Shida ilivyonichochea kuwa mlafi wa kuisoma Biblia

[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Niliwahi kuulizwa swali, Unakiamini kitabu kinachoitwa Biblia nikajibu naamini. Pia nikaulizwa unazisadiki simulizi za mfalme Suleiman nikasema ndiyo.

Likaja swali kwanini moja kwa moja hakuhitaji utajiri na mengineyo ila aliomba sana upeo wa namna ya kuwaongoza wale aliyeambiwa anateuliwa kwenda kuwaongoza?

Hapo ungetoa jibu gani?
 
Inawezekana alifahamu tokea mwanzo kuwa HEKIMA NI BORA KULIKO VITU VYOTE; Mithali 4:7.
 
Shida haina adabu!

Huo ni usemi ambao nilizoea kuusikia kwa wakubwa nilipokuwa mdogo. Lakini baada ya kuwa mtu mzima, nimebaini kuwa japo shida si nzuri, lakini wakati mwingine huweza kukusababisha kukutana na mambo mazuri.

Miaka mingi imeshapita, lakini ningali nikikumbuka jinsi changamoto ilivyonisukuma na kuishia kuwa mlafi wa Biblia, tabia ambayo namshukuru Mungu kuwa nayo. Imenisaidia sana.

Bada ya kuhitimu kidato cha Sita, nilikuwa na matumaini makubwa kuwa ningeunganisha na masomo ya Chuo Kikuu mwaka huo huo. Tofauti na matarajio yangu, sikupata nafasi mwaka huo, na hata mwaka uliofuatia.

Kana kwamba hilo halitoshi, uchumi nao ulinibana vilivyo. Kila kitu kiligeuka kuwa kinyume na matarajio niliyokuwa nayo.

Baada ya kufanya kila nililolifahamu bila mafanikio, ikiwa ni pamoja na kushauriwa na watu mbalimbali, niliona mahali pekee pa kupata msaada ni kwa Mungu. Niliamua kwamba kama Mungu huwa anajibu maombi, na nilijua kuwa anajibu, basi wakati huo ndiyo uliokuwa wakati wa muhimu sana kujibiwa kuliko wakati mwingine wo wote ule niliowahi kuwa nao. Niliazimia kuomba kwa namna ambayo sikuwahi kuomba.

Lakini, pamoja na maamuzi hayo, bado nilikuwa na changamoto mbili.
Ya kwanza, sikujua jinsi ya kuomba maombi yatakayoniletea majibu niliyoyahitaji.
Na ya pili, niliuhofia uliwengu wa roho.

Nilikuwa nimeuzingatia ushauri uliotolewa na Mhubiri mmoja aliyeshauri kuwa kama mtu ni mwombaji sana, ni muhimu sana Neno la Mungu liwepo kwa wingi ndani yake. Anapoomba sana, macho yake ya kiroho hufunguka na kuweza kuuona ulimwengu wa roho na vilivyomo humo. Pasipo ufahamu wa Neno, anaweza akashindwa kutofautisha cha MUngu na cha adui.

Ikiwa ataingia katika uliwengu wa roho bila kuwa na ufahamu wa Neno la Mungu moyoni mwake, kuna hatari ya kuweza kupotoshwa au kuathiriwa vibaya. Ni katika ulimwengu wa roho ndiko anakopatikana Mungu na Malaika Wake, na pia Shetani na jeshi lake la mapepo. Lakini kwa kuwa Neno nla Mungu ni Nuru, hukusaidia kutofautisha giza na Nuru.

Ilinichukua miezi mitatu kuisoma Biblia nzima kuanzia kitabu cha Mwanzo hadi Ufunuo. Nilipomaliza hiyo awamu ya kwanza, nilinogewa na kuamua kuisoma tena kwa awamu nyingine, awamu ya pili.

Kwa jinsi nilivyohamasishwa na mambo niliyoanza kuyagundua kwenye Biblia, niliongeza bidii kiasi kwamba wakati mwingine nilikuwa nikitumia zaidi ya masaa ishirini kusoma. Ndani ya mwezi mmoja nilijikuta nimeimaliza Biblia kwa awamu ya pili.

Awamu ya pili ilifuatiwa na awamu ya tatu, ambayo yenyewe ilinichukua miezi kadhaa kuimaliza.

Hatimaye nilipata nilichokuwa nikikitafuta, na zaidi. Kwanza, nilijifunza jinsi ya kuitumia Imani kupata kazi, na hatimaye nikapata kazi.

Pili, kwa njia iyo hiyo ya Iman, niliweza kupata nafasi ya kuendelea na masomo ya Chuo, kipindi amabcho baadhi ya watu wangu wa karibu walikuwa wameshanikatia tamaa.

