Elections 2010 Shibuda ahamia CHADEMA

Elections 2010 Shibuda ahamia CHADEMA

Umeona lakini nilivyokupigia extremes za anarchy na totalitalian systems halafu nikakurudisha kwenye middle way ya party politics na kwa nini ni muhimu kuwa na party vetting process?

Nimetumia extremes kama vehicles za kuona umuhimu wa middle way, tulipokuwa tunaangalia middle points tu tulikuwa hatuzioni katika larger context, sasa ukiingiz extremes zote ndipo unapoona kun umuhimu wa kuwa na middle way somewhere, not too hot, not too cold, just right.Then you can't get iced or torched, and you can actually enjoy the drink/ bath.

Kiranga bana

I always like your character. What I do, most of the time, I stay away (very far away) from your debates (one you are actively involved). This was too important for me to stay away.... I am glad you could see the middle.

Thanks
 
Mkenda 1000, mzee unamaanisha Shibula ni msikiti kwa nje lakini ndani ni ukumbi wa Disco??????? Hahaaaa hii kali:nod:

Maelezo yako juu ya huyu bwana ni SADAKTA!! Ninakugongea thanks!!
 
Kama mpaka saa hizi "Tetesi" hazijathibitishwa kuna mawili

1. haya yatakuwa ni majungu ya mshindi wa kura za maoni Maswa kumfukuza kueneza fitina kuhusu Shibuda akihofia kuwa alicheza rafu na huenda CC ikabinua meza ya matokeo ya kura za maoni na kumchukua Shibuda sasa anachofanya ni kueneza doubts na mkanganyiko, maana magazeti hayakawii kuchukua hii habari na kesho kuikuta ukurasa wa mbele.

2. Huu utakuwa ni mchezo wa Shibuda mwenyewe kutishia nyau CC ili wamchukue kama clean, hakutoa rushwa, maana aliisha sema CCM bila rushwa hakuna ushindi.

Cha kufanya ni kwamba mtoa mada athibitishe ama topic ifungwe
 
Kuwatumikia wananchi hakuna mipaka eti nyumba hii ni ya Chadema hii ni ya CCM, ukiwa mbunge unakuwa mtumishi wa wote ni sawa na rais anapochaguliwa anakuwa rais wa wananchi wote.

Siwelewi kina Kiranga and co. wanaposema watu wanaohama vyama wasipewe nafasi ya kugombea wana maana gani, kama chama hakikutaki au kimekufanyia faulo na unaona una uwezo kwa nini usitafute chama kingine?

Sote tumeona primaries za CCM zilivyokuwa chafu bado watu wanautetea huo uchafu kwa kulazimisha wagombea waliofanyiwa faulo wafie humo humo. Kama kuna chama wanaona kina ahueni na hewa safi wanauhuru kabisa wa kwenda huko.
 
Mkuu Kitila,
Hata kuzaliwa upya au kuokoka huja kwa kusikia neno, huyu neno kasikia lini. Hana tofauti na mtu anayehama dhehebu kwa vile kakosa cheo. Naheshimu uhuru wa mtu kuhama chama apendavyo ila kwa huyu jamaa nina wasiwasi naye. Je ana kitu cha ziada ambacho CHADEMA mtafaidika nacho kulinganisha na makombora ya Makamba kuwa huyo ni ''matapishi'' ya CCM. Kwa ufupi huyu jamaa hana staha ya kuwa CHADEMA labda kama chama chenu mmekuwa kokoro-sijui nimeandika sawa- lile linalovua samaki na matakataka mengine
Ngoja nikujibu kifupi tu kamwambie na Makamba wako naona unamtajataja sana kuwa tunayataka hayo 'matapishi'.
 
Lakini ukiniambia CHADEMA haina wagombea unaniambia udhaifu wa CHADEMA ambao CHADEMA inatakiwa kuuondoa kutoka ndani ya chama.

