Najua hoja yangu itaibua ukinzani wa kitheolojia na niko tayari kwa hilo hata kama majibu hayatakuwa timely kwa sababu ya majukumu mengine. Mungu ametuumba na kutupa FREE WILL. Kazi ya kuona free will inafanya kazi amemuachia malaika huyo tuliyembatiza majina mengi tu likiwemo jina la SHETANI. Bila involvement yake hatuna free will. Yeye ni malaika anayetenda kazi kwa maagizo ya Mungu na kamwe hana uwezo wa kupigana na Mungu kama baadhi ya maandishi, aghalabu maongezo ya hadithi za kipagani yaliyopenyezwa kwenye biblia yanavyodai.