Zaidi ya hayo, niliyojifunza kwenye Biblia yaliendelea kunisaidia kuanzia kipindi hicho mpaka sasa. Kwangu mimi, Biblia ndiyo kitabu changu bora kuliko vitabu vingine vyote. Ninasoma vitabu mbali mbali, lakini kitabu namba moja ni Biblia. Kwangu, ni zaidi ya Kitabu.

Imenisaidia sana. Najua iliponitoa, ni mbali sana. Sijui ningelikuwaje leo hii kama isingelikuwa msaada wa Mungu nilioupata kwa Imani, baada ya kapata ufahamu wa Neno la Mungu kupitia Biblia! Kupitia Biblia, nilipata ufumbuzi wa changamoto ambazo Wasomi walishindwa kuzitatua.

Wakati mwingine ninapowasikia watu wakitilia mashaka uwezo wa Mungu, najikuta nawaonea huruma. Naamini wanafanya hivyo kwa kuwa hawajui kuwa hawajui.

Shida siyo nzuri, lakini zinaweza kukupelekea kupata vitu vizuri.
Kuna watu waliopata kazi zenye mishahara mikubwa sana baada ya kuachishwa kazi zenye mishahara ya kawaida.
Kuna watu waliofanikiwa kwenye biashara na kupata faida kubwa sana lakini ni baada ya kupata hasara kwenye biashara ya awali. Changamoto iliyowakumba haikuaacha kama walivyokuwa. Iliwasogeza mbele zaidi, kwenye mafanikio.

Inawezekana kwa sasa una changamoto unayokabiliana nayo. Rai yangu kwako ni hii: USIKATE TAMAA.

Kila siku amka ukiamini kuwa ndiyo siku ya muujiza wako. Fanya bidii kufanya lililo katika uwezo wako. Usihofu ikiwa matokeo yataendelea kuwa kinyume na matarjio yako. Muhimu ni wewe kuwa na bidii kutimiza wajibu wako.

Huenda matokeo yasiwe kama ulivyotarajia, lakini ikiwa utaendelea kufanya bidii kufanya yaliyo katika uwezo wako, ikiwa ni pamoja na kuendelea kujifunza namna bora zaidi ya kufanya yakupasayo, ipo siku utayafikia matokeo mazuri kuliko hata uliyoyatarajia.

Unaweza ukaishia kugundua ambacho usingegundua kama usingekutana na hiyo changamoto.

Shida zipo, na zitaendelea kuwepo. Lakini, unaweza ukazitumia kama daraja la kukupeleka kwenye mazuri.

Zinaweza zikawa zimekuja kwa lengo la kukuzamisha, lakini wewe zigeuze ziwe daraja la kuvukia. Hata ziwe kubwa kiasi gani, usiziruhusu ziingie moyoni mwako. Tazamia kesho yenye shangwe!!!

Ni wakati wako wa kung'aa sana kuzidi ulivyowahi kung'aa!!!
Amen.!

[emoji817][emoji817][emoji817][emoji817][emoji817]
Acha Mungu aitwe Mungu.!
We share like the same situation. I have seen God live faight for me.
 
Ni kanisa gani la kilokole a.k.a(wanenao Kwa lugha ambayo haina maana) unasali na JINA la mchungaji tunalihitaji pia,,,tangazo lako bado halijakamilika!!!
 
Mwandishi hajakosea ,Biblia ndio kitabu bora wakat wote hata usome vya ma genius gan,lakin bible is number one book yenye maarifa na kila kitu kihusucho ,mwanadamu kimwili na kiroho.
Popote kwenye maisha panahitaji matumaini.

Huwezi fananisha vitabu vilivyoandikwa na ma-genius ukapanga na bible. Hapo ni kuwatukana hao magenius.
Unataka kufananisha hata kitabu cha nadharia ya special relativity na kitabu cha bible!?

Bible inawezaje kuwa kitabu bora wakati kina contradiction za wazi kabisa,
Unapataje maatifa kwenye kitabu kilichosheheni utata mkubwa kama huo.

Nikisema biblia ni kitabu cha hadithi za uongo zilizotungwa na watu wajinga wajinga unaweza kubatilisha madai yangu kwa facts !?
 
Niliposoma Biblia, nilishangazwa kukutana na masomo yaliyohusu Ujasiriamali, Biashara, Uwekezaji, Management, Leadership, Jeshi, Afya, Saikolojia, ndoa, malezi ya watoto, n.k.

Biblia ni STOO ya MAARIFA.
Imani ni shambulio la psychology.
 
Hongera kwa kuujua ukweli,uko huru sasa.
 
Amen.!

[emoji817][emoji817][emoji817][emoji817][emoji817]
Acha Mungu aitwe Mungu.!
We share like the same situation. I have seen God live faight for me.
Hata mimi pia. Huwa nawashangaa sana na kuwasikitikia watu wanaomtilia MUNGU mashaka.
 
