Shida haina hodi, mwenzenu nimefika mwisho, naombeni msaada

Shida haina hodi, mwenzenu nimefika mwisho, naombeni msaada

Pole hazitamsaidia ndugu makutopora wenye fursa mumpe, ningekuwa nayo ningempa ila ndo hivo hapa nimetoka zangu kuvuna viazi vitamu nikauze nipate japo ten!

KIDUMU CHAMA CHA JOBLESS PROMAX
C.E.O Hon. Intelligent businessman fanya mchakato kijana asaidike

NB: Kama una eneo kijijini rudi kalime hautajutia mkuu hukosa hela ya mahitaji muhimu, chakula, mavazi, malazi, dawa...
Kweli Boss! ... Asante mkuu
 
Kaka pole sana mtaani kwako umekosa hat bod boda jnaweza ukaanza kwa udeiwaka hasa kam unaweza kusosholaizi na wenzio mkuu usikate tamaa mi ni boda ktengo cha bajaji na nimesoma pharmacy kazi ni kipimo cha utu
 
Nina mazingira magumu sana mbele naona giza tu mpaka sioni thamani ya haya maisha.
Miaka miwili natafuta kazi, naishi kwa ndugu kwenye mazingira magumu, mama yangu ni mgonjwa na namuangalia anavyoteseka kila siku nikiwa sina namna ya kumsaidia.

Yoyote ambaye ana ofisi, biashara, taasisi au shughuli yoyote, SICHAGUI, naomba kazi au hata nafasi ya kujitolea kwa malipo au bila malipo (hata nauli tu inatosha - ili niweze kutoka nyumbani na kushughulisha kichwa).

Mimi ni graduate mwenye shahada, niko tayari kufanya kazi yoyote, tafadhali naamanisha yoyote ile. Mimi ni mchapakazi, naweza kusocialize na watu, napenda kuandika, kusoma vitabu na kufanya shughuli za kijamii.


WASIFU WANGU KWA UFUPI:


Umri - Miaka 30
Jinsia - Mwanaume
Taaluma - Bachelor of Social Work
Makazi - Dar es Salaam



Tunaambiwa wanaume inabidi tujikaze, tuwe strong ila mimi nimefikia mwisho kabisa wa uwezo wangu. NAOMBENI MSAADA WAKUU!
Msaada gani unaomba mkuu sema ndugu zako tupo
 
Back
Top Bottom