Sheria za kufuata unapotaka kumuacha Mke kwa talaka

1)Talaka Moja, ni talaka rejea
2) Talaka ya Pili, talaka rejea
3) Talaka ya Tatu, hauwezi kumrudia mkeo tena,na kama utataka kurejea ni lazima kwanza aolewe na mwanaume mwengine aachike ndio unaweza kumuoa tena...na itabidi uanze utaratibu upya kama ule wa mwanzo wakati unataka kuoa kwa mara ya kwanza.

NB: Hizo talaka rejea inabidi umrejee kabla ya kipindi cha eda hakijamalizika,kama kikiisha na haujamrudia inabidi ukaoe tena.
- Hakuna talaka tatu kwa mpigo,hata ukisema umemuacha mkeo talaka 3 basi kisheria inahesabika ni moja tu na unaweza kumrejea.
-Katika uislamu talaka si lazima iandikwe ndo iwe halali ila hata ukitamka tu japo kwa masikhara basi inahesabika kuwa umemuacha mkeo...Talaka ni katika jambo ambalo halina mzaha,yaani ukweli wake ni talaka na hata kama unatania bado itahesabika ni talaka eg ukasema "mke wangu nimekuacha" but hukumaanisha lbd ulikuwa unamfanyia mzaha tu basi kisheria tyr umeshamuacha kweli..so uchunge sana ulimi wako ktk hili.
-Talaka tatu ndo hatua ya mwisho na ndo hapo ndoa imevunjika na haiwezi kutengamaa tena isipokuwa kwa utaratibu maalum kama niliouleza hapo juu.
 
1)Talaka Moja, ni talaka rejea
2) Talaka ya Pili, talaka rejea
3) Talaka ya Tatu, hauwezi kumrudia mkeo tena,na kama utataka kurejea ni lazima kwanza aolewe na mwanaume mwengine aachike ndio unaweza kumuoa tena...na itabidi uanze utaratibu upya kama ule wa mwanzo wakati unataka kuoa kwa mara ya kwanza...
Safi sana mkuu, nimekuelewa vizuri..
 
1)Talaka Moja, ni talaka rejea
2) Talaka ya Pili, talaka rejea
3) Talaka ya Tatu, hauwezi kumrudia mkeo tena,na kama utataka kurejea ni lazima kwanza aolewe na mwanaume mwengine aachike ndio unaweza kumuoa tena...na itabidi uanze utaratibu upya kama ule wa mwanzo wakati unataka kuoa kwa mara ya kwanza..
Kwa bahati mbaya au nzuri ni kuwa talaka za kiislam hazitambuliki rasmi katika kuvunja ndoa kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya 1971.Sheria ya ndoa inatambua talaka kutoka mahakamani tu.
 
Sio sahihi mkuu, kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya Tanzania, ndoa za namna tatu ndo zinatambulika nchini kwetu nazo ni Civil Marriage (Ndoa za Kiserikali/Bomani), Customary Marriage (Ndoa za Kimila) na Religious Marriage (Za kidini na hapa hususani inakusudiwa Dini ya Kiislam). Ikiwa ndoa ya KIISLAMU inatambuliwa na Sheria basi bila shaka na utaratibu wake wa kuachana (talaka) unatambulika na kukubalika pia.

Kuna Mashauri mengi tu ambayo yanapelekwa Mahakamani na wanandoa waislamu na sheria inayotumika katika kuhumu kesi yao ni sheria za kiislamu iwapo ndoa hiyo kimsingi ilifungwa kwa taratibu za kiislamu. Kinachofanyika Mahakamani ni kwenda kutafuta Amri (Divorce Decree) tu ya Mahkama na sio kuachanishwa na hii sio lazima waislamu kuifanya, na mahkama haitoi hiyo Decree kwa wanandoa waislamu mpaka ijiridhishe kuwa tayari talaka 3 zimeshatimia kwa mujibu wa sharia za kiislamu....eg. Mahkama haiwezi kutoa Divorce Decree ikiwa mwanamke kaachwa talaka moja coz kimsingi hapo inakuwa ndoa haijawa irreparably broken down (ndoa imevunjika na haiwezi kutengemaa tena) ambapo hatua hii inafikiwa tu ikiwa talaka tatu tayari zimeshatoka.

