Shetani, kwa nini haukuomba msamaha yaishe? Ulipewa nafasi ya kujirudi au basi tu na wewe ulikuwa mhanga wa Matrix? Au ni kiburi chako tu?

Nasikia aliomba msamaha ila kapigwa chini, sisi tunaambiwa tusamehe mara 70, ni uuuuuuuuuungwana?
 
Haya ni mawazo yako lakini sio sahihi. Mungu ni Mungu hajaumba bali yeye ndiye kaumba vyote. Shetani ni kiumbe. Na Mungu hawezi kupigana na shetani maana ni kiumbe tu. Sisi ndio ametuwezesha ili tupigane na shetani.
 
Haya ni mawazo yako lakini sio sahihi. Mungu ni Mungu hajaumba bali yeye ndiye kaumba vyote. Shetani ni kiumbe. Na Mungu hawezi kupigana na shetani maana ni kiumbe tu. Sisi ndio ametuwezesha ili tupigane na shetani.
Amewawezesha kupigana naye mbona hamumshindi sasa
 
Kwa kiburi Cha walimwengu wa Leo,shetani alikuwa mwema sana.
Wanamkana Mungu bila kupepesa
 
Mungu ni msamehevu, alimsamehe, Ila atamchoma moto siku ya mwisho 😆😆
 
Hiyo ya nne kama nimeielewa hivi, anyway thanks for good attempt 🙏
 
Sababu kubwa ya Iblis kumuasi mola wake ilikuwa ni kuikataa amri ya Mola wake kuwa amsujudie (Kumpa heshima ) Adam .

Iblis aliongozwa na Kiburi na Jeuri ambazo kiuhalisia kiumbe hutakiwi kuwa nazo kwasababu ni sifa zinazomstahili MUNGU peke yake. MUNGU ndiye mwenye jeuri na kiburi. Akiamua lake huwa na hamsikilizi yeyote yule sio binadamu,Jini wala Malaika.


Iblis alijiona kuwa ni bora kuliko Adam kwasababu aliumbwa kwa Moto na Adam aliumbwa kwa udongo wa mfinyanzi uliovunda. Hivyo akaona kiasili hawezi kulipa heshima dongo.Kutokana na hayo ndio alimkufuru Mola wake.


Suala la kutubu hakulitaka bali aliona bora aombe apewe uhai mrefu ili tu avipoteze vizazi vya adam aingie navyo motoni.

Mungu ameuumba Moto wa Jehannam kwa ajili ya wajeuri na wenye viburi katika kufata haki.
 
Shetani sio malaika na hakuwahi kuwa malaika. Mungu anaeleza kupitia kitabu kitakatifu cha Quran kuwa IBLIS alikuwa ni miongoni mwa majini.

Asili ya Iblis ni moto ila alipata nafasi ya kipekee kukua na kulelewa pamoja na Malaika huko mbinguni mara baada ya Malaika kuja duniani kuwapiga vita majini waovu waliokuwa wakifanya ufisadi katika hii ardhi tunayoishi sisi.

Iblis alikuwa ni mtoto mchanga sana hivyo malaika wakamuomba Mungu awaruhusu waende nae mbinguni. Alilelewa akiwa ni mchamungu wa hali ya juu. Mtume Muhammad (s.a.w) anaeleza kuwa hakuna ardhi katika dunia hii ambayo iblis hakuweka paji lake la uso kumsujudia Mungu.

Alimuabudu Mungu kwa miaka mingi ila alikuja kumuasi mara. aada kukataa amri ya Mola wake kumsujudia Adam.

Iblis aliniona kuwa yeye ni bora zaidi kuliko Adam kutokana na kuumbwa kwa Moto wakati Adam aliumbwa kwa udongo.

Adam alieashinda Malaika wote na Iblis akiwemo katikati yao katika mtihani waliopewa na Mungu. Adam alipewa elimu ya kujua vitu vingi sana ambavyo malaika pamoja na Iblis hawakuvifahamu. Hivyo Adam aliwazidi sana na ndipo Mungu akawaamrisha wamsujudie Adam kumpa heshima.Malaika wote walisujudu isipokuwa Iblis ambaye alikataa akaasi na kuwa miongoni mwa waliokufuru.
 
Nani aliyemuumba shetani?

Huyo ndiye wakumlaumu kwasababu alimuumba akampa na akili ya kuasi!!
 

 
Shetani alivuta bangi, SI unajua Tena ukivuta bangi kila kitu unachukulia poa tu!!!!
 
Nani aliyemuumba shetani?

Huyo ndiye wakumlaumu kwasababu alimuumba akampa na akili ya kuasi!!
kwahiyo unataka kumlaumu aliyekuumba na wewe kwasababu kakupa akili kama aliyopewa shetani na bado hapa unamkataa!!

Binadamu ni kiumbe mjinga sana yaani unamlaumu Muumbaji kwa kuumba kwake viumbe? Una akili sawasawa wewe.

Aisee ndio maana Mungu ameuumba moto wa jehanam kwa ajili ya viumbe wa sampuli kama hizi.
 
Kabla hajatuchoma moto sisi inatakiwa ajichome yeye kwanza kwa kosa lake mwenyewe la kumuumba shetani wakati yeye anajua yote - Hata anapomuumba shetani alikua anajua Shetani ataasi.

Na kama huyo Muumba ana uwezo wote, basi alitengeneza kila kitu kwa makusudi, ikiwemo uwezo wa kuuliza maswali na kutafuta ukweli kama ninavyokuuliza.

Kwa maekezo yako si sawa na kusema hata hii akili ya kuuliza kanipa yeye au?

Kwanza huyo Mungu unayemtetea Chanzo chake ni nini? Alitokea wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…