Sheria za kufuata unapotaka kumuacha Mke kwa talaka

ndoa ya kanisani haifi hadi kifo au takala. kule kwa msajili majina yenu bado yanasomeka na hamtakiwi kufunga ndoa ingine kisheria hadi iyo ivunjwe. ukifunga ndoa wakati ipo inayoendelea ni kosa la jinai. be careful
Rudia tena kwanza!
 
Jamani, mkichokana mnafanyaje sasa?
 

anyways. Ok.... but mahakama inayotoa talaka in factors inazohusika nazo, hii paper can be supportive, that is all I am saying.. hata mahakama haiwajui hawa, so kuna input lazima wapate, that paper can be one of the input. WEWE UNAONGELEA SHERIKA KWENYE MAKARATASI, MIMI NAONGELEA BOTH MAKARATASI NA PRACTISE......
 
Hayo makubaliano yenu mwende nayo hivyohivyo tu, lakini siku mmoja akibadili gia angani na kwenda mahakamani, matokeo ndio haya unayopewa, ndoa bado ipo kisheria. Mahakama inazitambua ndoa za kimila na kidini lakini haitambui talaka zake, full stop.

Hivi mnasomaga vitu watu wanvyoandika kabla ya kukoment? nimesema lazima aende mahakamani na hizi document zitamsaidia huko mahakamani! wewe UNAONGELEA SHERIA KWENYE MAKARATASI, MIMI NAONGELEA KWENYE MAKARATASI NA PRACTICE!
 
Hii stori ya kutunga. Hivi ni.mali gani walizochuma wakati ndoa yenyewe imetimiza miezi michache tu? I can't believe this story.
 
Swala hapa ni kibali cha kuoa au kuolewa tena bila usumbufu.ila wote wanaoneka wehu.wanagawanaje mali/vyombo bila maamuzi hayo kuwa ya kisheria.

Hapo kivitendo ndoa ilishkufa ila kisheria bado ipo hai.kuepuka usumbufu wafuate taratibu za kisheria kulimaliza suala hilo.kwa sababu huyo mama anaweza kuja kumsumbu jamaa .

Walitumia busara zao ila siyo sheria.sheria ya ndoa iko wazi na haina mbadala
 
Nauliza hivi

Kuna binti rafiki angu antaka kumuoa alitengana na mumewe tangu 2015 akarudi kwao baada ya kutokea ugomvi na familia ya mumewe wa zamani

Sasa baada ya rafiki kuonyesha nia ya kumuoa binti

Mumewe ndo kaja jana kwao na binti kutaka suluhu je sharia inasema vipi kuhusu hili maana toka 2015 january mpk 2018 juni
 
Mhh!!
 
Asallaam alaikum.

Naam, kabla ya kusema turudi juu ya maandiko yako umesema kuwa wametengana je walitengana kwa talaka?
 
Nina swali la kisheria kuhusu talaka ya Kiislamu.

Kwa kuwa Tanzania haitambui dini yotote lakini wananchi wana uhuru wa kuabudu dini yoyote, Je, talaka ya maneno au ya kiandishi huwa inatambulika na serikali?

Kwa nchi kama Marekani, hata uwe na dini gani, lazima uende ofisi za serikali (city hall) kuapishwa na mke mtarajia, na kuomba leseni ya kuoa. Pia jaji au mtu mwenye leseni ya kukuoza ( justice of peace) lazima apige saini . Unarudisha fomu na kupewa cheti cha ndoa. Baada ya hapo, mnaenda kuoa kikabila au kidini.

Mkiachana, lazima muombe cheti cha kuachana. Bila hivyo, ndoa haitambuliki kuwa mumeachana.

Je, ndoa ya Kiislamu, mkiachana, lazima serikali ya Tanzania itambulishwe? Kuna " cheti cha kumwacha mume au mke"?
 
You are a real talentboy

Congratulation!
 
Kwanza lazima itambulike kuwa je Alimpa Talaka au walitengana pasina kupeana talaka? Mosi
Pili, Je kama alimpa talaka ilikuwa ya kwanza au ya pili ambayo ina nafasi ya Rejea?
Kama alimpa Talaka Tatu, kwa sharia ya dini yetu tukufu ya kiislam hawezi kumrudia ila mpaka aolewe na mtu mwingine na aachike tena ndo ataweza kumuoa
Sasa tuje katika kila scenario moja moja hapo juu
1. Scenario 1: Walitengana tu
Hii ina maana huyu bado ni mke wake halali hawezi kuposwa na mwanaume mwingine. Kama mwanamke angetaka ajulikane mtalaka angeenda kwa kadhi ambaye zingefuatwa taratibu za kumuita mumewe na hatimaye kusuluhisha na kama hakuna suluhu basi Talaka ingefuata hivyo angekuwa huru kuolewa baada ya muda wa eda kuisha
2. Scenario: Alimpa Talaka 1
Kama alimpa Talaka moja alikuwa na nafasi ya kumrejea kabla ya muda wa eda haujaisha (siku 90/100 nisahihishwe hapa) toka alipompa Talaka ya kwanza. Kama hakuwa mwenye kumrejea bhasi huyo mwanamke si mkewe tena
Na kama alimpa talaka angali mwanamke ana mimba, eda ya huyo mwanamke ilikoma mara baada ya kujifungua. Mfano kampa talaka leo huyo mwanamke ana mimba na akajifungua siku ya pili, huyo si mke wake tena. Na kama alimpa talaka wakati mjamzito akaja kujifungua miezi 8 mbele eda ndo itakuwa imeishia hapo na si ndani ya zile siku 90/100
3. Scenario 3: Alimpa Talaka ya pili
Hii itakuwa kama hapo scenario ya pili

