Nauliza hivi
Kuna binti rafiki angu antaka kumuoa alitengana na mumewe tangu 2015 akarudi kwao baada ya kutokea ugomvi na familia ya mumewe wa zamani
Sasa baada ya rafiki kuonyesha nia ya kumuoa binti
Mumewe ndo kaja jana kwao na binti kutaka suluhu je sharia inasema vipi kuhusu hili maana toka 2015 january mpk 2018 juni
Kwanza lazima itambulike kuwa je Alimpa Talaka au walitengana pasina kupeana talaka? Mosi
Pili, Je kama alimpa talaka ilikuwa ya kwanza au ya pili ambayo ina nafasi ya Rejea?
Kama alimpa Talaka Tatu, kwa sharia ya dini yetu tukufu ya kiislam hawezi kumrudia ila mpaka aolewe na mtu mwingine na aachike tena ndo ataweza kumuoa
Sasa tuje katika kila scenario moja moja hapo juu
1. Scenario 1: Walitengana tu
Hii ina maana huyu bado ni mke wake halali hawezi kuposwa na mwanaume mwingine. Kama mwanamke angetaka ajulikane mtalaka angeenda kwa kadhi ambaye zingefuatwa taratibu za kumuita mumewe na hatimaye kusuluhisha na kama hakuna suluhu basi Talaka ingefuata hivyo angekuwa huru kuolewa baada ya muda wa eda kuisha
2. Scenario: Alimpa Talaka 1
Kama alimpa Talaka moja alikuwa na nafasi ya kumrejea kabla ya muda wa eda haujaisha (siku 90/100 nisahihishwe hapa) toka alipompa Talaka ya kwanza. Kama hakuwa mwenye kumrejea bhasi huyo mwanamke si mkewe tena
Na kama alimpa talaka angali mwanamke ana mimba, eda ya huyo mwanamke ilikoma mara baada ya kujifungua. Mfano kampa talaka leo huyo mwanamke ana mimba na akajifungua siku ya pili, huyo si mke wake tena. Na kama alimpa talaka wakati mjamzito akaja kujifungua miezi 8 mbele eda ndo itakuwa imeishia hapo na si ndani ya zile siku 90/100
3. Scenario 3: Alimpa Talaka ya pili
Hii itakuwa kama hapo scenario ya pili
4. Scenario 4: Alimpa talaka ya tatu
Hii ina maana tayari aliwahi toa talaka ya kwanza wakarejeana, then akatoa talaka ya pili bado kuna nafasi ya kurejeana. Akishamaliza Talaka ya tatu, hakuna nafasi ya kurejeana tena hapa zaidi mpaka huyo mwanamke aolewe tena (na sio kwa kumpanga mtu amuoe halafu amuache laa) na mwanaume mwingine na aiachwa basi si kwa shinikizo la huyu mume wa awali
TURUDI KWA TALAKA MOJA NA MBILI
Sasa kutokana na muda kuwa umeisha wa eda kwa mujibu wa swali lako, na kama waliachana kwa talaka na jamaa anataka kumrejea mwanamke huyu, taratibu zote za kufungwa ndoa mpya zitafuata. Hii ikiwa na maana ya kutoa mahari iliyoridhiwa na mwanamke mwenyewe na ndoa kufungwa upya kwa kufuata sheria za dini yetu tukufu ya kiislam.
Vinginevyo kama hy mwanamke aliachwa kwa talaka na hayupo radhi kurejeana na mwanaume huyo wa awali, basi anahaki ya kuolewa na mwanaume mwingine yyt ampendae lakini mwislam
HAKIKA MWENYEZI MUNGU ANAJUA ZAIDI
Note: nimejibu kwa upana zaidi ili kupunguza maswali ambayo yangekuja kwa kujibu kwa kifupi