Mkiwakumbatia sana hawa rejects wa CCM kesho keshokutwa CCM watawafanyia bonge la takeover ya chama, kama James Mapalala alivyofanyiwa CUF.
Kiranga

Kwanini huu ushauri unaowapa Chadema usiwape CCM kiwe chama safi? Leo unaifundisha Chadema kuondoa udhaifu wa wagombea, kwani unazijua mbinu zao zote inawezekana mbinu mojawapo ni hii ya kuwapata viongozi toka vyama vingine wakiwemo wanaotoka CCM.

Afterall karibu viongozi wote wa vyama vya upinzani wametoka au walikuwa CCM, hebu tuambie mwaka 1980 nani alikuwa kiongozi wa upinzani. Tunavyojua kabla vyama vingi kuanzishwa CCM ilikuwa imehodhi karibu watu wote, sasa unapozuia watu kujiunga na upinzani unataka vyama vingine vitoe wapi wanachama wapya, Kenya? Kiranga wakati mwingine uwe unatumia hata a little common sense you have.
 
Kiranga yupo Far right, Nyani ngabu centre right, mwafrika centre left! ha ha ha interesting.
Ku sum up, kiranga anasema kama uliwahi kuwa mwanachama wa chama kingine huna nafasi Chadema, hata kama ulifukuzwa kwa misimamo mizuri tu. Mimi position yangu ni kuwa Chadema ipokee yoyote yule provided that the same person will embrace the norms, values and principle established. The vetting power should be exercised by the members based on the merits as stipulated by the bylaws/regulations or constitution.
That, new member should not be given special treatment as well as not deprived or denied their basic right.
 
Kiranga

Kwanini huu ushauri unaowapa Chadema usiwape CCM kiwe chama safi? Leo unaifundisha Chadema kuondoa udhaifu wa wagombea, kwani unazijua mbinu zao zote inawezekana mbinu mojawapo ni hii ya kuwapata viongozi toka vyama vingine wakiwemo wanaotoka CCM.

Afterall karibu viongozi wote wa vyama vya upinzani wametoka au walikuwa CCM, hebu tuambie mwaka 1980 nani alikuwa kiongozi wa upinzani. Tunavyojua kabla vyama vingi kuanzishwa CCM ilikuwa imehodhi karibu watu wote, sasa unapozuia watu kujiunga na upinzani unataka vyama vingine vitoe wapi wanachama wapya, Kenya? Kiranga wakati mwingine uwe unatumia hata a little common sense you have.

Kiranga anachofanya sio kibaya, ni lazima wanasiasa muwategemee watu kama Kiranga.

Yeye alishaamua kuwa kumtwanga Kikwete na CCM ni kuua nzi kwa mizinga (jaribu kupata picha) so huwa hapotezi muda huko.

Katika hili hapa amejikuta extreme views zake hazifanyi kazi vizuri na ameamua kurudi katikati.
 
Kiranga bana....mpaka nimeshindwa kuelewa hata unachobishania tena! Yaani sielewi kabisa. Total obfuscation....labda Mwafrika amekuelewa...
NN umesema kweli yaani anauliza baada ya muda anajijibu mwenyewe anasahau kama aliuliza swala hilo. Tatizo la Kiranga huwa ana muhe muhe wa kujibu haraka haraka bila kuelewa hoja inataka nini ni kama vile amesetiwa na jibu moja tu kichwani. Mfano kama kichwani ameseti jibu la 'hakuna kugombea kama umehama chama', hata akielezwa mbona katiba haisemi hivyo lazima jibu lake liwe hilo hilo moja tu.
 
Tatizo lako huelewi debate inavyoenda na hivyo huwezi kuelewa kwamba mii nina advocate merits za vyama kufanya ample vetting, na watu kuheshimu institutions na kuacha umalaya wa kisiasa, nimeonyesha extremes zote zilivyo mbaya (anarchy na totalitarianism) nikaonyesha jinsi middle way inavyoweza kutupa a sensible compromise.

