Shida zilipokubana uliwahi kuuza kitu gani kwa bei ya hasara ili ujinasue?

Shida zilipokubana uliwahi kuuza kitu gani kwa bei ya hasara ili ujinasue?

mengine hayavumiliki hayaelezeki mkuu..mimi binafsi nilishawai kusema kwenye maisha yangu sitakuja niuze kitu changu .
ila mwaka huu huu tu nilishataka kuuza pc yangu ya over 2m kwa ata laki tano tu nisolve mambo yalonitinga.
na hapo nilizunguka mnoo yan.
Mungu atusaidiee
 
Dah shida uzisikie tu Kwa wenzio tu ndugu, 2019 kibarua nimepoteza mtoto analia njaa mama ake mama wa nyumbani nikaanza kutoa kimoja kimoja tv, king'amuzi, Bomba la antenna ,showcase, na vingine kibao...afu hamna moment inauma unapoona uliyemuuzia Kwa bei kitonga anatumia mpaka kesho au Ile mtoto wako anauliza baba tv Iko wapi, baba blender tutengeneze juice, dah asee MUNGU atuepishe Kwa kweli . Tv Samsung Kwa laki??!! Blender 20, Jiko two plates kwenye box halijatumika Kwa 30???!!! Inauma sana mwisho nikaishia kuwa mdau wa double kick, cuca, robot na ma shit kama hayo yaani naomba isijirudie kamwe.
 
Gari niliyonunua milioni 5 nikiwa nimeitumia miezi miwili tu niliiuza kwa milioni 1 na laki 3 kumaliza kesi flani isifike mbali tumalizane kimya kimya, pesa ilikuwa inahitajika fasta hivyo mteja ilibidi awe wa fasta, kuna watu wengi wameishia jela kwa kuchukulia vitu poa kwa jicho la mtaani kwamba ni kawaida, unapopata nafasi ya ku negotiate itumie!

Laptop nilinunua laki 8, niliuza kwa laki 2 na nusu ili nikamilishe ada.
Uboho.
 
Ulibaka??
 
Nakumbuka nilikaa njaa siku 2 kuelekea ya tatu Plus Nina mjamzito Ndani Pikpk yangu ya 3M nikaiuza 650k ……Pia Nilishawah Nunua simu 1,950,000
Nikaja kupata shida nikaenda kuiweka bondi nikapewa 950,000 Baada ya mwezi nirejeshe 1,200,000
Mambo yakazidi kua mabaya mwezi umeisha nina 200k tu Nikaambiwa toa 200k kama Riba Then unaongezewa mwezi deni linabaki palepale mwezi unaofata nikafanya tena vile mwishoe nikakata tamaa kuna line nliiacha kwenye hio simu nikaenda tu nikaichukua line yangu nkaambiwa nimeshindwa sina jinsi Hivyo 950,000 - 400,000 = 550,000 ni kama nliuza ile simu kwa 550,000 Hapo ni miezi minne tu toka niinunue

MWISHO WA YOTE KILA UNAPOPITIA JARIBU ATA LIWE KUBWA KIASI GANI MUWEKE MUNGU MBELE PIGA GOTI CHINI FANYA IBADA
 
Nilichojifunza ukiwa na Shida kubwa, hakuna mtu wa nje wa kukusaidia, wewe mwenyewe na vitu uliyonayo ndio vina nafasi kubwa ya kukusaidia. Watu wengi unaowategemea watabaki kama watazamaji.
Nivizuri ukawa na vitu vinavyouzika kwa wepesi kwa ajili ya backup.

Namshukuru Mungu vyote nilivyoviuza baada ya msimu huo kupita vilirudi.
 
nilishauza laptop kwa elfu 10 ,,,,,,,,,,,,ndiyo wee hesabu elfu moja moja yaaani buku 1,000 ziwe kumi ,,,ila ilikuwa mbovu ,,,,,,,,sema nilikuwa nahitahi nipate hela ya kutuma maombi ya chuo kikuu ardhi way back 2019 deadline ilikuwa ni kesho yake ...japo nilipata chuo ila ilinibidi tuuu maana nilikuwa sina msaada wowote ulee
Sibora ungeiacha kwa stationery
 
Nilikunywa smart gin miaka miwili mpaka sukar ikashuka mwilini noma sana ........
Shida ni mwalimu anayetumia formula ngumu kukuelewesha topic usipo elewa ndo bai bai baba jeni maraaa kitanziiii shwaaaaaaaah....
 
Niliweka bondi dell inspiron core i7 ya laki 9 nikachukua 50k
Hp elite book 7th generation niliuza laki🤣🤣
Simu nishauza sana zote kwa vei ya hasara
Samsung s7 edge niliuza 15k
Fridge la laki 9 niliuza laki 2
Funga kazi ka cresta nilinunua milioni 3 kwa pesa ya kubeti nikauza laki 8
Visa vingi vimesababishwa na kamari hasa spin and win nashukuru mungu hua sikosi mteja
 
Dah shida uzisikie tu Kwa wenzio tu ndugu, 2019 kibarua nimepoteza mtoto analia njaa mama ake mama wa nyumbani nikaanza kutoa kimoja kimoja tv, king'amuzi, Bomba la antenna ,showcase, na vingine kibao...afu hamna moment inauma unapoona uliyemuuzia Kwa bei kitonga anatumia mpaka kesho au Ile mtoto wako anauliza baba tv Iko wapi, baba blender tutengeneze juice, dah asee MUNGU atuepishe Kwa kweli . Tv Samsung Kwa laki??!! Blender 20, Jiko two plates kwenye box halijatumika Kwa 30???!!! Inauma sana mwisho nikaishia kuwa mdau wa double kick, cuca, robot na ma shit kama hayo yaani naomba isijirudie kamwe.
The bump ungefuatilia huyu mtu
 
The bump ungefuatilia huyu mtu
daaah sikuweza kuona mkuuu walahi vile ningeona hiii Nisingemuamini

alichoandika hapo ndio maisha yake ya sasa ana piga hizo pombe hata ukimuona tu hujiulizi

ila kwakua case yake iko solved na ndugu zake haina shida sema Sikuweza hisi kama angekua hivi mapema Kiasi hiki
 
Back
Top Bottom