Kadhi Mkuu 1
JF-Expert Member
- Feb 4, 2015
- 19,687
- 23,689
Ukishamwacha talaka ya tatu ni PM namba yake nimsaidie.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naomba kujua ndoa ya kiislam ili ihesabike imevunjika rasmi huwa ktk stage gani ya talaka? Talaka tatu na maana zake kila moja
jazakuum llah kheir1)Talaka Moja, ni talaka rejea
2) Talaka ya Pili, talaka rejea
3) Talaka ya Tatu, hauwezi kumrudia mkeo tena,na kama utataka kurejea ni lazima kwanza aolewe na mwanaume mwengine aachike ndio unaweza kumuoa tena...na itabidi uanze utaratibu upya kama ule wa mwanzo wakati unataka kuoa kwa mara ya kwanza.
NB: Hizo talaka rejea inabidi umrejee kabla ya kipindi cha eda hakijamalizika,kama kikiisha na haujamrudia inabidi ukaoe tena.
- Hakuna talaka tatu kwa mpigo,hata ukisema umemuacha mkeo talaka 3 basi kisheria inahesabika ni moja tu na unaweza kumrejea.
-Katika uislamu talaka si lazima iandikwe ndo iwe halali ila hata ukitamka tu japo kwa masikhara basi inahesabika kuwa umemuacha mkeo...Talaka ni katika jambo ambalo halina mzaha,yaani ukweli wake ni talaka na hata kama unatania bado itahesabika ni talaka eg ukasema "mke wangu nimekuacha" but hukumaanisha lbd ulikuwa unamfanyia mzaha tu basi kisheria tyr umeshamuacha kweli..so uchunge sana ulimi wako ktk hili.
-Talaka tatu ndo hatua ya mwisho na ndo hapo ndoa imevunjika na haiwezi kutengamaa tena isipokuwa kwa utaratibu maalum kama niliouleza hapo juu.
Kwa bahati mbaya au nzuri ni kuwa talaka za kiislam hazitambuliki rasmi katika kuvunja ndoa kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya 1971.Sheria ya ndoa inatambua talaka kutoka mahakamani tu.
Je unauhakika kama talaka hudirectiwa kwa mzee wa mke?
Talaka huandikwa kwa kuanza na mwandishi kuandika majina yake kamili, kuandika neno nimemuacha na kuandika majina kamili ya mke na humalizwa kwa kuandikwa tarehe.
MUJARABUU ILA NI KUTALIKI SIO KUACHA, UKISEMA NIMEKUTALIKI HIYO NI TALAKA MOJAKWA MOJA ILA UKISEMA NIMEKUACHA UTAJIULIZA UMEMUACHA WAPI, LINI, KIVIPI, NA NANI. HIVYO MSAMIATI SANIFU NA FASAHA KATIKA TALAKA NI "TALIKI"Talaka ya Sunnah: Nayo ni mume kumuacha mkewe katika utwahara ambao hujawahi kukutana naye kimwili.
Talaka Bid‘ah (Uzushi): Ni mume kumuacha mkewe akiwa katika siku zake za ada, au katika kipindi cha damu ya uzazi, au katika twahara aliyomuungilia au kumuacha talaka tatu kwa mpigo mmoja. Mwenye kutoa talaka aina hii huwa ana madhambi lakini talaka yenyewe huwa imepita ila ile ya tatu huhesabiwa kuwa ni moja tu.
Talaka Baain: Ni ile ambayo mume anamuacha mkewe akakosa haki ya kumrejea kwa kuwa eda imekwisha. Hivyo, mume huyo akawa ni mposaji kama waposaji wengine na mke akikubali inabidi mume apose, atoe mahari na ifungwe ndoa upya.
Talaka Rejea: Hii ni ile ambayo mume anamiliki haki ya kumrejea mtalaka wake. Huku ni mume kumrejea mkewe katika kipindi cha eda la kuachwa talaka ya kwanza au ya pili.
Talaka Bayana: Hii ni talaka iliyo wazi kabisa isiyo na utata aina yoyote. Nayo ni kamakusema: “Nimekuacha”. Na talaka hii si lazima ukusudie kwani tamko lako linatosha.
Talaka Kinaya (isiyo bayana): Hii ni lazima ukusudie talaka kwa kuwa tamko lako si bayana kama kusema: “Nenda kwa ndugu zako” au “Usiseme na mimi” na yanayofanana na hayo. Ikiwa talaka imenuiwa basi itakuwa imetuka.