4. Scenario 4: Alimpa talaka ya tatu
Hii ina maana tayari aliwahi toa talaka ya kwanza wakarejeana, then akatoa talaka ya pili bado kuna nafasi ya kurejeana. Akishamaliza Talaka ya tatu, hakuna nafasi ya kurejeana tena hapa zaidi mpaka huyo mwanamke aolewe tena (na sio kwa kumpanga mtu amuoe halafu amuache laa) na mwanaume mwingine na aiachwa basi si kwa shinikizo la huyu mume wa awali

TURUDI KWA TALAKA MOJA NA MBILI
Sasa kutokana na muda kuwa umeisha wa eda kwa mujibu wa swali lako, na kama waliachana kwa talaka na jamaa anataka kumrejea mwanamke huyu, taratibu zote za kufungwa ndoa mpya zitafuata. Hii ikiwa na maana ya kutoa mahari iliyoridhiwa na mwanamke mwenyewe na ndoa kufungwa upya kwa kufuata sheria za dini yetu tukufu ya kiislam.

Vinginevyo kama hy mwanamke aliachwa kwa talaka na hayupo radhi kurejeana na mwanaume huyo wa awali, basi anahaki ya kuolewa na mwanaume mwingine yyt ampendae lakini mwislam

HAKIKA MWENYEZI MUNGU ANAJUA ZAIDI

Note: nimejibu kwa upana zaidi ili kupunguza maswali ambayo yangekuja kwa kujibu kwa kifupi
 
Madam samahani hapo sentensi nanukuu " kwanza kukaa muda mrefu kwa mume bila kutimiza majukumu yako kwa mke tayari ni talaka" SI KWELI. Usipotoshe umma. Ittaqillaah
 
Tatizo mnajitia dini mwaijua ninyi tu. Alikuwa anawasiliana na mkewe? Wajua kutokuwasiliana na mwenza kwa muda mrefu kwa makusudi hukumu yake ni nini?
Wajua kumtamkia mtu kuwa humtaki si mumeo/ mkeo ni talaka?? Ngoja niishie hapa baadae ntarudi.
Asante madam kwa jibu lako
Lakini uislam hauendi kwa mazoea au kujuana nk.
Mosi, Naomba unipe japo hadithi au aya au dalili ya hayo usemayo kuhalalisha Talaka usemayo wewe ya kutokuwepo mawasiliano baina ya wanandoa ni tayari Talaka
Pili, umezungumzia suala jingine kabisa. Mume kumtamkia mke kuwa hamtaki/kamwacha hii ndiyo ni Talaka halali. Hili nakubaliana nalo lkn si kwa la juu hapo la muda
Wabillah Tawfiq
 
Swali hili nalo tulifanyie kazi kupeana elimu zaidi.
Mume kamuoa mke wakakaa muda mrefu tu mfano miezi sita LAKINI KATIKA kukaa kote huko HAJAWAHI KUFANYA NAE TENDO LA NDOA, Je
1. Akiachwa atakaa eda?
2. Je mume akifa, mke akiwa ndani ya ndoa ya namna hii suala la eda yake litakuwaje?
 
talaka ni mahakamani, ila watu tunaachana huku mitaani kwa vile hakuna cha kupoteza.
 
talaka ni mahakamani, ila watu tunaachana huku mitaani kwa vile hakuna cha kupoteza.
Ahsante kwa kujibu swali langu.

Serikali inapoteza data hapo ndio maana ni muhimu kuoa na kuachana bomani. Halafu tufanye sherehe tunavyopenda.

Sikubaliani vitu muhimu kama vyeti vya ndoa viwe vimeshikwa na wakuu wa dini bali na serikali tu. Hii itapunguza kyachana mitaani kama unavyosema na kuwa na data serikalini.
 
Ndugu zangu ndoa sasa hivi inawaka moto nimeishi na shemeji yenu miaka kumi ila sasa naona ni wakati sahihi kila mtu achukue time yake.

Naomba msaada wa kisheria ili tuachane kiamani kila mtu akafanye mambo yake kuanzia utaratibu wa kutoa taraka mpaka mwisho wa mahakama na kuchukua cheti changu cha talaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…