mali. Ntatafuta niachie wanangu. Mwanaume anatafuta anamjengea hawara. Nani kichaa hapo.

Wanaume Wengi wanatabia ya kuzaa kama kumbikumbi huko nje, na anaweza tu akaamka akajiskia kwenda kumuoa mwajuma, wewe huku ulisshajiwekeza mzima mzima kwake utakuja kulia.

Wanawake jipambanieni, tafutieni watoto wenu maisha, mwanaume anaweza asiwe na uchungu na mtoto, atakutelekeza akaoe mwanamke mwengine unabaki na wanao mweupee huna mia
 
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
Oooh!
Bado unasafari ndefu kujua na kung'amua kile kilichoandikwa na ujumbe uliopo
mimi nina ushahidi na kesi ilyoamriwa mwanamke apewe 30% na mwanaume 70% ya thamani ya nyumba, ila huyo demu alijua ni pasupasu. aliangua kilio mahakamani.
sikutegemea uwe na uelewa sawa na huyo demu
 
Lakini mali inabaki ya mmiliki. Anamhusisha tu kama anataka kuuza etc.
HUWEZI kusema hili shati ni langu kama huruhusiwi kulikata mikono bila idhini ya mjombaako! Shati ni lako kama unaweza kulichana ddkio bila kuomba idhini. Simplest logic there is.

Kiwanja ambacho huwezi kukopea mkopo ufanye mambo mengine au kuuza uhame uswahilini au kugawia mtoto wako anaelala kwa shemeji yake, mpaka kwanza upate idhini, hiyo nyumba sio yako!
 
Mwanamke anayejitambua hawezi kukaa nyumbani tu hata siku moja bila kuongeza kipato cha familia.
Hapo unakosea. Wengine hawaoi wanawake kwa lengo la kusaidiana maisha. Na ktk imani za watu kuoa ni ibada na wanawatumikia wake zao kwa Kila hali hata km wake hao wana kazi tena za heshima.

Tusipende kulazimisha matamanio au malengo ya mmoja yawe ya wote. Kwa wale wanao abudu (Waislam na Wakristu) hoja ya mwanamke kuwa na kazi/kutokuwa na kazi wanaijua vizuri. Kwa Wakristu kipengele Cha kusaidiana hakikumaanisha wote mkafanye kazi/muwe wafanyakazi/muwe na vipato. Kwa Waislam hii ndio iko wazi kabisa, hata mkeo akiwa Rais wa nchi wewe ni mpiga debe una LAZIMIKA kumhudumia hadi nguo za ndani.

Mwisho, hao unao waita wajinga ndio wanaishi kwa amani na waume zao kuliko hao unaoona werevu. Wanaume mnataka wanawake wawe na kazi ili wawasaidie majukumu. Kumbe ndio maana ndoa za sasa ni kimbembe. Sikatai wasiwe na kazi, la hasha, wawe na kazi kwa manufaa yao binafsi. Wewe mume ubaki mume Yani mtafutaji na mhudumiaji wa familia. Suala la kulazimisha kujua mshahara wa mkeo/kukaa na ATM card ya mkeo au kumlazimisha kuweka mezani mshahara wake ili uufanyie matumizi km wako ni upuuzi na unyanyasaji na ni dalili za kuyakwepa majukumu yako km mume. Kumbe ndio maana wanawake wengi Wana chepuka sababu hawatunzwi na waume zao kisa kila mtu ana kazi au kipato!!

Vijana wa kiume tambueni kazi/ nafasi ya mwanamke ktk familia kabla ya kuoa. Mwanamke haolewi kwa lengo lakuja kukusaidia maisha. Na wala usioe kwa lengo hilo, na km utaoa kwa lengo hilo jua ipo siku utajuta. Tafuteni pesa acha kuwategemea wake zenu kwani hayo sio makusudio ya Mungu kumuumba mwanamke.
 
Kwa taarifa ya zipo ndoa nyingi zenye matatizo ambao wake zao ni wamama wa nyumbani. Na kuna ndoa ambazo wote wanafanya kazi na ziko stable kabisa. Unayoongelea yamepitwa na wakati.
 
Ni yako, na siku mkiachana inabaki kuwa yako. Nina experience na hilo.
 
Kuwatunza wote au kumtunza mtoto? Toa mfano hai kwa hapo. Uache uongo... kuwatunza wote my foot?
 
Umeacha kuharisha matusi! Vizuri sana, naona unaanza kujirekebisha. Siku nyingine usirudie kuleta upumbavu wako wa kujibu-jibu hovyo kila mtu hapa jukwaani ukidhani ni mtoto mwenzako au mjinga. Shika sana adabu yako, tena ishike sana!
Kama wewe ni baba nafikiri wanao wana hasara sana. Hustahili kuheshimiwa kwa sababu kwa majibu yako kwenye uzi huu ni kuwa HUJIHESHIMU.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…