Kinachotuponza watanzania ni unafiki na kuwa waoga kupitiliza. Kwa ninayoyaona sasa, hata rais Samia hakuwa anakubaliana na mambo mengi sana ya Magufuli na alikuwa anaburuzwa tu. Kuwa sahihi zaidi, alikuwa ametengwa na hakuwa anashirikishwa kwenye mambo mengi ya maamuzi. Lakini ajabu na yeye alikuwa ameufyata na akabaki kuabudu na kutukuza. Anyways, siwezi kumlaumu sana kwani watanzania hawabebeki na ukijaribu kuwatetea, likikupata la kukupata wanajifanya kama hawaoni! Hii nchi bila wananchi kuamka na kuacha ''hewala bwana'' bado uongozi utaendelea kufanya makosa makubwa bila hofu. Rais Samia naye anajaribu kufuta yale mabaya ya Magufuli lakini naye anatengeneza mabaya yake mengi tu! Ni check and balance hakuna!