Talaka ya hapo kwa hapo: Ni ile ambayo inapotolewa mke huachika hapo hapo bila kuchelewa. Hiyo ni kusema: “Wewe umeachika” baada ya mume kutamka hayo mke atakuwa ameachika.
Talaka ya Kutungika: Ni ambayo mume ameitungika juu ya kitu kingine kuwa kitu hicho akikifanya au akikiacha atakuwa ameachika. Mfano ni mume kusema: ukitoka hapa nyumbani utakuwa umeachika” na mfano kama huo.
Talaka ya Khiyari: Hii ni mume kumwambia mkewe nimekupatia khiyari kutengana nami au kubaki nami. Akichagua kutengana talaka itakuwa imepita. Hii ni kama Anavyotueleza Allaah Aliyetukuka kuhusu uteuzi waliopatiwa wakeze Mtume na Mtume mwenyewe (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kama ilivyo katika Suratul Ahzaab (33), Aayah ya 28.
Talaka kwa Uwakala au Maandishi: Mume kama atamuwakilisha mtu mwingine kumuacha mkewe au akamuandikia mkewe talaka akimuarifu katika maandishi hayo kuwa amemuacha, mke atakuwa ameachika.
Talaka kwa Kuharamisha: Hii ni kusema kwa mume kumwambia mkewe: Wewe ni haramu kwangu au unakuwa haramu, kama atakusudia kwa tamko hilo talaka itakuwa talaka, na kama atakusudia dhihari itakuwa dhihari naye atawajibika kwa tamko hilo kafara la dhihari.
Neno moja linaweza kuwa na maana zaidi ya moja inategemea na mazingira.MUJARABUU ILA NI KUTALIKI SIO KUACHA, UKISEMA NIMEKUTALIKI HIYO NI TALAKA MOJAKWA MOJA ILA UKISEMA NIMEKUACHA UTAJIULIZA UMEMUACHA WAPI, LINI, KIVIPI, NA NANI. HIVYO MSAMIATI SANIFU NA FASAHA KATIKA TALAKA NI "TALIKI"
MKE UNAMTALIKI HUMUACHINeno moja linaweza kuwa na maana zaidi ya moja inategemea na mazingira.
Kaka umemaliza yote, baarakallahu laka,1)Talaka Moja, ni talaka rejea
2) Talaka ya Pili, talaka rejea
3) Talaka ya Tatu, hauwezi kumrudia mkeo tena,na kama utataka kurejea ni lazima kwanza aolewe na mwanaume mwengine aachike ndio unaweza kumuoa tena...na itabidi uanze utaratibu upya kama ule wa mwanzo wakati unataka kuoa kwa mara ya kwanza.
NB: Hizo talaka rejea inabidi umrejee kabla ya kipindi cha eda hakijamalizika,kama kikiisha na haujamrudia inabidi ukaoe tena.
- Hakuna talaka tatu kwa mpigo,hata ukisema umemuacha mkeo talaka 3 basi kisheria inahesabika ni moja tu na unaweza kumrejea.
-Katika uislamu talaka si lazima iandikwe ndo iwe halali ila hata ukitamka tu japo kwa masikhara basi inahesabika kuwa umemuacha mkeo...Talaka ni katika jambo ambalo halina mzaha,yaani ukweli wake ni talaka na hata kama unatania bado itahesabika ni talaka eg ukasema "mke wangu nimekuacha" but hukumaanisha lbd ulikuwa unamfanyia mzaha tu basi kisheria tyr umeshamuacha kweli..so uchunge sana ulimi wako ktk hili.
-Talaka tatu ndo hatua ya mwisho na ndo hapo ndoa imevunjika na haiwezi kutengamaa tena isipokuwa kwa utaratibu maalum kama niliouleza hapo juu.
Na uzuri au ubaya pia uislam pia hautambui ndoa ama talaka yoyote isiyokuwa yenye kufuata tartibu za uislam kwa waislam, maana yake mkiwa waislam mmefunga ndoa yenu kwa mujibu wa tartibu na mila za kiislam kama mnataka kuachana hamna budi kufuata tartibu zilezile za dini yenu.Kwa bahati mbaya au nzuri ni kuwa talaka za kiislam hazitambuliki rasmi katika kuvunja ndoa kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya 1971.Sheria ya ndoa inatambua talaka kutoka mahakamani tu.
Nini maana ya talaka.??MKE UNAMTALIKI HUMUACHI
Kauli/Tamko la kuvunja ndoa linalotolewa na mume juu ya mkewe.Nini maana ya talaka.??
ndoa ya kanisani haifi hadi kifo au takala. kule kwa msajili majina yenu bado yanasomeka na hamtakiwi kufunga ndoa ingine kisheria hadi iyo ivunjwe. ukifunga ndoa wakati ipo inayoendelea ni kosa la jinai. be carefulWananzengo!!
