Ndio akili zetu wabongo za kimasikini, kumsubiria mtu ashuke alafu iweje, diamond kaza hata bakhresa walimtabiria atashuka kaanza na mikate, mandazi mara unga leo bakhresa ana bidhaa zaidi ya kumi sokoni, diamond platnumz kushuka kimziki atashuka muda wake ukifika na hata akifa kimziki bado kiuchumi atakuwa stable, leo hii ana label, studio na amefungua wasafi.com kwa ajili ya kuuza nyimbo online (idea kama ikifanikiwa, diamond atameki ela ndefu vibaya sana), perfume na bado Kuna bidhaa nyingi atauza kwa kutumia jina lake. Alafu mbona kila siku mnatabiria diamond kushuka kwani wasanii wengine hamuwaoni, manake tokea 2013 mlianza kutabiri lkn mpaka leo dogo yupo juu, alafu msipende kujipa unabii kwa kutabiri maanguko ya wenzenu wakati ww hujui unaanguka lini na huyo shigongo ana stress mitandao ya jamii inampa stress kwani siku hizi habari zake za kwenye magazeti watu washazisoma mitandaoni na ndio maana mauzo ya magazeti ya udaku yamepungua sana na msishangae nae akashindwa kuiendesha kampuni yake.