Ungekuwa umecheza mpira ungeelewa hoja ya mtoa mada. Ukweli ni kwamba mtenda kosa wa kwanza kabisa ni TFF wenyewe.. Wao ndio wenye wajibu wa kutunza rekodi zote za mchezo wa soka hapa Nchini! Wao ndio wenye kusema nani atashiriki katika mchezo na nani hatoshiriki!
Kabla ya mchezo wowote kuna kikao kinaitwa Pri-match meeting! Kikao hiki hushirikisha wadau muhimu katika mchezo, marefa, viongozi wa timu, kamisaa na wengineo. Hapa ndipo kila mmoja hupewa utaratibu wa mchezo. Ni jezi gani timu zitavaa, ni wachezaji gani wenye kadi wasioruhusiwa kwenye mchezo, ni muda gani mchezo utaanza nk.
Lengo la kikao hiki huwa ni kuondoa sintofahamu za kipuuzi ili hatimaye matokeo ya uwanjani yabaki salama.
Swali la kujiuliza ni je, kikao hiki kilifanyika? Na kama kilifanyika, je kilitimiza wajibu wake?
Ukianzia hapa ndipo utakuwa na uelekeo sahihi wa kujua kosa liko wapi!
Jambo lingine muhimu ni kujua nani aliwataarifu Simba juu ya kasoro hiyo lkn akaona sio muhimu kuwataarifu Kagera Sugar.
Ninaamini Kagera sugar na hata vilabu vingine wanastahili haki ya kupewa takwimu mbali mbali zihusianazo na mchezo wa soka hapa Nchini, na chombo pekee chenye wajibu huu ni TFF. Je, wanafanya hivyo?