Tushauriane jinsi ya kumsaidia huyu dada, ameachwa. Scenario iko hivi:
Kuna scenario kwamba watu walioana kwa ndoa ya kanisani kisha wakaingia mgogoro ndani ya miezi michache tu, mke akatoroka, akarudi kwao. Kisha baada ya miezi kadhaa akafuata mali zake kwa mumewe (zake/walizochuma pamoja), mumewe akubali kumpa kwa sharti la kwamba pawepo na mashahidi. Mke akatafuta mashahidi na mume akatafta mashahidi pia (miongoni ni wazazi wa mume na mke). Aliitwa pia polisi na balozi wa mtaa kusimamia usalama kwakua palikua na tishio la kuibuka kwa ugomvi wakati wa kugawana vitu.
Mume akaweka sharti mbele ya mashahidi kwamba waandikishane kwanza kila mali atakayochukua mwanamke na ikadraftiwa "hati ya kugawana mali" pale nyumbani na hati ikaeleza wazi kwa maandishi kwamba mke kachukua chake kwasababu "ndoa imevunjika"....wanandoa na mashahidi, polisi na balozi wakaweka sahihi zao na kila mmoja (mme, mke na polisi) wakapata nakala.
Kisha mke akaondoka na vitu vyake akarudi kwao na mume nae akaendelea na maisha yake, hawakuwa na mawasiliano tena. Lakini talaka ya mahakama haijatolewa mpaka sasa na wala hawajafanya mchakato wa kwenda mahakamani, ni mwaka tangu wamegawana mali.
Maswali:
1. Je, ndoa bado ipo kisheria? Kwanini?
2. Je bado wanandoa wanayohaki ya kuenforce ndoa yao (eg. Kukamatana ugoni)
3. Nani anayohaki ya kufungua shauri lolote kuhusu status hii. (e.g mke kudai arudi/ mume kudai mkewe)
4. Kuna makosa yoyote kisheria?
Na kule kuandikishana kwao kwamba wameachana haiwezi kuwa ni utetezi?ndoa ya kanisani haifi hadi kifo au takala. kule kwa msajili majina yenu bado yanasomeka na hamtakiwi kufunga ndoa ingine kisheria hadi iyo ivunjwe. ukifunga ndoa wakati ipo inayoendelea ni kosa la jinai. be careful
ni kupoteza muda tu, sheria haitambui kuandikishana huko. hakuvunji ndoa wala nini huko kuandikishana kwa mashahidi. kwani ndoa mlifungishwa na hao mashahidi au na mchungaji?...mbona ipo wazi?Na kule kuandikishana kwao kwamba wameachana haiwezi kuwa ni utetezi?
ni kupoteza muda tu, sheria haitambui kuandikishana huko. hakuvunji ndoa wala nini huko kuandikishana kwa mashahidi. kwani ndoa mlifungishwa na hao mashahidi au na mchungaji?...mbona ipo wazi?
umesema kweli, yeye alitaka alazimishe kwamba kwasababu waliandikishana na aliondoka mwenyewe, ndoa inaweza kuwa ilivunjika, pasipo kuvunjwa na mahakama. hapo bado ndoa ipo nzima.Ni kweli ni sheria, lakini huku kuandikisha sio kupoteza mda, na ukienda mahakamani kutafuta official talaka itakuwa raisi kupata hata huyo binti asipotokea kwa maana alisha ridhia kuachana 100%... so huko kuandikishana kutakusaidia kuelekea officia talaka, so ulifanya vyema!
Sasa hiyo karatasi pekee haiwezi kukusaidia, ila ni nyenzo nzuri ya kufanya hatua itakayokusaidia sana ndugu!
Duh...ok!Ni kweli ni sheria, lakini huku kuandikisha sio kupoteza mda, na ukienda mahakamani kutafuta official talaka itakuwa raisi kupata hata huyo binti asipotokea kwa maana alisha ridhia kuachana 100%... so huko kuandikishana kutakusaidia kuelekea officia talaka, so ulifanya vyema!
Sasa hiyo karatasi pekee haiwezi kukusaidia, ila ni nyenzo nzuri ya kufanya hatua itakayokusaidia sana ndugu!
ni kupoteza muda tu, sheria haitambui kuandikishana huko. hakuvunji ndoa wala nini huko kuandikishana kwa mashahidi. kwani ndoa mlifungishwa na hao mashahidi au na mchungaji?...mbona ipo wazi?