Ukisema talaka za kiislamu hazitambuliki rasmi katika kuvunja ndoa inamaana kwamba hao wanandoa watatambulika kuwa bado ni mume na mke jambo ambalo sio sahihi kwa maana kwa mujibu wa sheria yao ya kiislamu hawana ndoa tena...kama hivyo ndivyo, sasa ni nini msingi wa kusema sheria ya bunge haitambui talaka ya kiislamu? na ilhali ama itambue au isitambue hao watu tayari wameshaachana...?

Na hii dhana yako ukiipeleka kwenye suala la mirathi iwapo huyo mume atafariki utaona kabisa inavyokufa kifo cha kawaida. Mke akiachwa hana tena haki ya kumrithi mtalaka wake, swali la kujiuliza jee, huyu mke ambae aliachwa kwa kufuata utaratibu wa kiislamu tu, lets say kwa kutamkiwa tu kuwa ameachwa na hakuwahi kurejewa tena mpka mume anakutwa na umauti, anaweza kwenda mahakamani kudai mirathi ya marehemu mumewe kwa sababu tu Talaka yake haikutolewa na mahakama hivyo haitambuliki na bado alikuwa mke halali wa marehemu? hivyo mahakama impatie haki yake ya mirathi?
 
Kwa bahati mbaya au nzuri ni kuwa talaka za kiislam hazitambuliki rasmi katika kuvunja ndoa kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya 1971.Sheria ya ndoa inatambua talaka kutoka mahakamani tu.

Hio SHERIA WANAYOIELEWA NI WAPAGANI TU[emoji1321]
Ningefunga ndoa mahakamani au ingekua ndoa haifungwi ila mahakamani pekee,hapo labda kidooogo ningekuelewa
 
1)Talaka Moja, ni talaka rejea
2) Talaka ya Pili, talaka rejea
3) Talaka ya Tatu, hauwezi kumrudia mkeo tena,na kama utataka kurejea ni lazima kwanza aolewe na mwanaume mwengine aachike ndio unaweza kumuoa tena...na itabidi uanze utaratibu upya kama ule wa mwanzo wakati unataka kuoa kwa mara ya kwanza.

NB: Hizo talaka rejea inabidi umrejee kabla ya kipindi cha eda hakijamalizika,kama kikiisha na haujamrudia inabidi ukaoe tena.
- Hakuna talaka tatu kwa mpigo,hata ukisema umemuacha mkeo talaka 3 basi kisheria inahesabika ni moja tu na unaweza kumrejea.
-Katika uislamu talaka si lazima iandikwe ndo iwe halali ila hata ukitamka tu japo kwa masikhara basi inahesabika kuwa umemuacha mkeo...Talaka ni katika jambo ambalo halina mzaha,yaani ukweli wake ni talaka na hata kama unatania bado itahesabika ni talaka eg ukasema "mke wangu nimekuacha" but hukumaanisha lbd ulikuwa unamfanyia mzaha tu basi kisheria tyr umeshamuacha kweli..so uchunge sana ulimi wako ktk hili.
-Talaka tatu ndo hatua ya mwisho na ndo hapo ndoa imevunjika na haiwezi kutengamaa tena isipokuwa kwa utaratibu maalum kama niliouleza hapo juu.
Allah akufanyie wepesi kwa ufafanuzi uliochanga mipaka ya kisheria na kwa imani yangu inaeleweka kwa kiasi kikubwa
 
Mwanamke wa Kiislamu anafanyaje kama anataka kuachana na Mumewe ?

Je anaweza kumpa talaka Mumewe ?
 
Naomba kujua ndoa ya kiislam ili ihesabike imevunjika rasmi huwa ktk stage gani ya talaka? Talaka tatu na maana zake kila moja
Talaka katika Uislamu hutolewa na mume kwa mkewe na huwa directed kwa baba(kwa kuwa ndio aliekukabidhi, mf Mzee J mpokee mwanao Namtaliki talaka 1 sio mkewangu kuanzia leo. pawe na mashahidi wakuthibitisha hilo tamko, talaka mwisho ni tatu na hutolewa mojamoja hadi zikifika tatu hapo huna uwezo wa kumrejea huyo mke mpaka aolewe kwingine then akiachwa(isiwe plan et kaolewe then dai talaka nikuoe tena hiyo itakuwa haram) unaanza kuoa upya.
Talaka huwa ni moja hata kama ndani ya hiyo talaka umeandika namba kubwa eg 10 itahesabiwa ni moja tu.Allah Alahm
Kama hujanielewa kuuliza ruksa
 
