Shida zilipokubana uliwahi kuuza kitu gani kwa bei ya hasara ili ujinasue?

Simu ya laki 3 niliuza kwa 7500, ndio elfu saba na mia tano
 
Shida zisikie Tu Mku Mwaka 2015 nilikuwa na Pikipiki nimempa jamaa afanye bodaboda nikapata tatizo kubwa sana wakuu. Nilipata kesi ambayo huenda leo ningekuwa natumikia kifungo jela ma la heshima yangu ingekuwa imeondoka na imani yangu kwa watu.

Nikapata bahati ya kuongea na mlalamikaji pamoja Na mwendesha mashitaka tuimalize kifamilia. wakawa wanahitaji hela kiasi fulani hivi kwa haraka nikawaomba wasubiri kidogo mshahara uingie wakatisha ukichelewa kesi kesho naanza kuita Mashahidi.

Nilitafuta mteja usiku ule ule Niliinunua 1.3M lakini niliuza laki tano fedha taslimu nikaenda kuuza na TV yangu kwa elfu arobaini pamoja na friji langu la laki sita kwa laki mbili tu mzee.

Mwaka jana nilipata changamoto ya kazi sehemu nilifua kinoma hadi nikaanza kutamani visungura maana ya bai sina, kodi ikawa mzigo home nilienda kuuza kiwanja changu nilinunua 4M nikauza kwa 2M ya kupew kwa awamu.

BINADAMU WAKIJUA UNA SHIDA WANAWEZA KUFANYA NEGOTIATION NA MKEO, WARUDISHE MAHARI WAMCHUKUE
 
MTU CHAKE
 
nilishauza laptop kwa elfu 10 ,,,,,,,,,,,,ndiyo wee hesabu elfu moja moja yaaani buku 1,000 ziwe kumi ,,,ila ilikuwa mbovu ,,,,,,,,sema nilikuwa nahitahi nipate hela ya kutuma maombi ya chuo kikuu ardhi way back 2019 deadline ilikuwa ni kesho yake ...japo nilipata chuo ila ilinibidi tuuu maana nilikuwa sina msaada wowote ulee
 
Baada ya kufukuzwa kazi na ndani hakuna hata punje ya mchele watoto wameamka na mama yao hana cha kufanya ikinibidi kubeba kiatu changu aina ya cat ile original nikaanza kuzunguka kuhama nzima napiga uchinga kuanzia asubuhi hadi sa tisa mchana ndo napata mteja wa buku 20 nilikiuza huku machozi yananitoka lakin nilipata hela ya mchele na watoto wakala wali
 
Nimecheka Hadi nimepaliwa
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…