Sheria ya uhaini ya sasa iko kisiasa zaidi na inawanufaisha wanasiasa pekee, imepitwa na wakati, irekebishwe isaidie kwenye nyanja za kiuchumi kama walivyofanya wenzetu wa China, Korea Kusini, Singapore, Botswana, Mauritius.
Mfano leo Lissu akinyongwa taifa litapata faida gani.
Sheria isomeke, mtu yeyote atakayehujumu taifa au kuingia mkataba wa hasara kwa taifa ashitakiwe kwa uhaini, hakuna uhaini wa raia mmoja kupindua serikali, sheria ya uhaini na uasi wa kupindua nchi ibaki kwa wanajeshi na jeshi.
NASHAURI;
Wanaoingia mikataba inayosababisha hasara na mikataba isiyoisha kwa wakati mf. SGR, wakibainika washitakiwe kwa uhaini sio uhujumu uchumi.
Watakaobainika kununua mitambo iliyochakaa, mf. mabehewa, injini za treni, magari used ya serikali nk hao wote washitakiwe kwa kesi ya uhaini.
Watakaouza Bandari kwa kisingizio cha mkataba wa muda mrefu wa hasara wakibainika washitakiwe kwa uhaini wanyongwe na mali zao zitaifishwe.
Watakaoingia mkataba na kandarasi wa barabara ikibainika kujengwa chini ya kiwango, wote kandarasi na aliyeingia mkataba washitakiwe kwa uhaini, China wananyongwa.
Wanaoingia mikataba ya bei ya kutupwa ya viwanja vya ndege wakibainika hata kama waliingia mikataba zamani ni kesi ya uhaini sio uhujumu uchumi.
Mabwawa na vituo vya kuzalisha umeme, Gesi, mf. Bwawa la Nyerere kama tuliambiwa litazalisha megawati kiasi fulani zisipozalishwa aliyeingia mkataba apewe kesi ya uhaini.
Meli, na Vivuko; mf. Kigamboni, MV Victoria hakimalizi miezi 6 kimekufa, anayeingia mkataba apewe kesi ya uhaini, labda akili zitawarudi.
Atakayeuza archi ya serikali, mf. eneo la aridhi ya Tanganyika kama lile la Bagamoyo, atakapojulikana alihusika au kushawishi afungwe kwa uhaini na anyongwe.
Waliohusika na wanaoendelea kuuza hifadhi za taifa na wanyama pori wachunguzwe na washitakiwe kwa uhaini hakuna faini wala dhamana.
Madini ni rasilimali za Taifa, waliohusika na wanaoendelea kuingia mikataba ya kitapeli wachunguzwe na washitakiwe kwa uhaini.
Wanaohujumu makampuni na mashirika ya umma – kwa mfano TANESCO, TRC, TPA, TTCL, ATCL, TPDC, NHC na mengine, wachunguzwe na washitakiwe kwa sheria mpya ya uhaini.
Tukifanya haya ndani ya miaka 10 Tanzania itakuwa miongoni mwa nchi tajiri Afrika, lakini tukiendelea na sheria ya sasa ya kisiasa tutaendelea kuonea raia na kuleta migogoro ya wenyewe kwa wenyewe isiyo na faida kwa taifa, kama DRC.
Na Quinine wa JF.