Unaelewa kuwa hata sie huwa tunawashangaa sana watu wanaoamini habari za Mungu asiyepo!?

Unalijua hili!?
 
Sidhani kwamba hujui kuwa MUNGU Yupo. Inaonekana umeamua kupinga huku ukijua kuwa unaupinga Ukweli.

Kama nia yako ingekuwa ni kutaka kumjua Mungu kwa undani zaidi, ungeweza kuelekezwa na ukasaidika. Lakini mwelekeo wako siyo huo. Ni
kama vile wa mtu mwenye akili
timamu aliyeamaua kuikana familia yake huku akijua alifanyalo. Anafahamu kabisa kuwa
"MAKOROBOI" ni mama yake wa kumzaa lakini anaamua kusema hadharani kuwa hamfahamu. Mtu kama huyo huwezi kumsaidia mpaka atakapoamua kubadilika.

Ingekuwa nia yako ni kumjua HUYU MUNGU ambaye wengine wanakiri kuwa amewatendea mambo makubwa, ungesaidika. Lakini kwa jinsi msimamo wako unavyojionesha, ni umeamua kupinga ingawa unajua moyoni mwako kuwa ufanyalo ni kosa.
 
Hoja yako yote umeijenga kwa kunidhania kuwa najua Mungu yupo ila nnapinga tu.

Kitu ambacho sio sahihi.

Siko hapa kujaribu mtu, nasema Mungu hayupo kwa hakika wala si kujaribu watu.

Kwahyo hoja yako ni batili.

Mungu hayupo, Mungu ni dhana iliyotungwa na watu,
Watu waliamua kujitungia tu kukidhi haja za akili zao walipojaribu kujibu maswali magumu yaliyowakabili.

Na kila jamii zina namna wanavyoeleza mambo hayo.

Kwahyo habari za miungu ni hadithi tu wala sio kweli ndugu.

Kama unabisha, thibitisha kweli huyo Mungu yupo.
 
Shida haina adabu!

Huo ni usemi ambao nilizoea kuusikia kwa wakubwa nilipokuwa mdogo. Lakini baada ya kuwa mtu mzima, nimebaini kuwa japo shida si nzuri, lakini wakati mwingine huweza kukusababisha kukutana na mambo mazuri.

Miaka mingi imeshapita, lakini ningali nikikumbuka jinsi changamoto ilivyonisukuma na kuishia kuwa mlafi wa Biblia, tabia ambayo namshukuru Mungu kuwa nayo. Imenisaidia sana.

Bada ya kuhitimu kidato cha Sita, nilikuwa na matumaini makubwa kuwa ningeunganisha na masomo ya Chuo Kikuu mwaka huo huo. Tofauti na matarajio yangu, sikupata nafasi mwaka huo, na hata mwaka uliofuatia.

Kana kwamba hilo halitoshi, uchumi nao ulinibana vilivyo. Kila kitu kiligeuka kuwa kinyume na matarajio niliyokuwa nayo.

Baada ya kufanya kila nililolifahamu bila mafanikio, ikiwa ni pamoja na kushauriwa na watu mbalimbali, niliona mahali pekee pa kupata msaada ni kwa Mungu. Niliamua kwamba kama Mungu huwa anajibu maombi, na nilijua kuwa anajibu, basi wakati huo ndiyo uliokuwa wakati wa muhimu sana kujibiwa kuliko wakati mwingine wo wote ule niliowahi kuwa nao. Niliazimia kuomba kwa namna ambayo sikuwahi kuomba.

Lakini, pamoja na maamuzi hayo, bado nilikuwa na changamoto mbili.
Ya kwanza, sikujua jinsi ya kuomba maombi yatakayoniletea majibu niliyoyahitaji.
Na ya pili, niliuhofia uliwengu wa roho.

Nilikuwa nimeuzingatia ushauri uliotolewa na Mhubiri mmoja aliyeshauri kuwa kama mtu ni mwombaji sana, ni muhimu sana Neno la Mungu liwepo kwa wingi ndani yake. Anapoomba sana, macho yake ya kiroho hufunguka na kuweza kuuona ulimwengu wa roho na vilivyomo humo. Pasipo ufahamu wa Neno, anaweza akashindwa kutofautisha cha MUngu na cha adui.

Ikiwa ataingia katika uliwengu wa roho bila kuwa na ufahamu wa Neno la Mungu moyoni mwake, kuna hatari ya kuweza kupotoshwa au kuathiriwa vibaya. Ni katika ulimwengu wa roho ndiko anakopatikana Mungu na Malaika Wake, na pia Shetani na jeshi lake la mapepo. Lakini kwa kuwa Neno nla Mungu ni Nuru, hukusaidia kutofautisha giza na Nuru.