Tatizo watu wanataka kushinda viti vya bunge bila mkakati ulio deeper than that, empty calories and fat, no nutrients, add nothing but weight, and they are not good for your health.

Huyo Shibuda hata akipata ubunge CHADEMA haina uhakika hata chembe kwamba loyalty yake iko kwa chama au Shibuda kama Shibuda mwenyewe.
 
Kiranga bana....mpaka nimeshindwa kuelewa hata unachobishania tena! Yaani sielewi kabisa. Total obfuscation....labda Mwafrika amekuelewa...

Kumwelewa huyu Kiranga, unatakiwa uende kwenye extreme ya whitest white ati!
 
Kiranga anachofanya sio kibaya, ni lazima wanasiasa muwategemee watu kama Kiranga.

Yeye alishaamua kuwa kumtwanga Kikwete na CCM ni kuua nzi kwa mizinga (jaribu kupata picha) so huwa hapotezi muda huko.

Katika hili hapa amejikuta extreme views zake hazifanyi kazi vizuri na ameamua kurudi katikati.

I am almost always moderate mazee, ila mimi ninaweza kuwa moderate katika a Kaluza-Klein spacetime continuum's 12th spatial dimension, wewe kama one dimensional carbon-based biped ukaniona extremist kwa sababu natumia extremist vehicles to drive moderate views home to you.
 
Another extreme position unajaribu kuchukua hapa mazee,

It will take time to bring you to the middle, hili nimeling'amua baada ya kufuatilia debates zako kwa muda. Ona hapo sasa, wewe tayari umengamua kuwa mimi ni .... what did you say again? ....

Okay ... tulikuwa wapi vile?

You see, how hard it can be (to some pple of course) kujua ni kipi exactly unaongelea. Mimi kwa vile naijua hii game ya kucheza na extremes, huwa nakuachia tu uwanja mazee.

Trust me, nikicheza hiyo game na wewe, itachukua miaka na pages kadhaa hapa kufikia kwenye introduction ya kile tunachotaka kuongelea.
 
Jamani anybody but Shibuda - I wouldn't touch this high power electric semi-conductor with a ten-foot-pole ! Huyu bwana kwa kubadilisha rangi hata kinyonga anamwonea wivu - kesho akiahidiwa kula hatasita kuwaacha kwenye mataa ama kwa kurudi CCM au kujitoa kwenye kinyang'anyiro dakika za majeruhi kwani ndivyo alivyo. Shibuda ! Labda aoshwe kwa mkorogo ama maji ya betri lakini kwa sabuni tu kaniki utaisugua weee kumbe rangi yake.
 
Mag3,

Tushasema, kesho keshokutwa yakiwakuta hawawezi kusema Mag3 na Kiranga hawakutuonya.
 
Jamani anybody but Shibuda - I wouldn't touch this high power electric semi-conductor with a ten-foot-pole ! Huyu bwana kwa kubadilisha rangi hata kinyonga anamwonea wivu - kesho akiahidiwa kula hatasita kuwaacha kwenye mataa ama kwa kurudi CCM au kujitoa kwenye kinyang'anyiro dakika za majeruhi kwani ndivyo alivyo. Shibuda ! Labda aoshwe kwa mkorogo ama maji ya betri lakini kwa sabuni tu kaniki utaisugua weee kumbe rangi yake.

Mag3,

Usijepata ugonjwa wa moyo bure?

Hizi bado ni tetesi tu (hakuna uthibitisho wowote uliotolewa kuwa Shibuda kahamia CHADEMA) as far as I know. kinachoongelewa hapa kati yangu na Kiranga (and NN) ni principles za kuhama vyama in general.
 