KWA KUONGEZEA, MKE ANAYO HAKI YA KUDAI TALAKA NA ENDAPO MUME ANAKATAA KUTOA TALAKA LICHA YA UKATILI ANAOMFANYIA MKEWE, BASI MKE ANAWEZA KWENDA KWENYE BARAZA LAO HUKO (NADHANI BAKWATA) KUSHNIKIZA TALALA, NAO WAKILETA MAGHUMASH AU KUSHNDWA BAS MKE ANAKWENDA MAHAKAMANI

KWA UTARATIBU WA NCHI YETU YA TZ, MAHAKAMA NDYO CHOMBO CHA JUU CHA KUTAFSIRI SHERIA YA NDOA, HVYO IKTOA AMRI YA TALALA ENDAPO MUME ATAKATAA KUTOA TALAKA BAS MAHAKAMA INAYO MAMLAKA YA KUVUNJA NDOA HYO KISHERIA NA IKAWA TALAKA HALALI.

MWISHO LENGO LA KUTOA TALAKA MOJA NADHAN NI KUWEKA RESERVE YA KUHMILI HASIRA, IKIFKIA HATUA YA TALAKA 3 INA MANA HYO NDOA IMESHNDKANA

AIDHA, ENDAPO HAUTAMRUDIA MKEO BAADA YA KIPINDI CHA EDA KWISHO MAANA YAKE ITAHESABIKA HUYO SYO MKEO TENA NA KUMWOA TENA HAPO NI MPAKA AOLEWE NA MWINGNE AACHWE NDO ULE MATAPISH.
 
Mwanamke wa Kiislamu anafanyaje kama anataka kuachana na Mumewe ?

Je anaweza kumpa talaka Mumewe ?
Anaomba Talaka,inayoitwa khulu,lazima aende kwa kadhi,na hata akienda lazima sababu zake ziwe zenye uzito maana kama kuna halal inayomchukiza Mungu ni Talaka.
 
Sawa mkuu,
kwahiyo kama mwanaume ataonekana anamakosa yanayostahili kuachana.
Mume analazimishwa kutoa talaka ?
Au Kadhi mwenyewe anaruhusiwa kuvunja ndoa hiyo ?
Maana mume anaweza kugoma kutoa talaka sasa sijui inakuwaje hapo.
 
Itavunjwa bakwata kama mume amekutwa na makosa na mwanamke amekataa suluhu.Kazi kubwa ya kadhi ni kutafuta suluhu katika ndoa hiyo,na haichukui siku moja taklaka hyo kutolewa,hapana itachukua muda mpaka suluhu ishindikane na mke aseme hapana hawezi kuendelea na ndoa hiyo,Kwa mfano ukipata ajali gegedo likawa halifanyi kazi tena ndoa hamna mkuu itavunjwa kuepusha uzinzi kwa bibie.
 
Sawasawa mkuu.
 
1)Talaka Moja, ni talaka rejea
2) Talaka ya Pili, talaka rejea
3) Talaka ya Tatu, hauwezi kumrudia mkeo tena,na kama utataka kurejea ni lazima kwanza aolewe na mwanaume mwengine aachike ndio unaweza kumuoa tena...na itabidi uanze utaratibu upya kama ule wa mwanzo wakati unataka kuoa kwa mara ya kwanza.
Nashukuru sana mkuu nmeelewa vema
 
Talaka katika Uislamu hutolewa na mume kwa mkewe na huwa directed kwa baba(kwa kuwa ndio aliekukabidhi, mf Mzee J mpokee mwanao Namtaliki talaka 1 sio mkewangu kuanzia leo. pawe na mashahidi wakuthibitisha hilo tamko, talaka mwisho ni tatu na hutolewa mojamoja hadi zikifika tatu hapo huna uwezo wa kumrejea huyo mke mpaka aolewe kwingine then akiachwa(isiwe plan et kaolewe then dai talaka nikuoe tena hiyo itakuwa haram) unaanza kuoa upya.
Talaka huwa ni moja hata kama ndani ya hiyo talaka umeandika namba kubwa eg 10 itahesabiwa ni moja tu.Allah Alahm
Kama hujanielewa kuuliza ruksa
Je unauhakika kama talaka hudirectiwa kwa mzee wa mke?
Talaka huandikwa kwa kuanza na mwandishi kuandika majina yake kamili, kuandika neno nimemuacha na kuandika majina kamili ya mke na humalizwa kwa kuandikwa tarehe.
 
Umeenda OP totally KUACHA na TALAKA wapi na wapi we hujuwi kiswahili Kabisa hayo ni maneno mawili yenye maana tofauti.
 
Back
Top Bottom