Ilinichukua miezi mitatu kuisoma Biblia nzima kuanzia kitabu cha Mwanzo hadi Ufunuo. Nilipomaliza hiyo awamu ya kwanza, nilinogewa na kuamua kuisoma tena kwa awamu nyingine, awamu ya pili.

Kwa jinsi nilivyohamasishwa na mambo niliyoanza kuyagundua kwenye Biblia, niliongeza bidii kiasi kwamba wakati mwingine nilikuwa nikitumia zaidi ya masaa ishirini kusoma. Ndani ya mwezi mmoja nilijikuta nimeimaliza Biblia kwa awamu ya pili.

Awamu ya pili ilifuatiwa na awamu ya tatu, ambayo yenyewe ilinichukua miezi kadhaa kuimaliza.

Hatimaye nilipata nilichokuwa nikikitafuta, na zaidi. Kwanza, nilijifunza jinsi ya kuitumia Imani kupata kazi, na hatimaye nikapata kazi.

Pili, kwa njia iyo hiyo ya Iman, niliweza kupata nafasi ya kuendelea na masomo ya Chuo, kipindi amabcho baadhi ya watu wangu wa karibu walikuwa wameshanikatia tamaa.

Zaidi ya hayo, niliyojifunza kwenye Biblia yaliendelea kunisaidia kuanzia kipindi hicho mpaka sasa. Kwangu mimi, Biblia ndiyo kitabu changu bora kuliko vitabu vingine vyote. Ninasoma vitabu mbali mbali, lakini kitabu namba moja ni Biblia. Kwangu, ni zaidi ya Kitabu.

Imenisaidia sana. Najua iliponitoa, ni mbali sana. Sijui ningelikuwaje leo hii kama isingelikuwa msaada wa Mungu nilioupata kwa Imani, baada ya kapata ufahamu wa Neno la Mungu kupitia Biblia! Kupitia Biblia, nilipata ufumbuzi wa changamoto ambazo Wasomi walishindwa kuzitatua.

Wakati mwingine ninapowasikia watu wakitilia mashaka uwezo wa Mungu, najikuta nawaonea huruma. Naamini wanafanya hivyo kwa kuwa hawajui kuwa hawajui.

Shida siyo nzuri, lakini zinaweza kukupelekea kupata vitu vizuri.
Kuna watu waliopata kazi zenye mishahara mikubwa sana baada ya kuachishwa kazi zenye mishahara ya kawaida.
Kuna watu waliofanikiwa kwenye biashara na kupata faida kubwa sana lakini ni baada ya kupata hasara kwenye biashara ya awali. Changamoto iliyowakumba haikuaacha kama walivyokuwa. Iliwasogeza mbele zaidi, kwenye mafanikio.

Inawezekana kwa sasa una changamoto unayokabiliana nayo. Rai yangu kwako ni hii: USIKATE TAMAA.

Kila siku amka ukiamini kuwa ndiyo siku ya muujiza wako. Fanya bidii kufanya lililo katika uwezo wako. Usihofu ikiwa matokeo yataendelea kuwa kinyume na matarjio yako. Muhimu ni wewe kuwa na bidii kutimiza wajibu wako.

Huenda matokeo yasiwe kama ulivyotarajia, lakini ikiwa utaendelea kufanya bidii kufanya yaliyo katika uwezo wako, ikiwa ni pamoja na kuendelea kujifunza namna bora zaidi ya kufanya yakupasayo, ipo siku utayafikia matokeo mazuri kuliko hata uliyoyatarajia.

Unaweza ukaishia kugundua ambacho usingegundua kama usingekutana na hiyo changamoto.

Shida zipo, na zitaendelea kuwepo. Lakini, unaweza ukazitumia kama daraja la kukupeleka kwenye mazuri.

Zinaweza zikawa zimekuja kwa lengo la kukuzamisha, lakini wewe zigeuze ziwe daraja la kuvukia. Hata ziwe kubwa kiasi gani, usiziruhusu ziingie moyoni mwako. Tazamia kesho yenye shangwe!!!

Ni wakati wako wa kung'aa sana kuzidi ulivyowahi kung'aa!!!
My ordinary level was so sweet!!!

Yap so sweet but challenging !!!

An overcomer I was!But these days uuuuuuwwwiiiiiiiihh!!!!!!😭😭😭😭😭😭😭
 
Nimesoma mwanzo hadi ufunuo.. Yani agano la Kale hadi agano jipya mara moja

Nikasoma agano jipya Mathayo hadi Ufunuo Kwa kurudia mara mbili.

Ni bible race.. Hakika nimejikuta na uelewa mkubwa wa kujitambua mimi binafsi, mazingira yanayonizunguka na ulimwengu Kwa ujumla.
 
Very encouraging aiseee,nimesoma mara mbilimbili mkuu.
 
Back
Top Bottom