Shikamoo ni salamu ya ovyo

Shikamoo ni salamu ya ovyo

Ujikute we kwenu ndo last born hyo shkamoo utaitoa mpaka ukome mpaka kwa mashemeji af watoto wadogo tu
 
Mtoto wa miaka kumi akikusalimia 'habari yako'' au akasema 'hello'ni sahihi?

Mimi naona kama ni dharau
Salamu imekaa kimtego sana kwa watu wazima aisee.

Mtoto mdogo anatakiwa kunipa heshima kwa kuniamkia.

Ingawa wenzetu Wazungu wamezoea kusoma Good morning/Afternoon n.k

Wakati wenzetu Waarabu wanatumia Asalaam Alleikum!

Yaani rahisi kabisa
 
Hivi muasisi wa hii salamu ni nan ?Kwan haina tija na imekaa kiutumwa tumwa hivi.Kama inawezekana wizara inayohusika na mambo ya kiutamaduni walitazame na hili tuwe na salamu nyingne ya taifa ukiondoa hizo za kidini.Nakumbuka nilishawahi kugombana na mama mmoja njiani kisa hiyo salamu ya shikamoo.
 
Hiyo salam naamini imemsumbua karibia kila mtu katika makuzi yake. .ukiwa mtoto inajulikana wazi, ni yupi anastahili shikamoo, na yupi hastahili. Na huyo asiye stahili manaake ni mtoto mwenzio kwahyo mnatazamana tu.

Kuna kaumri flani kanafikaga yani unashindwa kabisa kujua yupi ni wa shikamoo na yupi ni wa habari yako. Na wote unatakiwa kuwasalimia😅
 
Bro angu ras alishatuambiaga home shkamoo ni salamu ya kishamba, salamu yetu ni amani na upendo, unajibu idumu milele, na ukimjia na shkamoo yako haitikii.😀
 
Yani ile kuna watu unamwangalia unashindwa jua ni mkubwa ama mdogo,,,nimpe salamu aina gani

Nsipopata jibu hapo nakula bati
Hii kitu imenichosha kuna watu ni ngumu kufahamu ni mkubwa au mdogo
 
Kusalimia inaonekana kama inawapa watu shida sana.

Mimi awe mdogo ama mkubwa akitaka shikamoo nampa kwa sababu hainipunguzii wala kuniondolea chochote.

Kwenye jamii ama kabila letu, mkubwa anaweza kuanza kumsalimia mdogo ama baba akamsalimia mtoto ama mama akamsalimia mtoto na ila anaanza na salamu ya kuitikia, mfano, shikamoo inatolewa na mdogo, mkubwa anaitikia marahabaa, sasa kikwetu mkubwa anaweza kuanza na marahabaa wewe ukamalizia shikamoo.

So sisi hatuna ulazima nani aanze, ila salamu lazima ipo.

Mtu kumpa shikamoo inakuuma nini? Polepole alisema, mpe shikamoo hata 9 kwa siku anaezitaka.
Kuna watu zina wachoresha hawazipendi
 
Back
Top Bottom