Word,

Lakini wanasema pia mwanzo wa ngoma lele, na liemwalo lipo na kama halipo laja. Nami nasema la uvundo hili halina ubani, hata liende chama gani hili Bendera lifuatalo upepo lililokosa kuvishwa pete CCM kwa kukosa kuwa chanda, litachovya chovya mpaka limalize buyu la asali kama jenzake Mrema kisha lirejee CCM tu, kwani chombo cha kuzama hakina usukani na sikio la kufa halisikii dawa. Dalili ya mvua ni mawingu, tushayaona mawingu haya aliposhindwa CCM sasa kwa nini tunataka kuchukua jitu liloshindwa ? Huyu ni mfuata nyuki atafutaye asali tu, hajui damu nzito kuliko maji na kwani hakuna watu CHADEMA damu wanaoweza kuchukua kiti hiki ? CHADEMA ikiacha mbachao kwa msaala upitao itajionyesha inakimbia mbio za sakafuni ziishiazo ukingoni.

Jino la pembe si dawa ya pengo, kanga hazai ugenini mpeni muda wa kukubalika kwanza.
 
Word,
v
Lakini wanasema pia mwanzo wa ngoma lele, na liemwalo lipo na kama halipo laja. Nami nasema la uvundo hili halina ubani, hata liende chama gani hili Bendera lifuatalo upepo lililokosa kuvishwa pete CCM kwa kukosa kuwa chanda, litachovya chovya mpaka limalize buyu la asali kama jenzake Mrema kisha lirejee CCM tu, kwani chombo cha kuzama hakina usukani na sikio la kufa halisikii dawa. Dalili ya mvua ni mawingu, tushayaona mawingu haya aliposhindwa CCM sasa kwa nini tunataka kuchukua jitu liloshindwa ? Huyu ni mfuata nyuki atafutaye asali tu, hajui damu nzito kuliko maji na kwani hakuna watu CHADEMA damu wanaoweza kuchukua kiti hiki ?

Jino la pembe si dawa ya pengo, kanga hazai ugenini mpeni muda wa kukubalika kwanza.

Kiranga,

Watu wa chadema watalitosa hili jamaa hadi utafurahi, wewe lipe nafasi tu ligombee huko ndani. Uzuri wa chadema hakuna watu wanaoshinda automatic as far as i know. Mambo ya super delegates wameyafuta.

This guy kwa jinsi ulivyoandika hapa, huko chadema atakusikia.

Mimi nilidhani Mpendazoe alikuwa na nafasi zaidi ya kushinda CHADEMA zaidi ya this guy.
 
Kuwatumikia wananchi hakuna mipaka eti nyumba hii ni ya Chadema hii ni ya CCM, ukiwa mbunge unakuwa mtumishi wa wote ni sawa na rais anapochaguliwa anakuwa rais wa wananchi wote.

Siwelewi kina Kiranga and co. wanaposema watu wanaohama vyama wasipewe nafasi ya kugombea wana maana gani, kama chama hakikutaki au kimekufanyia faulo na unaona una uwezo kwa nini usitafute chama kingine?

Sote tumeona primaries za CCM zilivyokuwa chafu bado watu wanautetea huo uchafu kwa kulazimisha wagombea waliofanyiwa faulo wafie humo humo. Kama kuna chama wanaona kina ahueni na hewa safi wanauhuru kabisa wa kwenda huko.

Wewe hujaelewa somo, tatizo si kwamba wasihame vyama. Mimi sitaki huu umalaya wa kisiasa na uroho wa madaraka wa kusubiri mpaka ushindwe primaries za ubunge ndio uhame chama. Kama unahama chama on principles bila tamaa ya madaraka poa tu, kaa miezi mitatu na kamisaa mnajadili mambo, soma literature za chama, unapigwa msasa watu wanakukubali.

Sio leo umelala CCM, kesho unaamka unakuwa CHADEMA, keshokutwa mbunge wa CHADEMA. Hata itikadi ya chama na sera zake hujui.

Mambo ya aibu hayo.
 
Back
Top Bottom