Shida zilipokubana uliwahi kuuza kitu gani kwa bei ya hasara ili ujinasue?

Shida zilipokubana uliwahi kuuza kitu gani kwa bei ya hasara ili ujinasue?

Dah shida uzisikie tu Kwa wenzio tu ndugu, 2019 kibarua nimepoteza mtoto analia njaa mama ake mama wa nyumbani nikaanza kutoa kimoja kimoja tv, king'amuzi, Bomba la antenna ,showcase, na vingine kibao...afu hamna moment inauma unapoona uliyemuuzia Kwa bei kitonga anatumia mpaka kesho au Ile mtoto wako anauliza baba tv Iko wapi, baba blender tutengeneze juice, dah asee MUNGU atuepishe Kwa kweli . Tv Samsung Kwa laki??!! Blender 20, Jiko two plates kwenye box halijatumika Kwa 30???!!! Inauma sana mwisho nikaishia kuwa mdau wa double kick, cuca, robot na ma shit kama hayo yaani naomba isijirudie kamwe.
Post hii kaiandika July 24 siku aliyopiga TUKIO asubuhi akiwa anatoka Ofisini SweetPain
 
nilishauza laptop kwa elfu 10 ,,,,,,,,,,,,ndiyo wee hesabu elfu moja moja yaaani buku 1,000 ziwe kumi ,,,ila ilikuwa mbovu ,,,,,,,,sema nilikuwa nahitahi nipate hela ya kutuma maombi ya chuo kikuu ardhi way back 2019 deadline ilikuwa ni kesho yake ...japo nilipata chuo ila ilinibidi tuuu maana nilikuwa sina msaada wowote ulee
Kumbe wee ni intake ya 2019? Daaah Dogo kabisaa. Lol
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Halafu ni msomi wa Chuo kikuu cha Dodoma.
Bachelor Degree ya Internal Relations.

Ninachoona hapa tabia ni kama ngozi, kuibadilisha ni ishu ngumu sana
Kwao hawamuelewi hadi wanahisi kalogwa sijui, kuna wakati naamini uchawi upo ila sijui kwakweli

nilishamuhisi ila sikutaka chukulia serious past life yake kwa kazi alizonambia kafanya na kwann kaacha

sikua na majibu mazuri nikasema acha nijionee namimi,sasa nmeshagundua hata huko aliacha kwann
 
Gari niliyonunua milioni 5 nikiwa nimeitumia miezi miwili tu niliiuza kwa milioni 1 na laki 3 kumaliza kesi flani isifike mbali tumalizane kimya kimya, pesa ilikuwa inahitajika fasta hivyo mteja ilibidi awe wa fasta, kuna watu wengi wameishia jela kwa kuchukulia vitu poa kwa jicho la mtaani kwamba ni kawaida, unapopata nafasi ya ku negotiate itumie!

Laptop nilinunua laki 8, niliuza kwa laki 2 na nusu ili nikamilishe ada.
Hiyo kawaida sana kwenye maisha mkuu. Assets utazipata tena tu
 
Gari niliyonunua milioni 5 nikiwa nimeitumia miezi miwili tu niliiuza kwa milioni 1 na laki 3 kumaliza kesi flani isifike mbali tumalizane kimya kimya, pesa ilikuwa inahitajika fasta hivyo mteja ilibidi awe wa fasta, kuna watu wengi wameishia jela kwa kuchukulia vitu poa kwa jicho la mtaani kwamba ni kawaida, unapopata nafasi ya ku negotiate itumie!

Laptop nilinunua laki 8, niliuza kwa laki 2 na nusu ili nikamilishe ada.
Nilikua nauza viwanja wiwili milion2.6 saizi jamaa anataka milion 1.6 nataka nikubal maana sina hata hela
 
Sitasahau nilivyopigiwa cm na kaka yangu kabisa akanipa mchongo wa kazi Tanga wkt huo nipo Arusha

Kwasababu skua na mke wakati huo na kazi ilikua ya muda mrefu na ukizingatia Tanga ndo home
Ikabidi niuze vitu vyote vya ndani kwa bei ya hasara
Kilichofuata kwakifupi kazi nilikosa nikaishia kulala nje kwa bro kwa miezi 6 kwasababu yeye alikua kaoa na chumba ni singo

Kwakweli iliuma Sana
 
Niliwekaga tangazo home nauza nguo zangu na nikawatafuta wadada wale masista duu waliokuwa wanakuja kukodishaga nguo zangu waje tufanye biashara.!!
Mzee alivyorudi akalichana tangazo tulikula mikanda mimi pamoja na wateja wangu, aiseee wazee wa kichaga jau sana 🤣🤣🤣

Ila bila kujua ile ndio ilikuwa hatma yangu, ss hivi nimekuwa winga mzoefu.!! 😹
 
Shida zisikie Tu Mku Mwaka 2015 nilikuwa na Pikipiki nimempa jamaa afanye bodaboda nikapata tatizo kubwa sana wakuu. Nilipata kesi ambayo huenda leo ningekuwa natumikia kifungo jela ma la heshima yangu ingekuwa imeondoka na imani yangu kwa watu.

Nikapata bahati ya kuongea na mlalamikaji pamoja Na mwendesha mashitaka tuimalize kifamilia. wakawa wanahitaji hela kiasi fulani hivi kwa haraka nikawaomba wasubiri kidogo mshahara uingie wakatisha ukichelewa kesi kesho naanza kuita Mashahidi.

Nilitafuta mteja usiku ule ule Niliinunua 1.3M lakini niliuza laki tano fedha taslimu nikaenda kuuza na TV yangu kwa elfu arobaini pamoja na friji langu la laki sita kwa laki mbili tu mzee.

Mwaka jana nilipata changamoto ya kazi sehemu nilifua kinoma hadi nikaanza kutamani visungura maana ya bai sina, kodi ikawa mzigo home nilienda kuuza kiwanja changu nilinunua 4M nikauza kwa 2M ya kupew kwa awamu.

BINADAMU WAKIJUA UNA SHIDA WANAWEZA KUFANYA NEGOTIATION NA MKEO, WARUDISHE MAHARI WAMCHUKUE
😆😆😆😆😆😆😆 Pole Mkuu
 
Baada ya kufukuzwa kazi na ndani hakuna hata punje ya mchele watoto wameamka na mama yao hana cha kufanya ikinibidi kubeba kiatu changu aina ya cat ile original nikaanza kuzunguka kuhama nzima napiga uchinga kuanzia asubuhi hadi sa tisa mchana ndo napata mteja wa buku 20 nilikiuza huku machozi yananitoka lakin nilipata hela ya mchele na watoto wakala wali
Sasa kiatu sio ishu
 
mengine hayavumiliki hayaelezeki mkuu..mimi binafsi nilishawai kusema kwenye maisha yangu sitakuja niuze kitu changu .
ila mwaka huu huu tu nilishataka kuuza pc yangu ya over 2m kwa ata laki tano tu nisolve mambo yalonitinga.
na hapo nilizunguka mnoo yan.
Mimi nadhani vitu vipo Kwa Ajili ya kutusaidia pale tunapohitaji kutatua Changamoto,Sasa ulisema huwezi kuuza ndio manake nini?
 
Back
Top Bottom